Kwa Dar es salaam kuna maeneo ambayo viwanja vinaweza patikana Kwa laki 3?

Kwa Dar es salaam kuna maeneo ambayo viwanja vinaweza patikana Kwa laki 3?

Njoo na hiyo laki tatu uupate shamba eka moja miono,ulime mihogo ,ukivuna mara mbili,inatosha kununua kiwanja mbagala
 
Unapata vipo usibishe ila maeneo hayo ukinunua mvua ikinyesha huna wa kumlaumu umenunua kwenye makazi ya maji yaan juakali ukienda kununua unapaona pako safi kabisa lipia subiri mvua inyeshe uone ulichokinunua ndio utaelewa kwanini walikuuzia kwa bei hio
Umesema vyema. Miaka fulani tulitafuta kiwanja dar kila mtu anasema huoati chini million 5 asee watu wengi hovyoo na bure kabisaa na hawapendi wenzao wapate. Tulikuwa kupata kiwanja chini ya milion Cha kujenga vyumba vitatu na sebule sema palikuwa na gema la kusawazisha kwa 50,000 tu. Ila kuna la kujifunza kuwa ukitafuta kwa haraka hupati.
 
Kwa Dar es salaam kuna maeneo ambayo viwanja vinaweza patikana Kwa laki 3?

Upimaji usiwe Kwa foot

Tuseme mfano Kwa 20m Kwa 20m Kwa kuanzia.

Kigezo eneo lolote ila iwe ndani ya Dar

Wajuzi mtujuze📌
Nenda Boko mlemela. Unaweza kuja kunishukuru
 
Pembezoni mwa Dar huko vipo tena kuna jamaa alikua anadalia ni laki 1 tu sio laki 3 ila ni mbali huko hata huduma za jamii hakuna kukavu au unafikiri Dar ndogo km inavyoonyeshwa kwenye ramani kwamba unaweza ukaizunguka siku 1 tu ukaimaliza yote?
Hakuna eneo hilo dar... labda laki 6 tena pwani kunaitwa Magodani
 
Back
Top Bottom