Kwa hali hii ya uwingi wa majeshi huko Loliondo kwanini Serikali isitangaze hali ya hatari?!

Umesahau kuwa Dola ya KIISLAM imewahi kutawala Dunia?
Dunia ipi unayoiongelea? Ottomans walitawala Arabian Gulf North Afrika na Europe ni sehemu ndogo tu ya Sayari hii.

Sisi huku tulikuwa na Mizimu yetu na Tamaduni zetu.
 
Afadhali umeleta hoja. Edit maandishi uweke space tusome vizuri.

Pia unijibu uelewa wako juu ya VIBALI vya uwindaji vinatolewaje na Uwindaji unafanyikaj?

Nikuoneshe video uone wanavyowinda kikatili na kuua wanyama wetu?
 
Unajua pia kuwa Nyumbu na wanyama wengine huhama wakiwa na mimba kwenda Kenya na wakirudi hurudi wakiwa na watoto?

Mipaka ya nchi kuhusiana na mbuga zetu ni shirikishi.

Mipaka yote Kuna huo muingiliano wa watu.

Suala hili halipasi kuleta uhasama.

Masai waliotenda kutibiwa Kenya ni Watanzania na mbunge wao amethibitisha bungeni.

Ni Kweli KENYA huleta chokochoko sana tu, Jeshi wameweka KAMBI loriondo ni jambo zuri.

Bt Ngorongoro pale Pana mkono wa mtu.
 
Show show
Hii nchi bila nguvu huwezi kuiendesha.
Wahuni wapigwe, wapewe na kesi za uhujumu uchumi
 
Mimi Binafsi Imhotep napinga swala zima la Tophy Hunting hizo fedha za Uhifadhi wa Wanyama na Uoto wa Asili tulipe kwa kodi zetu ili Wageni waje kuangalia urithi tulioachiwa na Mababu zetu.
 
Dunia ipi unayoiongelea? Ottomans walitawala Arabian Gulf North Afrika na Europe ni sehemu ndogo tu ya Sayari hii.

Sisi huku tulikuwa na Mizimu yetu na Tamaduni zetu.
Turudi kwenye HOJA, umekiri Ngorongoro anapewa mwekezaji.

Faida anayoleta Mwindaji wa wanyama hai na faida ya watalii wanaokuja kupiga picha tu na kuondoka, ipi Ina manufaa Kwa vizazi na vizazi?
 
Mimi Binafsi Imhotep napinga swala zima la Tophy Hunting hizo fedha za Uhifadhi wa Wanyama na Uoto wa Asili tulipe kwa kodi zetu ili Wageni waje kuangalia urithi tulioachiwa na Mababu zetu.
Hoja nzuri hiyo.

Usafirishe Simba kwenye cage wakazaliane Nchi za watu huko.

Unadhani watakuja kwetu kutalii?

Mbona hawatujibu hili? Hapo hakuna uchama, jambo hili ni la KITAIFA tulipinge Kwa nguvu zote.
 
Usafirishe Simba kwenye cage wakazaliane Nchi za watu
Nimesema wapi ila kumbuka mpaka sasa kuna maeneo kama Florida huko USA kuna Safari Parks Watalii wanaenda kuona Wanayama ila Watalii wengi hupenda kuona Wanyama kwenye Natural habitat zao

Isitoshe hata ikaja ikatokea Wanyama wetu wakajazana Dunia nzima hawa ni Wanyama tumeumbwa nao tusiwamalize kumbuka Wazee wetu wa zamani walikuwa wakiishi na Wanyama na kuwawinda pale tu wanapohitaji kitoweo lakini leo tunazaliana bila hesabu

Mapori mengi tumeyachukua wewe unafikiri hawa Wanyama watatoboa kweli Karne ijayo.

Iko siku tutawanunua kutoka Mazoo ya Marekani na Ulaya ili warudi kuzaliana.
 
mambo ya dola ni hatari sana.....jicho lako sio jicho la dola....kuna salamu dola inakaribu kutuma mahala juu ya hilo jambo..

Kuna wakati ushabiki wetu wa siasa unakwenda mbali sana na kusahau hata utanzania wetu..
 
Ona huyu mnafiki, anajifanya amesahau mara hii, enzi za JPM aliwatandaza wanajeshi mijini ati wanafanya usafi. Kisa CDM? Leo unalialia nini? Vumilia sindano ikuingie vizuri.
 
Nimekiri wapi? Hebu uwe unaninukuu tafadhali.

Nilikuambia uache Ubaguzi that's all"
Hizo tophy hunting, zinafanyika bila mikataba? Ilikuwa mwaka mmoja mmoja, ikawa 5 MITANO enzi za Kikwete, now miaka 15,

HOFU yangu kama mzalendo wasijetafuta madalali waanze uharibifu kutafuta vya chini ya mbuga afu tuje kusingizia wakenya.๐Ÿ˜ ๐Ÿ˜ 
 
Afadhali umeleta hoja. Edit maandishi uweke space tusome vizuri.

Pia unijibu uelewa wako juu ya VIBALI vya uwindaji vinatolewaje na Uwindaji unafanyikaj?

Nikuoneshe video uone wanavyowinda kikatili na kuua wanyama wetu?
Mimi si deal na vibali vya wawindaji, bali na deal kwanz na hawa mafisadi wanaofanya ardhi yetu kuwa shamba la bibi yao. Kutumia ardhi yetu bure kwa faida yao, serikali yao na vizazi vyao hili haliwezi kukubalika kamwe. Acha tu deal na hawa wa bure, tukishamaliza ndo tutaangalia hao walioingia mikataba kile wanachowinda kinaendana na kile wanacholipa au la. Kuna msemo unaosema kwamb mkono mtupu haulambwi. So wakenya kupitia ndugu zetu wa kimasai, na wale wa kwao wanatumia ardhi yetu bure kabisa, kwa faida zao na vizazi vyao. Na mwarabu kupitia serikali anataka kuja kuwinda wanyama wetu kwa malipo fulani kwa faida yao na vizazi vyao.
Najua kama kila mpaka huwa kuna muingiliano wa watu wa pande zote mbili, lkn wenzetu wameutumia muingiliano huo kama kichaka cha kuhalalisha haya yanayopingwa na serikali. Sizani kama muingiliano huo ndo unaruhusu watu waingie na kujichimbia katika nchi nyingine bila kufuata taratibu za kisheria. Sizani kama muingiliano huo unaruhusu kundi la watu kutoka nchi moja kwenda kulisha mifugo katika nchi nyingine bila kufuata sheria. Pia sio kila mmasai aliekimbilia kenya kutibiwa ni mtanzania, wengine ni wakenya waliokuwa wakiishi Tanzania kwa kutumia vibali vya mchongo wanavyopewa na baadhi ya askari wa uhamiaji wenye tamaa ya pesa. Mwenye jukumu la kujua kwamb wamasai wote walienda kutibiwa Kenya ni watanzania au sio ni mamlaka ya uhamiaji au ofisi ya wizara ya mambo ya ndani. Na ndo maana uhamiaji wenyew wamekwenda kukita kambi kule ili kujiridhisha na haya yaliyosemwa na mbunge wao. Maana mbunge anaweza tu kulitumia hili neno kisiasa kwa faida zake mwenyewe.
 
Unasapot usafirishaj wanyama ndugu?
 
Trust me,Kenya Uganda Rwanda wakishaban Trophy Hunting limebaki Shamba la Bibi lenye Viongozi wenye Low IQ ambao wakivaa mashati ya Kijani tu wanajiona wao ni miungu.
 
Unasapot usafirishaj wanyama ndugu?
Kuna Zoo's Duniani kote wananunua Wanyama pori na sioni tatizo ila kumbuka ndiko kwenye Faru wengi kuliko Mwituni

Ipo siku tutawanunua kutoka huko kwa sababu sisi Waafrika tuna Uzembe wa kipuuzi kabisa.

Nakumbuka Askari wa Savimbi walikuwa wanaingia porini na SMG na RPG kwenda kuua Tembo kwa ajili ya chakula cha Jeshi lao.
 
Dunia ipi unayoiongelea? Ottomans walitawala Arabian Gulf North Afrika na Europe ni sehemu ndogo tu ya Sayari hii.

Sisi huku tulikuwa na Mizimu yetu na Tamaduni zetu.
Ottoman empire ni utawala uliyokuwa chini ya nchi ambayo leo hii inaitwa Uturuki. Uturuki kijiografia ipo ulaya na asia ya kaskazini. Kwahiyo ipo mbali mbali mno na zile nchi za kiarabu. Waturuki sio waarabu na wala hawajawahi kuwa na asili ya uarabu. Na pia jamaa anatakiwa afahamu sio kila mwarabu ni muisilamu, na vilevile sio kila muislam ni mwarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ