Naona watu wengi mnamshambulia mleta mada, ukweli ni kwamba Paul Kagame na Timu zake (Majeshi) wako vizuri ktk masuala ya vita na ujasusi. Endapo kama kweli hao majirani zake wanapanga au wanataka kuanzisha vita dhidi yake, basi wanatakiwa Wajipange sawasawa kabla ya kuanzisha mtiti dhidi ya Paul Kagame. La sivyo wanaweza wakajikuta wapo matatani sana huku Kagame akiendelea kuneemeka kutokana na uchokozi wa majirani zake.
Kumbuka: Kushinda vita kunachangiwa na sababu nyingi, ikiwamo na Intelijensia kali, ari ya wapiganaji, ubora wa zana/silaha za vita, etc. In short Majeshi ya Bw. Paul Kagame yana Intelijensia kali sana, pia wako vizuri ktk suala zima la Manpower & Logistics ukilinganisha na hao wapinzani wake. Wingi wa Wapiganaji au wingi wa silaha siyo vigezo vizuri sana vya kuweza kushinda vita katika dunia hii ya leo ya Sayansi na Teknolojia ya hali ya juu, hoja ya msingi ni Ubora walionao hao wapiganaji, ubora wa silaha wa silaha za kupigania vita, ari au morali ya wapiganaji pamoja na suala zima la Logistics. Kwa hiyo msiidharau Rwanda licha ya udogo wake wa eneo la kijiografia iliyo nayo, "Ukubwa wa Pua siyo wingi wa kamasi."