Ndugu yangu, ukweli ni kwamba hali hii ni pigo kwa serikali na wananchi kiuchumi. Kumbuka kuwa hii ni siku ya kilele kwa wafanya biashara ambao ndiyo tegemeo la kodi na pato la taifa.
Niko hapa sabasaba hali siyo nzuri kabisa ya kibiashara, lakini pia gharama inayotumika kuandaa hii siku ni kubwa na kubwa zaidi ni gharama kubwa sana inayotumika ktk ulinzi na usalama kufuatia matamko ya maandamano ya mtandaoni. Achilia mbali hali mbaya eneo la sabasaba huko mitaani nako shughuli za biashara na kijamii zimedorola, hii siyo afya kwa taifa.
Kama haya maandamano yatakuwa yanatolewa ktk kila siku muhimu za kitaifa na kupata hasara kama hivi ni wazi kuwa waandamanaji watakuwa wameshinda maana kwao ni kama hawana cha kupoteza ila sisi wananchi ndiyo tunaopata hasara ya kiuchumi, hofu na kukosa utulivu wa kijamii.
Kama taifa tunahitaji mazungumzo ya kweli ya ufumbuzi kutoka hapa tulipo.