Kwa CV hii ya Msigwa! Je, ni eligible kuweza kusimamia maliasili na utalii??

Status
Not open for further replies.
 

Unajua ukiwa unaandika uwe unashirikisha kichwa chako, napata shaka na kiungo unachotumia kukifikirisha unapokuwa unaandika. Unasema eti Mrema aliweza kuongoza wizara ilhali hakuwa na shahada, hivi unaeza kufananisha uhalifu wa kupindi cha 90s na kipindi cha sasa??? mlete Mrema wako sasa hivi uone atakavyo tokota. Elimu ina nafasi kubwa katika kuhakikisha mtu ana discharge duties zake effectively, tusipende kupotosha hapa kisa tu ametajwa Msigwa! wakatii humu humu jukwaani mmekuwa mkihoji elimu ya Nape, Mulugo n.k
 


Nilikuwa najua ana CV ya kutisha kwa jinsi alivyomzungumzaji mzuri bungeni huyu jamaa kumbe hata A level hakusoma?Kweli kwenye siasa Elimu haina nafasi sana ni juhudi zako tu za kushawishi walalahoi. Na hiyo B.MINISTRY ndiyo nini?
 
hivi kunakilaza zaidi ya yule aliyepata zero kidato cha sita.
Wakati watu wazima wanaongelea Akili, na wewe unaongelea mitihani nakufananisha na mtoto wa mwaka mmoja.
Look around you, dont be like a damn robot.
Hata mkiwekewa picha hamuelewi what the people of this country are going through!
What the hell are you people!!
 
Nilikuwa najua ana CV ya kutisha kwa jinsi alivyomzungumzaji mzuri bungeni huyu jamaa kumbe hata A level hakusoma?Kweli kwenye siasa Elimu haina nafasi sana ni juhudi zako tu za kushawishi walalahoi. Na hiyo B.MINISTRY ndiyo nini?
Kama hiyo huijui basi wewe ndio huwezi hata kuwa mjumbe wa kamati ya shule ya msingi.
 
Hao maprofesa na wenye PhD hapo CCM wameifanyia nini nchi hii zaidi ya uoga,kutokuthubutu.rushwa na kuila nchi kwa kwenda mbele.?CV ya mtu its not a big deal kama unavydhani....Uzalendo kwanza!
 
msigwa nyerereism ypo kwa maslai ya wakatoriki


Nianze tu kwa kusema Msigwa hawezi kuwa pale alipo kwa maslahi ya Wakatoliki kwa kuwa mbunge ni wa wananchi wote. Hilo la kwanza. Lakini la pili ni kwamba Msigwa siyo Mkatoliki na kwa sababu hiyo dhana iliyojengwa haina mashiko. Baada ya maelezo hayo ninaomba kukuuliza wewe Salumu Mitema swali. Ni nani yuko kwa maslahi ya Waislamu? Je, kama kila mbunge au kiongozi akiwa mahali kwa maslahi ya dini yake wapagani nani atawasemea? Jamani ndugu zangu, mtu kumudu stadi za kUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU (KKK) hakumpi uwezo wa kuchangia kwenye jukwaa la JF. Hapo kwenye red siyo Kagame, Kabuta na Kenyatta.
:cheer2:
 
Hao maprofesa na wenye PhD hapo CCM wameifanyia nini nchi hii zaidi ya uoga,kutokuthubutu.rushwa na kuila nchi kwa kwenda mbele.?CV ya mtu its not a big deal kama unavydhani....Uzalendo kwanza!

Sidhani kama hii ni hoja. Kama maprofessor wa serikali ya CCM hawana tija, unafikiri kuwa hata wataalam wa CHADEMA watakuwa hivyo?

Au unataka kumaanisha kuwa CHADEMA hakuna wasomi wanaoweza kukamata nafasi nyeti na wakafanya vizuri zaidi ya wasomi wa CCM?!
 
du mkuu kumbe chadema kunamagarasa hivi sasa kwa elimu hizi tegemeeni vurugu mwanzo mwisho wataongea nini sasa.

Kumwita mtu garasa/garasha inategemea na unavyo define, mbona hawa ndio wanaokimbiza? Serikali yote badala ya kufikiria maendeleo inafikiria kuiua CHADEMA ambayo wewe unasema ina magarasa, hata sifa mojawapo ya kupandishwa cheo serikali au ili uchaguliwe kua kiongozi magambani, unesha jinsi gani ulivyo au utakavyo iua CHADEMA hiyo yenye magarasa, kumbe kuna wasomi walioenda kukariri formula, laws za watu lakini hawana uwezo wa kuzitafsiri hizo laws na formula ili upate maendeleo, hivi mkuu wa kaya nae si ni mchumi? Linganisha sasa, elimu yake na matendo yake. Nawashauri mwende pia mkatafute CV ya Paul Kagame.
 
Hapa hatukawii kusikia hizo nondo za All Africa Bible College, from 1999-2004 kwavile ni miaka mitano basi elimu yake ni Equivalent to PhD!
 
Hivi hao wenye shahada wamelifanyia nini taifa? Mbona ndo mafisadi wakubwa wa rasilimali zetu? Ccm yote imejaa wapumbavu!

usimsahau baregu nae Ni msomi toka kwa nyerere, itoshe Tu kusema wasomi wameiangusha nchi hii bila kushirikisha vyama
 

Hahahahaha... mkuu, kweli wewe una dharau! umesema KKK sio standard ya mtu kuweza kuchangia JF?

Umenichekesha kweli!
 
Wewe kilaza mbona mgumu kuelewa? mleta mada amesema waziwazi umuhimu wa raslimali watu katika kusukuma gurudumu la maendeleo, hivyo tuanze kujadili hao watu wenyewe kabla ya kuwapa fursa!

"I failed in some subjects in exams, my friend passed in ALL. He is now an engineer in Microsoft and I am the OWNER of Microsoft" Bill Gates.
 
Mkuu naona hukunisoma vizuri..nimejibu hii hoja kulingana na mleta mada alivyoiweka na kutaka kutuaminisha kwamba CV ni muhimu kuliko lolote ktk ujenzi wa nchi.Hapo nimetanabaisha kwamba mbona CCM ina watu wenye PhD na maprofesa kibao na bado wanafeli?Sababu kubwa sii CV ni kutokuwepo uzalendo tu na kukumbatia uzembe na ubabaishaji?
 

Hao wenye shahada mbona walishindwa kuikoa Tanzania yetu kutoka katika mikataba ya Kitapeli na ya Kinyonyaji kutoka kwa Wawekezaji wa Kigeni??
 

Hapo sasa! Kuna msemo nilijifunza shule ya msingi zamani unasema: "Heri kijana maskini mwenye hekima kuliko mzee mfalme mpumbavu."
 

Lakini si hoja ilikuwa kwamba Msigwa hajasomea utalii au umesahau ulivyoanza? Ujue nimekula logic mpaka basi na hivyo huweza kuleta conclusion ambayo ni 'unintelligible' nikaikubali mpaka iwe supported by premisses.
 
ana mawazo ya kusaidia kuliko hao maprofesa wenu wasio wazalendo na wanaofikiria kwa urefu wao tu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…