Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 11,208
- 20,517
Juzi nilienda hospital moja ya serikali. Baada ya mlolongo mrefu wa huduma za hapa na pale, hatimae nikaelekezwa ilipo duka la dawa la hospital nkaenda kununua hapo.
Nikiwa hapo katika foleni ya kununua dawa Kuna wagonjwa waliokuwa mbele yangu na wengine pembeni yangu ambao walishindwa kumudu gharama za dawa hivyo kushindwa kujua wafanye Nini ili wapate hizo dawa wakaendelee na matibabu.
Kuna wengine waliokuwa wanawapigia simu watu wao kwa ajili ya kupata mchango wa kununua dawa lakini upande wa pili wa simu walijibiwa hawana hata mia.
Kuna ambao walikuwa wanalia kutokana na wagonjwa wao kuzidiwa hivyo zilihitajika dawa Kwa haraka na wakati huo hawana pesa mkononi.
Kuna ambao baada ya vipimo waliondoka majumbani bila dawa Kwa madai Kwa muda huo hawana pesa bali waende nyumbani wakatafute pesa mtaani wanavyojua wao halafu dawa watanunua huko huko mtaani.
Kwa muda mfupi niliokaa pale kusubiria foleni yangu ifike nipatiwe niliona ni Kwa jinsi Gani serikali yetu inatakiwa ifanye jambo kusaidia na kuokoa wananchi wake walio chini.
Tukija kwenye Bima ya afya Kwa wote sio magonjwa yote yanaingizwa kwenye Bima bali ni baadhi TU hivyo unakuta Bado mwananchi wa kawaida ambao ndio wengi kwenye nchi hii anateseka pale anapokosa pesa.
Hii nchi Ina Kila aina ya Rasilimali