Kwa Gavana tuliyenaye, sikushangaa nilipoona habari ya shilingi ya Tanzania kufanya vibaya zaidi Duniani

Kwa Gavana tuliyenaye, sikushangaa nilipoona habari ya shilingi ya Tanzania kufanya vibaya zaidi Duniani

Tatizo kumbe ni chuo alichosoma? Kwani UDSM ina nini cha ajabu dhidi ya MU?

Acheni kukariri na dharau vyuo vyetu.
Shida sio chuo. Shida ni hicho chuo kuwahi kusemwa vibaya kipindi fulani. Ndo hoja ya mchangiaji.
 
Exposure sio lazima kwenda nje au kuajiriwa nje

Viwanda mfano vya china na japan vya magari na pikipiki vina idara ya research and Development yaan8 R&D wanajikita tu kwenye research ku develop new products bila kukanyaga nchi yeyote

Exposure waweza ipata tu kwenye simu yako au compter bila kwenda popote duniani vyote viko online
Jipige kifua sema mini ni mjinga

Hao China na Japan unaowasema hapo ndo wanaongoza kwa kuwapeleka wasomi wao nje ya mataifa yao kupata uzoefu na kuiba teknolojia mbalimbali kisha wanarudi kwao kufanya hayo unayoyaona.

Kama hujui Vyuo vya Marekani na Ulaya vimejaa watu kutoka Urusi na Asia. Na hawaendi huko kwa bahati mbaya ni mkakati wa kupata hiyo Exposure na kwenda kuifanyia kazi nchini kwao.
 
Jipige kifua sema mini ni mjinga

Hao China na Japan unaowasema hapo ndo wanaongoza kwa kuwapeleka wasomi wao nje ya mataifa yao kupata uzoefu na kuiba teknolojia mbalimbali kisha wanarudi kwao kufanya hayo unayoyaona.
Hujui kitu wewe wajapan na wachina wanaongoza duniani kupeleka wasomi nchi zilizoendelea kutafuta fursa za maisha yao wakifuatiwa na wahindi

Kwa Africa nchi zinayoongoza kupeleka watu wao kusoma ulaya na marekani watafute fursa kule ni wa Nigeria wakifuatiwa na wa Ghana

Kwa Afrika mashariki wakenya ndio wanashika nafasi ya kwanza mjinga wewe
 
5 March 2025

Gavana Tutuba - Sababu riba kubwa Tanzania zatajwa


View: https://m.youtube.com/watch?v=0mdwEixj1GU

Kwa mwaka wa 2024 deni letu la taifa la takriban shillingi trilioni 100, lipo katika uwiano wa takriban asilimia 44% ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55%unaokubalika kimataifa’’

-Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba amekiri kuwa deni la taifa hilo linazidi kukua ila bado lipo chini ya ukomo wa uwiano wa deni la taifa na pato la taifa unaokubalika kimataifa wa asilimia 55%.

-‘’Deni letu ni himilifu kwa muda mfupi wa kati na mrefu na lipo ndani ya viwango vinavyokubalika kimataifa.’’

-Kauli hiyo imetolewa na wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Florian Kaijage.

Hata technical terms zinamshinda

Hawezi elezea ‘direct financing’ and ‘indirect financing’

Primary market and Secondary market

Financial intermediaries ‘anaita bank za reja-reja; kama basic concept zinamshinda ndio technical aspects za kazi ataweza.

CB za Africa haziitaji kuwa na governor kipanga, wanafuata rules tu za usimamizi Basil 1, 2, 3
Kuwa lender of last resort
Kuishu government.

Lakini shughuli ya kuchochea uchumi toka nchi ipate uhuru aijawahi kuwa na governor wa aina hiyo, wote hovyo tu ndio maana tumaskini.

Anyway they are all the same serikalini awachekani, asilimia kubwa ndio sampuli yake.

Tanzania nchi ya ajabu sana utakuta msomi anasifiwa, ukimsikiliza salaleh. Halafu unaweza kuta lecture tu hana jina lolote anaongelea topic hiyo hiyo ana depth mpaka unajiuliza sasa huyu anaejua hivi sio mtaalamu huko serikalini.
 
Likimjia wazo la kuutaka urais utasikia tu anatunukia ya heshima kutokea UDOM. 😀
Sio UDOM huyo Gavana zao la MU enzi inaitwa Institute of Development Management-mzumbe (IDM) 😹
 
Hata technical terms zinamshinda

Hawezi elezea ‘direct financing’ and ‘indirect financing’

Primary market and Secondary market

Financial intermediaries ‘anaita bank za reja-reja
Kasoma elimu zote za digrii kiingereza sio kiswahili

Haya wewe mbabe wa kiswahili tupe tafsiri ya kiswahili ya neno YouTube

YouTube kiswahili inaitwaje ? Bwege wewe
 
Ndo akili zenu zinavyowaza huko CCM. Kila kitu mnaleta tafsiri za wivu na chuki wakati watu wanaongelea masuala serious kwa Taifa.

Hao Mtei na Nyirabu walikuwa magavana kipindi gani? Idadi ya wasomi ilikuwaje hapa nchini?

Unaweza linganisha na sasa ambapo tuna Watanzania wabobezi wa uchumi na masuala ya fedha wa kutosha hadi wengine wanafanya kazi kwenye Mashirika Makubwa kabisa duniani huko?

Tatizo kila kitu mnawaza ulaji ndo mana mkiambiwa ukweli mnakimbilia eti wivu. Nyie ni majinga sana kwa kweli.
Utakufa maskini wewe na kijiba cha roho sababu ya wivu. PhD ni nini kwani? Kwani kuna PhD ngapi zimepewa kazi na zimefeli?

Yale ma PhD ya akina Prof Osoro na Dr Mruma yametusaidia nini kwenye madini?? Hawa waliandika ripoti kuwa ACACIA inadaiwa USD 190 Billion sawa na Tsh 450 Trillion kwa kodi waliyokwepa. Je tulipata hizo hela kutoka ACACIA au Barrick?? Mbona wakienda ICSID wanasambaratishwa na wanasheria wadogo tu wenye LLM?

Mwaka 2005 Govenor wa Bank alikuwa Dr Balali na Tsh ilikuwa 1,050 kwa USD na akamuachia Prof Benno Ndulu (PhD) kuanzia 2008 hadi 2018 na wakati Benno Ndulu anatoka Tsh ilikuwa 2,100 kwa USD.

Kama PhD zinazuia Tsh isiporomoke niambie hizo za Balali na Ndullu kwa nini hazikuzuia ??

Acha wivu, fanya kazi, ukiwa na sifa utaitwa
 
Kwa miaka mingi sana, nimekuwa mfuatiliaji wa CV za Magavana wa Benki Kuu za nchi mbalimbali duniani.

Katika ufuatiliaji wangu, miaka yote kwenye mataifa mbalimbali, Magavana wa Benki Kuu wamekuwa wakiteuliwa wabobezi wa masuala ya Uchumi , Fedha au Sheria na wenye uzoefu wa kufanya kazi katika eneo la uchumi ndani na nje ya nchi zao. Pia wenye uzoefu wa kufanya kazi kwenye Taasisi mbalimbali za kifedha zenye historia ya kufanya vizuri kwenye masuala ya Fedha.

Kwenye mataifa mbaimbali, nafasi ya Gavana wa Benki Kuu inahusisha kuteuliwa watu wenye PhD katika masuala ya Uchumi, Fedha na Biashara au Sheria. Hata kama asipokuwa na PhD basi anapaswa kuwa mtu mwenye rekodi ya outstanding performance kwenye masuala ya Fedha, Uchumi na Sheria.

Kwa utafiti wangu mdogo, haya hayafanyiki kwa bahati mbaya. Gavana wa Benki Kuu anapaswa kuwa kichwa cha nchi kwenye suala nyeti la uchumi. Anapaswa kuwa mshauri wa mwisho pale nchi inapokuwa kwenye crisis yeyote ya kiuchumi.

kwenye kufanya haya anatakiwa awe mbobezi sana kwenye masuala ya uchumi. Anatakiwa kuwa na exposure kubwa sana ya kimataifa na kitaaluma katika masuala ya kiuchumi.

Nakumbuka wakati Emmanuel Tutuba anateuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu niliwahi toa maoni yangu kuwa ule haukuwa uteuzi sahihi.

Kwa haya matokeo ya shilingi yetu kufanya vibaya zaidi nadhani sasa niko sahihi nikisema uteuzi wa Tutuba kuwa Gavana wa Benki Kuu haukuwa sahihi. Ni bahati mbaya sana mamlaka za Uteuzi nchi hii hazihojiwi kutokana na kuwa na Katiba mbovu.

Angalieni wenyewe biography kwa kifupi za Gavana wetu wa Benki Kuu alafu linganisha na Magavana wa Mataifa mengine.

Hii ndo Bio ya Gavana wetu Tutuba
👇- Amesoma Diploma Mzumbe na Master kwenye chuo hiko tena kipindi kinachojulikana kuwa Chuo hiko hakikuwa Chuo chenye hadhi ya Chuo Kikuu hata kwa Tanzania. Zaidi kafanya kazi public sector tu tena Tanzania.
View attachment 3282699

Hii ndo Bio ya Gavana wa Benki Kuu Kenya👇
View attachment 3282700

Hii ndo Bio ya Gavana wa Benki Kuu Uganda👇
View attachment 3282701

Hii ndo Bio ya Gavana wa Benki Kuu ya Marekani. Hana PhD ya Uchumi ila angalia rekodi yake ya utendaji kwenye sekta ya Umma na sekta binafsi hasa kwenye firms zinazotambulika vizuri Marekani kwenye masuala ya Fedha na Mitaji👇
View attachment 3282704


Mwisho.
Ni hitimisho langu kuwa Tanzania tupambane sana kupata Katiba Mpya maana tutapata watu wasiostahili kwenye nafasi za juu hadi tutajikuta tunazikwa kabisa kimaendeleo na Kiuchumi.
Kipindi cha nyuma kusoma hizo Diploma unazo/unazoziita kwenye vyuo vya DIT/ Mzumbe/IFM ilikua mpaka upate ufaulu wa juu mfano point 12 kuliko sasa hivi vyuo vilivyoongezeka kwa cut point za 5 au 4 ( DD) Kijana anatinga Chuo Kikuu
Pia kumbuka tuna Miradi Mikubwa inatekelezwa ambayo inasababisa importation of Materials.. mfano SGR
 
Sio UDOM huyo Gavana zao la MU enzi inaitwa Institute of Development Management-mzumbe (IDM) 😹
Raisi mchapa kazi Mama Samia ni mhitimu wa chuo cha uongozi Mzumbe yaani IDM

Kwani kusoma IDM kuna shida,?

Dr Emmanuel Nchini pia kasoma IDM
 
Utakufa maskini wewe na kijiba cha roho sababu ya wivu. PhD ni nini kwani? Kwani kuna PhD ngapi zimepewa kazi na zimefeli?

Yale ma PhD ya akina Prof Osoro na Dr Mruma yametusaidia nini kwenye madini?? Hawa waliandika ripori kuwa ACACIA inadaiwa USD 190 Billion sawa na Tsh 450 Trillion kwa kodi waliyokwepa. Je tulipata hizo hela kutoka ACACIA au Barrick?? Mbona wakienda ICSID wanasambaratishwa na wanasheria wadogo tu wenye LLM?

Mwaka 2005 Govenor wa Bank alikuwa Dr Balali na Tsh ilikuwa 1050 kwa USD na akamuachia Prof Benno Ndulu (PhD) kuanzia 2008 hadi 2018 na wakati Benno Ndulu anatoka Tsh ilikuwa 2,100 kwa USD.

Kama PhD zinazui Tsh isiporomoke niambie hizo za Balali na Ndullu kwa nini hazikuzuia ??

Acha wivu, fanya kazi, ukiwa na sifa utaitwa
Balali alisoma Harvard, Balali alifanya kazi Mashirika ya Kimataifa.

Kwa hoja zako unakubaliana na hoja zangu kuwa Tutuba hafai kuwa Gavana wa BOT.
 
Kasoma elimu zote za digrii kiingereza sio kiswahili

Haya wewe mbabe wa kiswahili tupe tafsiri ya kiswahili ya neno YouTube

YouTube kiswahili inaitwaje ? Bwege wewe
Hiyo post ipo juu ya uwezo wako wa uelewa.

Reja-reja = retail

Sasa hela wanazochukua bank ni kwa sababu ya retail tu?

Hiyo habari yako ya YouTube ainihusu mimi naongelea banking finance.

Unajua kwanini nikasema neno sahihi ni ‘financial intermediary’ na si kutumia commercial bank.

Au hata unaelewa tofauti ya direct na indirect financing, google hizo concept; sikiliza clip uone alivyo na maelezo ambayo terminologies zinampiga chenga.

Alipoulizwa kwanini Tanzania aizalishi hata toothpaste majibu yake ndio ukawa mwisho wa kusikiliza interview yenyewe. Hajui hata role ya BoT kwenye kuchochea uchumi.

Idea yake ya commercial bank kupunguza NPL ni kuandika a good business proposal. Yaani default risk inaangaliwa kupitia a business plan, hakuna moral hazard, adverse selection, and so forth.

Yeye ni kilaza, wewe ni kilaza maradufu
 
Hiyo post ipo juu ya uwezo wako wa uelewa.

Reja-reja = retail

Sasa hela wanazochukua bank ni kwa sababu ya retail tu?

Hiyo habari yako ya YouTube ainihusu mimi naongelea banking finance.

Unajua kwanini nikasema neno sahihi ni ‘financial intermediary’ na si kutumia commercial bank.

Au hata unaelewa tofauti ya direct na indirect financing, google hizo concept; sikiliza clip uone alivyo na maelezo ambayo terminologies zinampiga chenga.

Alipoulizwa kwanini Tanzania aizalishi hata toothpaste majibu yake ndio ukawa mwisho wa kusikiliza interview yenyewe. Hajui hata role ya BoT kwenye kuchochea uchumi.

Idea yake ya commercial bank kupunguza NPL ni kuandika a good business proposal. Yaani default risk inaangaliwa kupitia a business plan, hakuna moral hazard, adverse selection, and so forth.

Yeye ni kilaza, wewe ni kilaza maradufu
Asipokuelewa kwa hizi nondo basi atakuwa ni chizi wa mwisho.
 
Hatuna gavana pale Benki Kuu ya Tanzania, huo ndiyo ukweli.

Gavana hawezi kufafanua jambo kwa lugha ya kiSwahili wala kiingereza. Gavana awe na uwezo wa hadhara kumsikiliza akiwa katika mkutano wa bodi hapa Dar es Salaam, au bodi ya Benki ya Afrika ADB makao makuu mjini Abidjan, au katika mkutano wa mwaka wa bodi ya Fuko la Fedha Duniani IMF Washington n.k

Gavana hawezi kuhojiwa na vyombo vya habari mambo mazito akatoa ufafanuzi

Gavana huyu hata hatisho kuwa katibu mkuu wa wizara yoyote nyeti na ngumu hapa Tanzania.

TOKA MAKTABA :
Gavana anatakiwa kuwa kama huyu aliyepita :

Bank of Tanzania Governor Benno Ndulu discusses financial inclusion in Tanzania and the Alliance for Financial Inclusion (AFI) in this video interview.


View: https://m.youtube.com/watch?v=-ji1pmmOypU


TOKA MAKTABA :

2023 AFI GPF - Plenary 4: Financial Inclusion for Shared Prosperity​

Emmanuel Mpawe Tutuba, Governor, Bank of Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=0pZ-VfgL0Ic

Hebu bagamoyo maliza tofauti zako na Emmanuel Tutuba. Nimesikia English yake sijaona broken yeyote katika maeneo aliyochangia kwenye huo mjadala wa financial inclusion prosperity.

Kama kuna màkosa yeyote hapa ya grammar basi andika ni dakika ya ngapi kwenye hiyo YouTube link.

Acheni kuchukia watu waliowazidi nyazifa na maisha, hatakusaidii chochote
 
Back
Top Bottom