Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Mwaka 2020 katika Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, nikiwa nimevutiwa na Sera ya CHADEMA kuhusu kuanzisha utawala wa majimbo nchini Tanzania niliandika uzi kuonesha namna gani utawala huu utafanikiwa katika kuharakisha maendeleo ya Tanzania
Uzi wenyewe huu hapa👇
www.jamiiforums.com
Ikiwa imepita miaka 5, napenda kusisitiza kuwa suala la kugawa majimbo ya Uchaguzi ili kuongeza idadi ya Wabunge, halina maana yeyote ya msingi katika kuwaletea Wananchi Maendeleo.
Ili Tanzania tupate maendeleo ya uhakika kwenye nchi yetu na Wananchi wetu hatupaswi tena kuwaza kugawa majimbo ya uchaguzi ili kuongeza idadi ya Wabunge bali tubapaswa kufikiria kuanzisha utawala wa majimbo kama nilivyopendekeza katika uzi wangu wa mwaka 2020.
Kutokana na ubovu wa Katiba yetu, mfumo tulionao sasa hauwezi kuleta maendeleo ya uhakika kwa wananchi kwa sababu zifuatazo:
1. Wananchi hawataweza kupata Viongozi wanaowajibika kweli kwao kwa sababu mtu anayeteuliwa na mamlaka nyingine hawezi kuwajibika ipasavyo kwenu ila atawajibika zaidi kwa mamlaka iliyomteua. Madhara ya haya leo ni kwamba, Wakuu wa Mikoa hawawezi kuwagomea Mawaziri au Rais wakiamrishwa kutenga fedha kwa shughuli za CCM badala ya shughuli za kuwahudumia Wananchi. Mfumo wa Majimbo utahakikisha Viongozi wa Majimbo wanatumia fedha wanazokusanya kwa Wananchi wao kuwahudumia kwa maji salama, shule bora, barabara nzuri za uhakika na masuala mengine ya kimaendeleo.
2. Kamwe hatutaweza kuwa na Consistency kwenye huduma bora kwa Wananchi. Hii ni kwa sababu mfumo wa sasa unakusanya fedha katika kapu moja na kuzitawanya maeneo mengine kwa namna wanavyojisikia. Hasara ya mfumo huu ndo haya tunayoona mfano kwenye shule zetu na hospitali zetu ambazo zinategemea kupata fedha kutoka mfuko mkuu wa Serikali.
Endapo Majimbo yakijitegemea ikiharibika x-ray machine ya hospitali ya Jimbo hakutatokea ucheleweshaji katika kuitengeneza maana fedha za kutengeneza zitakuwepo jimboni badala ya kutegemea kuomba na kupewa kutoka Serikali Kuu.
Endapo majimbo yakijitegemea hatutaona kuchelewa kukarabatiwa barabara au kujengwa kwa miondombinu kwa sababu fedha husika zitakuwa katika mfuko wa jimbo husika na kupatikana haraka sana pale zinapohijtajika. Kwa hali ya sasa ni haiwezekani barabara na miundombinu kutunzwa vizuri na kukarabatiwa kwa wakati kwa sababu unahitaji kwenda kuomba hela kwenye mfuko mkuu wa Serikali na zifuate mchakato mrefu ili zije kukujudumia wewe mwenye uhitaji wa haraka. Ndo mana tunaona hakuna Consistency kwenye huduma bora kwa wananchi.
3. Tutaendelea kulea na kujenga Viongozi wazembe wasiotumia maarifa vizuri ili kuwapatia maendeleo Wananchi wao. Mfumo wa sasa hautengenezi suala la Viongozi na Watendaji kuumiza vichwa kutafuta vyanzo vya mapato sahihi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wao vizuri. Hii ni kwa sababu wote wanategemea mfuko mmoja wa Serikali. Hawawezi kuwa creative, hawawezi kuwa innovative na kamwe hawawezi kuwa pro active.
Endapo tukiwa na mfumo wa Majimbo Viongozi watalazimika kuwa creative, innovative na pro active kwa sababu wakilala it's obvious majimbo yao yatakosa mapato ya kujiendesha.
Naomba kuwasilisha.
Uzi wenyewe huu hapa👇
Ufafanuzi: Je, kuna Majimbo yatashindwa kujiendesha kwenye mfumo wa Majimbo?
SWALI NI: JE, MFUMO WA MAJIMBO UTALETA UKABILA NA KUFANYA BAADHI YA SEHEMU TANZANIA KUTOKUWA NA MAENDELEO? Amani iwe nanyi wadau! Leo napenda kuwajibu wana CCM wanaosema mfumo wa Majimbo utachochea ukabila na kusababisha baadhi ya maeneo kutokuwa na maendeleo, Ukweli ni kuwa kamwe mfumo wa...