Kwa hapa Dar wapi naweza kupata hii mboga inayoitwa mgagani?

Kwa hapa Dar wapi naweza kupata hii mboga inayoitwa mgagani?

Wakuu

Nimemiss kula mboga za asili,kuna anaejua wapi kwa hapa Dar naweza kupata hii mboga ya majani inayoitwa mgagani?

Ni mboga maarufu zaidi huko kanda ya ziwa.View attachment 3265940
nimeziona sana maeneo ya cota za ilala
Wakuu

Nimemiss kula mboga za asili,kuna anaejua wapi kwa hapa Dar naweza kupata hii mboga ya majani inayoitwa mgagani?

Ni mboga maarufu zaidi huko kanda ya ziwa.View attachment 3265940
nimeziona sana maeneo ya kota za ilala BOMA,
 
Majuzi tu nimetoka Simiyu huko vijiji vya Nyang'hwale, Nkindwabiye, Byuna, Nkololo, Nyangokolwa, Sanungu na Ng'washagata. Nimekula sana migagani tena ile orijino kabisa inayoota na kustawi vizuri kwenye matongo (maeneo yaliyokuwa mazizi ya ng'ombe zamani).

Kwa taarifa tu ya nyongeza mgagani (hasa ule mchungu kabisa) ni dawa moja safi sana kwa walioanza kupungukiwa na nguvu za nyuklia mwilini. Ukipikiwa hiyo wiki moja tu pamoja na maboga tayari mtambo wa nyuklia unaanza kuzalisha umeme. Pengine ndiyo sababu inasemekana Wasukuma wengi hawaishiwi umeme kirahisi rahisi hata wakizeeka namna gani....

Kwa Dar sikushauri maana utaishia kula sumu tu sawa na mboga zingine kama mchicha na matembele. Kuna tasnifu ya uzamili iliyochunguza makemikali na sumu zilizomo kwenye mboga zinazolimwa na kuzalishwa huko Dar. Ni sumu tupu na sikushauri!

Kama kweli uko siriazi, agiza mtu akutumie kutoka Simiyu na sisitiza sana upate ule mgagani wenye rangi nyekundu nchani kama jogoo zee. Ungepata na majani kidogo ya būtembetembe ukachanganya dah! Ungesafisha mishipa yako ya damu na kurudi kuwa kama tineja! 😎😎😎
 
Nimetoka Simiyu huko vijiji vya Nyang'hwale, Nkindwabiye, Byuna, Nkololo, Nyangokolwa, Sanungu na Ng'washagata. Nimekula sana migagani tena ile orijino kabisa inayoota na kustawi vizuri kwenye matongo (maeneo yaliyokuwa mazizi ya ng'ombe zamani).

Kwa taarifa tu ya nyongeza mgagani (hasa ule mchungu kabisa) ni dawa moja safi sana kwa walioanza kupungukiwa na nguvu za nyuklia mwilini. Ukipikiwa hiyo wiki moja tu pamoja na maboga tayari mtambo wa nyuklia unaanza kuzalisha umeme. Pengine ndiyo sababu inasemekana Wasukuma wengi hawaishiwi umeme kirahisi rahisi hata wakizeeka namna gani....

Kwa Dar sikushauri maana utaishia kula sumu tu sawa na mboga zingine kama mchicha na matembele. Kuna tasnifu ya uzamili iliyochunguza makemikali na sumu zilizomo kwenye mboga zinazolimwa na kuzalishwa hapa Dar. Ni sumu tupu na sikushauri!

Kama kweli uko siriazi, agiza mtu akutumie kutoka Simiyu na sisitiza sana upate ule mgagani wenye rangi nyekundu kichwani kama jogoo zee.
We kijana, unajua haya maeneo yote? Kwanini umesahau Kashishi, Mbalandwa, Ngeme, Ngw'amapalala, Kasori, Malita, na Zanzui mwanangu?
 
Ila kuna mboga unawaza binadamu alikuwa anawaza nini! Kuna mgagani, mnavu na mchunga🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
Mnafu mboga nzuri sana sana. Mimi ndiyo chaguo langu na niseme ndiyo mboga nayoipenda kuliko zote. Ila siyo huu mnafu wa Dar wa kufoji. Ukienda Moshi kuna mnafu wa aiana nyingine, ule wenye vi-matunda vidogo vidogo.
 
Back
Top Bottom