Juzi nilienda hospital moja ya serikali. Baada ya mlolongo mrefu wa huduma za hapa na pale, hatimae nikaelekezwa ilipo duka la dawa la hospital nkaenda kununua hapo.
Nikiwa hapo katika foleni ya kununua dawa Kuna wagonjwa waliokuwa mbele yangu na wengine pembeni yangu ambao walishindwa kumudu gharama za dawa hivyo kushindwa kujua wafanye Nini ili wapate hizo dawa wakaendelee na matibabu.
Kuna wengine waliokuwa wanawapigia simu watu wao kwa ajili ya kupata mchango wa kununua dawa lakini upande wa pili wa simu walijibiwa hawana hata mia.
Kuna ambao walikuwa wanalia kutokana na wagonjwa wao kuzidiwa hivyo zilihitajika dawa Kwa haraka na wakati huo hawana pesa mkononi.
Kuna ambao baada ya vipimo waliondoka majumbani bila dawa Kwa madai Kwa muda huo hawana pesa bali waende nyumbani wakatafute pesa mtaani wanavyojua wao halafu dawa watanunua huko huko mtaani.
Kwa muda mfupi niliokaa pale kusubiria foleni yangu ifike nipatiwe niliona ni Kwa jinsi Gani serikali yetu inatakiwa ifanye jambo kusaidia na kuokoa wananchi wake walio chini.
Tukija kwenye Bima ya afya Kwa wote sio magonjwa yote yanaingizwa kwenye Bima bali ni baadhi TU hivyo unakuta Bado mwananchi wa kawaida ambao ndio wengi kwenye nchi hii anateseka pale anapokosa pesa.
Hii nchi Ina Kila aina ya Rasilimali
ndugu mdau, kwanza unisamehe kwa maelezo marefu,
lakini pili,
asante kwa maoni yako muhimu sana na kwa namna ulivyoguswa na changamoto za watu mbalimbali wakiwa katika harakati za kupata suluhisho na majawabu dhidi ya afya zao katika maeneo ya kupatia huduma yaani kwenye mahospitali na kwenye maduka ya dawa. Mwenyezi Mungu akubariki sana kwa ukarimu wako.
kwa maoni yangu,
nadhani katika yote uliyoyaeleza hapo juu, suluhisho lake ni kuu ni kua na bima ya afya. Full STOP. Tunaweza kubishana na kutofautiana kwa kila namna, lakini hitimisho la mabishano au tofauti zetu za maoni inafaa kua bima ya afya.
Nadhani hata ulivyokua ukishuhudia hekaheka za wagonjwa na wasaidizi wao katika kupata dawa, changamoto yao kubwa ni pesa ya kununua dawa tu. Na hii ikimaanisha huduma zingine zote wamepata kwa 100%, kwa mfano huduma za vipimo zipo vizuri 100%, huduma za dawa zipo kwa 100%, huduma za ushauri n.k ziko 100%, right?
Na,
haya yote yanamaanisha serikali sikivu ya ccm inafanya kazi kubwa na nzuri sana ya kuhakikisha waTanzania wote wanapata huduma bora sana na za uhakika za kiafya.
kama waTanzania,
ni muhimu sana,
kutambua umuhimu wa kua na bima ya afya ili kuondokana na adha ambazo ni wazi kila familia ya kitanzania inao uwezo kabisa wa kua na bima ya afya kwanza, kabla ya members wa familia hizo kua na iphones mojamoja tena za kisasa za mamilioni ya pesa.
inafaa kila familia kujinyima na kujifunga mkaja bara-bara na kuipa kipaumbele zaidi afya ya kila mwanafamilia kwa kua na bima ili kuondokana na kutia huruma au kua na unyonge ambao kabisa tunaweza kuondokana nao tukiamua.
hakuna haja ya kumsingizia au kumlaumu mwingine kwenye hili la afya. Tuchangie na kua na bima za afya kama ambavyo tunachangia sendoff na harusi na kupewa kadi za kwenda kuinjoy karamu na wana harusi ukumbini, tujinyime na kuchangia bima za afya kama ambavyo tunajinyima na kupeleka pesa kwenye vikoba ili baadae tuinjoy kua na pesa mingi n.k
Kumbuka,
changamoto zisizo husika au kugharamiwa na bima ni chache mno, na ni za changamoto nadra zinazohitaji tiba maalumu, za kipekee na mahususi zaidi.
Ni muhimu kua na bima za afya ili kuondokana na stress za kutokua na pesa tukiugua na badala yake tuwe na uhakika wa kupata huduma za afya
complex31