Kwa CHADEMA kuwa Rafiki na Chama cha Kikiristo cha UJERUMANI, Wanafuata Mrengo wa chama hicho?

Status
Not open for further replies.

WATANZANIA wengine wanafiki sana, yaani hapa wanainanga CDU lakini kila mwaka tunapokea misaada kibao kutoka Ujerumani inayoongozwa na CDU. Sasa si tungesema hatutaki hiyo misaada maana CDU ni chama cha Kikristo??

Hivi unajua serikali ya CDU imewapa hifadhi Waislamu kutoka Somalia,Uturuki n.k kiasi gani?? mbona hatusemi msiende huko kwenye nchi inayoongozwa na chama cha CDU??
Bajeti yetu ina upungufu wa karibu 40% na wanaojalizia hiyo 40% ndio hao CDU, twapokea tena tukitabasamu sana na tunaomba zaidi, ila leo hatutaki kushirikana nao hata kwa ushauri eti kwa kua ni Ukristo.

Hivi chama cha Kikomunisti Cha Uchina (CCP) wanapinga uwepo wa MUNGU, na ukiwa unaamini MUNGU uwe Mkristo au Muislam ukijulikana unafukuzwa uanachama wa CCP. Wao CCP ni marafiki wa CCM sasa unataka kutuaminisha kuwa CCM nao ni watu wanaopinga uwepo wa MUNGU ndio mana wanatajwa kulipua watu kwa mambomu na risasi?? CCP kinatajwa kukiuka haki za binadamu sasa je na CCM ni hivyo ndio mana Waalimu wakidai nyongeza wanatishwa?? au ndio mana wazee wa East Africa hawajalipwa hadi leo??

Acga ushabiki na tulia jiulize ushirika wa CDU na CHADEMA ni kwenye maeneo gani?? au CCM na CCP ni kwenye maeneo gani???
 
Tungewekewa katiba au ilani ya uchaguzi ya CDM tungepata majibu ya udini, ukabila wa CDM
 
Hoja ni balozi anayewakikisha nchi kujihusisha na ukada wa chama ndani ya nchi anayowakilisha. Na hapa CCM mtueleze CHINA inahusikaje na kulipua mabomu kule Arusha. Je lengo lilikuwa kubomoa CHADEMA kwakuwa wanapinga mikataba ile mingi ya siri, ya kifisadi lakini yenye maslahi kwao?
HOJA HAPA URAFIKI WA CHINA NA CCM UNAMANUFAA KWA WA TZ Wote AU ni kwa ajili tu ya WACHINA NA MAFISADI wanaokihodhi CCM? including kuokoa mtoto asinyongwe. Na je URAFIKI WA CHADEMA NA CDU AU CSU UMELETA MADHARA GANI KWA WA TZ?
 

Hoja dhaifu, nani kakuambia kuwa CDM na CDU wanashirikiana katika ukristo? Kwani ni vimesajiliwa kama vyama vya kidini au kisiasa? Je wajerumani wamekulalamikia kuwa wanabaguliwa kutokana na dini zao na chama tawala hivyo uwasaidie watanzania kuachana na chama chochote rafiki na CDU? Kama ndo hivyo; vip ccm ni chama cha kikomunist? Mbona kimeazima mpaka balozi kuwasaideni kupiga kampeni? Fikira zangu ni kwamba kwenye siasa kuna maslahi mapana zaidi ya dini!
 
Wacha ushamba wa siasa za kimataifa chama cha CD si cha kidini ni jina tuu. Pia angalia CCM ina urafiki na chama cha kikomonist cha China ambacho hakiamini uwepo wa MUNGU, je utasema nacho kinafuata imani hiyo ya Wachina?
 
Chadema ni chama killicho waz bila maficho kutekeleza sera za kanisa alichokisema mheshimiwa kina ukweli sema tu ubishi na ushabiki tu hamna kingine.......
 
Ponda kapigwa na serikali ya ccm ambaye mw\kit wake tunajua ni din gan je ccm ni wakristo wote kwa kumpiga ponda simama jitambue muache propaganda
 

toa uongo wako hapa. ujerumani wanatoa misaada gani kwa serikali zaidi ya kusaidia CHADEMA tu?
 

haya ndo madhara ya kulewa viroba. umesoma lakini hujaelewa. CDU maana yake ni Christian Democratic Union. chadema kwa tafsiri ya uswazi ili wafanane nao ni Christian Democratic Movement (CDM)
 
Chadema ni chama makini.Suala la kushirikiana na chama chenye itikadi tofauti siyo tatizo,dunia hii ya sasa huwezi ukaishi kama kisiwa.Au umesahau kwamba Nyerere alikuwa ni rafiki wa Soviet Union,Cuba na North Korea ambazo zilikuwa zinafuata itikadi ya UJAMAA na wakati huo huo akiwa ni rafiki wa Raisi John F kennedy wa USA ambayo inafuata itikadi ya UPEPARI.Leo CCM bado inashirikiana na China ya kisoshalist wakati Tz ujamaa umebaki kwenye makaratasi tu ya CCM.Mbona huhoji Raisi wako kikwete kwenda nchi za kiislamu kuomba misaada wakati TZ si nchi ya kiislamu?Jambo la msingi ndugu yangu hata kama unashirikina na yeyote la msingi ni kuhakikisha maslahi ya taifa hayawekwi rehani.Kumbuka CHADEMA ni chama cha mlengo wa kati(LIBERALS)hivyo wanaweza kushirikiana na yeyote pasipo kuhatarisha maslahi ya nchi.
 
hebu ainisha hzo sera za CDU zinazopandikizwa nchini otherwz kajpange..omba wanalumumba wakuelekezee namna ya kutunga uongo uonekane ukweli..
 
Hoja yako nini?!!chama kuwa na chama rafiki ktk nchi nyingine tatzo ni nini! Bac tufunge baloz zet katka nchi za zinazotawaliwa na sharia i mean nchi za uarabuni kama katib yetu hairuhusu. Ila njaa bana!!
 
Umeuliza swali zuri Elton John Ritz...nadhani ungemwambia huyu Elton John mwenzio mleta thread atuambie CHADEMA wanashirikiana na chama hicho kwenye maeneo gani?
Akili za Bavicha utazijua tu kwa michango yao haya nenda mtaa wa Ufipa ukachukue viroba vyako.
 
Nchi hii sikuzote ukisema ukweli sio unaonekana hufai,mchochezi ktk jamii lakini mm siachi kusema ukweli,kwasababu ndivyo nilivyo umbwa namutanichukia kweli,kama ponda anavyoonewa na serikali hii dhalimu kwa sababu kasimama kwenye ukweli
 
toa uongo wako hapa. ujerumani wanatoa misaada gani kwa serikali zaidi ya kusaidia CHADEMA tu?

Wewe jamaa wa ajabu sana yaani hujui kua bajeti ya nchi yetu inachangiwa na Ujerumani??? Hii ni aibu sana

Sasa naanza kujua ni mtu wa namna gani asiyejua hata abc za Nchi yake.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…