Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Kuna msemo wa wenzetu wa kusini usemao, "kukaa nchale, kusimama nchale." Kwa maoni yangu hapo ndipo tulipofikia sasa baada ya ripoti ya Jaji Chande.
Kama umepata nafasi ya kumsikiza Jaji Chande, kwanza alipowasilisha ripoti kwa Rais Samia na baadaye alipokuwa akitolea ufafanuzi ripoti yake kwa vyombo vya habari: Hotuba ya Rais kwa wazee wa Dar es salaam, mahojiano ya balozi Nyalandu, maoni ya watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, viongozi wa dini wakiwemo Mashehe na hivi kalibuni Baba askofu Ryeyongeza, utakubaliana na wakili msomi Madeleka kuwa unahitaji Neema ya Mungu pekee kutokuchanganyikiwa mpaka sasa.
Ukisoma maoni ya wengi, ni dhahiri kuwa serikali, vyombo vya dola, vyama vyote vya siasa na waandamanaji, wote kwa pamoja wana cha kulaumiwa kwa namna moja au nyingine; Lakini ripoti ya Jaji Chande inaegemea kupeleka lawama zaidi kwa waandamanaji, wachochezi kutoka nje ya nchi na wachochezi wa ndani ambao kwa ujumla wao walipanga, waliratibu na kufadhili vurugu.
Kwa mtazamo wangu, ripoti ya tume haijafanikiwa kuliunganisha Taifa kuelekea kwenye maridhiano. Tulipofikia sasa, tumegawanyika zaidi kuliko tulivyokuwa awali jambo linaloleta mashaka kama maridhiano yataweza kupatikana kwenye mazingira haya.
Kwa maslahi ya Taifa, na kuepuka kuendelea kupoteza fedha za walipa kodi masikini wa nchi hii kwenye hizi tume, ni vyema TUKAKUBALIANA KUTO KUKUBALIANA. Maadam tayari serikali ilishawasamehe watuhumuwa wa kinachoitwa vurugu za Oktoba 29, tuishie hapa hapa, tuendelee tu na shughuli zingine za ujenzi wa Taifa. Masuala ya haki na kuwajibishana tumwachie Mungu, sisi yameshatushinda.