Kwa hali hii, waandaaji wa Maandamano wameshinda kwa 100%

Kwa hali hii, waandaaji wa Maandamano wameshinda kwa 100%

Wewe shangilia tu - ila ujue na uchumi wako unashuka pia. Uchumi wa mtu mmoja mmoja unashuka kwa watu kukaa nyumbani. Kuna watu wamejiajiri - sio waajiriwa kama wewe. Wenzako waliojiajiri - wakikaa nyumbani - pesa haiingii kama wewe ulieajiriwa. Sasa hesabu hizo siku ambazo mnafanya watu wasiende kwenye shughuli zao kwa mwaka mzima (e.g. 8), kisha zidisha kwa kila kipato cha mtu aliekikosa (e.g. 8x50,000=400,000); fanya hivyo kwa idadi ya watu wote ambao hawakwenda, kisha jumlisha. Ile TOTAL - ndio vipato ambavyo walala hoi wamevikosa. Na hapo ndio kwenye tatizo. Ujue pia - serikali inaungurumisha hayo magari kwa kutumia kodi zako - usidhani kama kuna "DONOR" anaetoa pesa ili hayo magari yatembee - hizo ni "KODI ZAKO"; wewe endelea tu kupiga kelele kwenye Key Board.
 
Kama haya ndio mafanikio mnayojivunia, basi mshakubali kuwa Samia ni mpaka 2030.
Biashara kufungwa kwa siku moja ni jambo la kawaida sana, haliwezi kuiteteresha serikali
Mkuu hakuna aliyesema kuwa Samia asitawale maana tayari ni mkuu wa nchi.

Tunachozungumzia ni matokeo ya maandamano Na athali zake kwenye uchumi wa Taifa
 
Leo hii ilitangazwa kuwa itakuwa ni siku ya maandamano nchi mzima.

Huyo admin wa hayo maandamano inaonekana anatumia akili nyingi sana huku akiiacha serikali ikiandaa ulizi wakidhania watakutana na waandamanaji barabarani.

Leo hii hakuna makundi ya waandamanaji barabarani lkn pia hakuna shughuli zote zote za uzalishaji.

Sabasaba watu hakuna,Kariakoo watu hakuna na maduka yote yamefungwa.

Kiuchumi hili ni pigo kubwa sana kwa serikali maana shughuli zote za kiuzalishaji zimesimama.

Wapewe makopa yao hao kina Mange naona sasa wamekuja kivingine.
Uongo kitu kibaya sana nipo zangu saba saba kwa raha zangu na kuna watu wa kutosha sana na wengi wanaendelea kumiminika
 
Hakuna mtu wa kuandamana hapa Tanganyika.. kuna vijibwa kazi kubweka tu mitandaoni.. Kwa mfumo wa maisha wa nchi hii,, ambao mijini asilimia kubwa wanachokula kesho wanatafuta leo ,, na huko vijijini waliozoea umaskini wao, usitegemee wa kwenda kufumuliwa na risasi..

Tuwe wapole ndugu watanganyika wenzetu,,, tuendelee kutiwa ma-🖕 na wana-mfumo hakuna namna,...
Hata babu yako, baba yako nao pia walishindwa kama wewe,,, usife kwa hasira za mihemuko ya bure..
 
Back
Top Bottom