Kwa dhati nalipongeza Kanisa Katoliki Parokia ya Msimbazi kwa kudhibiti maadili wakati wa ibada

Kwa dhati nalipongeza Kanisa Katoliki Parokia ya Msimbazi kwa kudhibiti maadili wakati wa ibada

Matongee

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
1,056
Reaction score
2,729
Wakati fulani kwenye maisha yangu ya dhambi nilitokea kumpenda msichana aliyekuwa akiabudu kwenye kanisa moja la katoliki pale Msimbazi. Huyu binti alikuwa mkatoliki safi aliyenyooka. Ikawa ananisihi sana hata kama mimi sio mkatoliki niwe najiunga nae mara moja moja kwenye ibada kanisani kwao. Baada ya danadana nyingi kuna siku nikaamua ngoja niende nikasali. Nakumbuka hata sikumjulisha na ulikuwa ni uamuzi wangu binafsi.

Kwa kweli nilivyongia kanisani misa ya kwanza nilipata na mshangao mkubwa na nikatafakari sana kuhusu kanisa katoliki. Ni tofauti kabisa na nilivyokuwa nilifikiri. Kwanza pale Msimbazi hawaruhusu kabisa matumizi ya simu ndani ya ibada. Waumini wote huzima au kuweka silent simu zao. Hii ni tofauti kabisa hata na kanisa nililokuwa nikiabudu. Makanisa mengi siku hizi wamenasa kwenye mtego wa teknolojia.

Wengi wanajidanganya kuruhusu simu kwa kigezo cha kusomea biblia kwenye simu. Shetani kwa ubunifu wake akajua kabisa akiwaletea hii hoja ya biblia atafanikiwa kulivuruga sana kanisa kwasababu wengi wataanza kuchat na kurekodi matukio. Inafikia hatua watu wanasali kuna mpuuzi anachukua video. Kanisa la Msimbazi wameukwepa huo mtego wa shetani.

Ingawa sio sheria ya kanisa lakini pale Msimbazi kuna safu ya wanaume na wanawake.. yaani jinsia hizi mbili kila mmoja ina upande wake. Lakini kwa sababu sio rasmi inatokea kuona wanawake wachache upande wa wanaume na wanaume upande wa wanawake.

Mara nyingi wanakuwa ni wale wachelewaji. Huu utaratibu unafanana na waislamu ambao ni utaratibu bora kabisa kimaadili. Binafsi nikikaa tu kwenye kiti kwa dakika 20 bila kujishughulisha lazima isimame.. sasa chukulia umebanana na pisi iliyonona ibadani si concentration na focus inapotea? Kanisa katoliki Msimbazi nawapongeza.

Baada ya ibada nilifarijika sana na kujikuta nahudhuria mara kwa mara. Na kwa bahati nikapata manzi mwingine kulekule kanisani aliyekuja kusababisha nikaachwa na manzi wangu wa kwanza. Kibaya zaidi hata huyu manzi mpya tuliachana nikaanza kutangatanga.
 
Mbona huo ni utaratibu wa enzi na enzi wa makanisa yote ukiacha haya makanisa ya kisasa. Hakuna kutumia simu na kuna upande wa KE na ME.

Sema ukisoma na makanisa yasiyojitambua ndio watu wanarekodi hovyo hovyo. Sisi kwetu huku vijijini hakuna kurekodi, ukifika kanisani ulazima simu na tunakaa tofautitofauti.
 
Wakati fulani kwenye maisha yangu ya dhambi nilitokea kumpenda msichana aliyekuwa akiabudu kwenye kanisa moja la katoliki pale Msimbazi. Huyu binti alikuwa mkatoliki safi aliyenyooka...
Hata kwa upande wa mavazi pale kama umevaa ovyo ovyo wanakurudisha.Wanawake wanaopendelea kuvaa suruali na vinguo vya kubana(vinavyoonesha jiografia ya mwili😆😆) huwa hawaruhusiwi kuingia kanisani au wengine huambiwa wachukue khanga wajifunike kwanza ndio waruhusiwe kuingia ndani kanisani
 
Wewe nimalaya nakushauri tuko huku uende kule feel free church kwa masanja
Hapana. Nilishaacha hayo maisha na kurudi kundini. Ninapambana sana kuziepuka dhambi ingawa kama binadamu huwa wakati mwingine nashindwa.
 
Naona Shetani unatoa ushuhuda ulivyovutwa kwenda kanisani, kavamia kanisani ukaanza kufanya mambo yako kabla pepo haujaachwa mwenyewe kama ulivyoenda.
 
Hata kwa upande wa mavazi pale kama umevaa ovyo ovyo wanakurudisha.Wanawake wanaopendelea kuvaa suruali na vinguo vya kubana(vinavyoonesha jiografia ya mwili😆😆) huwa hawaruhusiwi kuingia kanisani au wengine huambiwa wachukue khanga wajifunike kwanza ndio waruhusiwe kuingia ndani kanisani
Pale Msimbazi Centre nikija Dar nitaenda tena kuabudu. Ni sehemu yenye upako sana.
 
Mbona huo ni utaratibu wa enzi na enzi wa makanisa yote ukiacha haya makanisa ya kisasa. Hakuna kutumia simu na kuna upande wa KE na ME. Sema ukisoma na makanisa yasiyojitambua ndio watu wanarekodi hovyo hovyo. Sisi kwetu huku vijijini hakuna kurekodi, ukifika kanisani ulazima simu na tunakaa tofautitofauti.
Hapana. Kuna makanisa yenye majina makubwa ila wanaendekeza upuuzi na kunasa kwenye mtego wa teknolojia.
 
Naona Shetani unatoa ushuhuda ulivyovutwa kwenda kanisani, kavamia kanisani ukaanza kufanya mambo yako kabla pepo haujaachwa mwenyewe kama ulivyoenda.
Mimi ni mdhambi ambaye napambana kuutafuta uso wa Mungu.
 
Mimi ni mdhambi ambaye napambana kuutafuta uso wa Mungu.
Safi sana. Ukishaijua nafasi yako unakua umefanikiwa kupiga hatua nyingi kutoka kwenye huo Mtego.
Rudi pale Msimbazi, omba kuonana na Paroko uingee naye, atakusaidia sana.
 
Safi sana. Ukishaijua nafasi yako unakua umefanikiwa kupiga hatua nyingi kutoka kwenye huo Mtego.
Rudi pale Msimbazi, omba kuonana na Paroko uingee naye, atakusaidia sana.
Niko nje ya Dar ila nikirudi nitaenda pale kwasababu siishi mbali na pale.
 
Wewe nimalaya nakushauri tuko huku uende kule feel free church kwa masanja
Hapana, siyo sahihi kumtamkia hivyo. Kanisani ndiyo mahala sahihi kwetu wadhambi. Hivyo huna sababu ya kumwambia atoke, pale ni nyumbani mwa Baba yake, hivyo yupo mahala sahihi. Kikubwa ni kumuombea na kumshauri apate Mwongozo wa Kiroho kutoka kwa viongozi wa Kiroho.
 
Umeongea kwa busara sana.
 
Kanisani ( katoliki) sijawahi kukutana na utaratibu wa kutenganisha wanaume na wanawake.

Ila watu wanajitenga wenyewe automatically, Kuna safu wanakaa zaidi jinsia ke na Kuna safu utawakuta zaidi jinsia Me
 
Ni utaratibu mzuri
 
Back
Top Bottom