Kwa hali hii, waandaaji wa Maandamano wameshinda kwa 100%

Kwa hali hii, waandaaji wa Maandamano wameshinda kwa 100%

Leo hii ilitangazwa kuwa itakuwa ni siku ya maandamano nchi mzima.

Huyo admin wa hayo maandamano inaonekana anatumia akili nyingi sana huku akiiacha serikali ikiandaa ulizi wakidhania watakutana na waandamanaji barabarani.

Leo hii hakuna makundi ya waandamanaji barabarani lkn pia hakuna shughuli zote zote za uzalishaji.

Sabasaba watu hakuna,Kariakoo watu hakuna na maduka yote yamefungwa.

Kiuchumi hili ni pigo kubwa sana kwa serikali maana shughuli zote za kiuzalishaji zimesimama.

Wapewe makopa yao hao kina Mange naona sasa wamekuja kivingine.
Serikali imejiweka kwenye mtego mbaya kabisa.
Maana kwa sasa maandamano yakitangazwa tu askari watasambaa kama hivi Leo.
Maana yake hata askari wenyewe wanaweza wakaanzisha matangazo ya maandamano kwenye mitandao ili wapate posho au shughuli ya kufanya.
Na Serikali lazima iweke maaskari kila matangazo ya aina hiyo yakifanyika na biashara lazima zifungwe hiyo wiki kwa kuogopa kuwa inaweza kuwa kweli wakaandamana.

Kwa hiyo,makundi yote yanayonufaika na maandamano au vitisho vyake kama vile akina Shehe Mwaipopo,Askari wa aina zote nk watakuwa wanahamasisha maandamano kila wakijisikia ili wanufaike bila kutumia gharama kubwa.
 
Sijui kama unachokisema unakijua kuhusu Serikali kukosa mapato kwa siku moja hii leo,nafikiri utakuwa unatumia kiungo kingine kufikiri
Mlituaminisha hapa kuwa lengo la maandamano ni free Lissu, katiba mpya na Samia must go. Haya jwa serikali kupoteza mapato ya siku moja ndo mshayafikia malengo?
 
Ndugu yangu, ukweli ni kwamba hali hii ni pigo kwa serikali na wananchi kiuchumi. Kumbuka kuwa hii ni siku ya kilele kwa wafanya biashara ambao ndiyo tegemeo la kodi na pato la taifa.

Niko hapa sabasaba hali siyo nzuri kabisa ya kibiashara, lakini pia gharama inayotumika kuandaa hii siku ni kubwa na kubwa zaidi ni gharama kubwa sana inayotumika ktk ulinzi na usalama kufuatia matamko ya maandamano ya mtandaoni. Achilia mbali hali mbaya eneo la sabasaba huko mitaani nako shughuli za biashara na kijamii zimedorola, hii siyo afya kwa taifa.

Kama haya maandamano yatakuwa yanatolewa ktk kila siku muhimu za kitaifa na kupata hasara kama hivi ni wazi kuwa waandamanaji watakuwa wameshinda maana kwao ni kama hawana cha kupoteza ila sisi wananchi ndiyo tunaopata hasara ya kiuchumi, hofu na kukosa utulivu wa kijamii.

Kama taifa tunahitaji mazungumzo ya kweli ya ufumbuzi kutoka hapa tulipo.
So tushaachana na free Lissu.
Hayo maonesho hata yakifutwa hayana athari
 
Nijuavyo mm makafiri waoga sana bora waislam wakisema tunaandamana kufa kwao ni ibada hawaogopi ila hawa akina john weeeh!!!
 
Labda kama unaandika kishabiki,lakini kiuhalisia serikali inachezeshwa kwata na hao wahamasishaji wa maandamano,wamekaa mahali wanatype kwenye simu zao kuwa Kuna maandamano halafu serikali inadance tune yao,hii inasikitisha sana,katika nchi ambavyo inasifika kuwa na mfumo wa intelijensia kama hii hakukuwa na umuhimu wa kuanza kuhangaika na road patrol kama hizo.
Tunakoelekea hao wanamaandamano watazitumia public holiday zote zenye matukio ya kitaifa kuihenyesha serikali kuhangaika na ulinzi wa barabarani wakati raia tumejifungia ndani.
Kwa mtindo huu hebu nambie sasa nini lengo la maandamano haya na je yamefikiwa. Ila msisahau saana mnawatengenezea ulaji tu polisi
 
Serikali imejiweka kwenye mtego mbaya kabisa.
Maana kwa sasa maandamano yakitangazwa tu askari watasambaa kama hivi Leo.
Maana yake hata askari wenyewe wanaweza wakaanzisha matangazo ya maandamano kwenye mitandao ili wapate posho au shughuli ya kufanya.
Na Serikali lazima iweke maaskari kila matangazo ya aina hiyo yakifanyika na biashara lazima zifungwe hiyo wiki kwa kuogopa kuwa inaweza kuwa kweli wakaandamana.

Kwa hiyo,makundi yote yanayonufaika na maandamano au vitisho vyake kama vile akina Shehe Mwaipopo,Askari wa aina zote nk watakuwa wanahamasisha maandamano kila wakijisikia ili wanufaike bila kutumia gharama kubwa.
upo sahihi kabisa kiongozi
 
Leo hii ilitangazwa kuwa itakuwa ni siku ya maandamano nchi mzima.

Huyo admin wa hayo maandamano inaonekana anatumia akili nyingi sana huku akiiacha serikali ikiandaa ulizi wakidhania watakutana na waandamanaji barabarani.

Leo hii hakuna makundi ya waandamanaji barabarani lkn pia hakuna shughuli zote zote za uzalishaji.

Sabasaba watu hakuna,Kariakoo watu hakuna na maduka yote yamefungwa.

Kiuchumi hili ni pigo kubwa sana kwa serikali maana shughuli zote za kiuzalishaji zimesimama.

Wapewe makopa yao hao kina Mange naona sasa wamekuja kivingine.
We leo tu umesafisha vyoo vingapi,Au hata matako ya vibibi vingapi huko,wewe na nyani ngabu mje huku Kina mangel waachwe wapigwe "MITI"
 
Back
Top Bottom