PostGE2025 Kwa hapa tulipofika; Ya Oktoba 29 tungeyaacha, tuendelee na mambo mengine

PostGE2025 Kwa hapa tulipofika; Ya Oktoba 29 tungeyaacha, tuendelee na mambo mengine

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Walionyimwa haki zao, wanafaidika vipi baada ya miaka 10 au hiyo 20?
Jamii yoyote inayoishi bila uwajibikaji na jamii ya hovyo. Hata hivyo Inaweza kuwa vigumu kuelewa mpaka utakapokutana na mtu aliyekaa gerezani miaka mitano bila makosa halafu akaja kuachiliwa baada ya mapambano ya muda mrefu kuitafuta haki yake.
 
Kuwatoa CHADEMA kwenye lawama ya Oktoba 29, nikama kubomoa msingi wa jengo. Chimbuko la haya yote, pamoja na mengine, ni malalamiko ya kukosekana kwa usawa katika chaguzi zetu. Hiki ndicho kilichopelekea kampeni ya "NO REFORMS, NO ELECTION" jambo lililopelekea kukamatwa na kushitakiwa kwa Tundu Lissu. Swali la msingi ni Je, CHADEMA wangekubali kuingia kwenye uchaguzi yaliyotokea yangetokea? Jibu dhahiri ni hapana! Sasa kwanini uwatoe kwenye lawama?
Unamaanisha kuwa pamoja na rais wa machawa kuchaguliwa Kwa asilimia 98 ile asilimia mbili ndio ilileta vurugu? Ni mpumbavu pekee anayeweza kuamini ule ujinga ulioitwa uchaguzi. By the way kama asilimia mbili ndio haikumkubali rais wa machawa maana yake kauli mbiu ya NO reforms no election ilishindwa maana haikushawishi umma hivyo CDM haiwezi kuhusishwa na ujinga wa ccm na machawa wao.
 
Unamaanisha kuwa pamoja na rais wa machawa kuchaguliwa Kwa asilimia 98 ile asilimia mbili ndio ilileta vurugu? Ni mpumbavu pekee anayeweza kuamini ule ujinga ulipitiwa uchaguzi. By the way kama asilimia mbili ndio haikumkubali rais wa machawa maana yake kauli mbiu ya NO reforms no election ilishindwa maana haikushawishi umma hivyo CDM haiwezi kuhusishwa na ujinga wa ccm na machawa wao.
Comrade hatuzungumzii takwimu za uchaguzi hapa, tunazungumzia chanzo cha yaliyotokea Oktoba 29.
Takwimu za uchagumzi mm na ww hatuna namna yoyote yakuzithibitisha, tumwachie Mwenyekiti wa tume ndiye anayejua alikozitoa.
 
Jamii yoyote inayoishi bila uwajibikaji na jamii ya hovyo. Hata hivyo Inaweza kuwa vigumu kuelewa mpaka utakapokutana na mtu aliyekaa gerezani miaka mitano bila makosa halafu akaja kuachiliwa baada ya mapambano ya muda mrefu kuitafuta haki yake.
Itoshe tu kusema kuna mambo only God can intervene.
 
Umewahi kusikia kwamba kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji?

Nigga if u cant carry a gun, you change nothin
Uelewa wako ni mdogo sana ndio maana huelewi impact ya watu kupigia kelele October 29
Halafu unasema kuongelea Oct 29 haitachange anything, kwa hiyo unashauri watu wasiongelee October 29 ndio changes zitatokea?
 
Uelewa wako ni mdogo sana ndio maana huelewi impact ya watu kupigia kelele October 29
Halafu unasema kuongele Oct 29 haichange anything, kwa hiyo unashauri watu wasiongelee October 29 ndio changes zitatokea?
You are diverging the important part nigga.
If you cant carry a gun, you are just an asshole.
 
Kuwatoa CHADEMA kwenye lawama ya Oktoba 29, nikama kubomoa msingi wa jengo. Chimbuko la haya yote, pamoja na mengine, ni malalamiko ya kukosekana kwa usawa katika chaguzi zetu. Hiki ndicho kilichopelekea kampeni ya "NO REFORMS, NO ELECTION" jambo lililopelekea kukamatwa na kushitakiwa kwa Tundu Lissu. Swali la msingi ni Je, CHADEMA wangekubali kuingia kwenye uchaguzi yaliyotokea yangetokea? Jibu dhahiri ni hapana! Sasa kwanini uwatoe kwenye lawama?
Sasa kwanini serikali haikufanya hizo reforms chadema waingie kwenye uchaguzi? hapo ndo utaona mtuhumiwa number moja ni CCM wamezoea Siasa za ulaghai
 
Serikali, Tume na jeshi la Polisi wanasema video clips za mauaji zilitengenezwa kwa AI, wanaopinga wanadema video ni halisi.

Sisi wananchi wa kawaida tumwamini nani?
Wananchi siyo wajinga.
Em sikiliza hizi video 2 hapa chini za walionusurika kufa halafu ulete mrejesho kama ni za Ai..

Huyu Bibi walimpiga risasi na kumjeruhi vibaya wakampeleka mochwari:
👇

View: https://youtu.be/j9yI9PAGIcA?si=IaN_K_PsyexBjbph

Huyu kijana alipigwa risasi akavunjwa na kukatwa mguu:
👇

View: https://youtu.be/SFUI36BQSwY?si=ilbtGHQwGXcLO4Iw
 
Huu ndio msingi wa hoja yangu kuwa kutenda haki kwenye hili imeshatushinda, tumwachie tu Mwenyezi Mungu.
Kwaakili ya kawaida tu, unadhani upo utashi wa kisiasa kutoka kwa viongozi wetu wa kuchukua hatua dhidi ya waliotenda vitendo hivi?
Kinachoendelea ni kumaliza pesa za walipa kodi kwa kuunda tume juu ya tume ambazo hazitatuletea uwajibikaji wowote.
Kwatulipofikia tumwachie Mwenyezi Mungu aje atoe hukumu yake siku ya kiama. Sisi acha tuendelee na 4R
 
Kuna msemo wa wenzetu wa kusini usemao, "kukaa nchale, kusimama nchale." Kwa maoni yangu hapo ndipo tulipofikia sasa baada ya ripoti ya Jaji Chande.

Kama umepata nafasi ya kumsikiza Jaji Chande, kwanza alipowasilisha ripoti kwa Rais Samia na baadaye alipokuwa akitolea ufafanuzi ripoti yake kwa vyombo vya habari: Hotuba ya Rais kwa wazee wa Dar es salaam, maoni ya watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, viongozi wa dini wakiwemo Mashehe na hivi kalibuni baba askofu mmoja, utakubaliana na wakili msomi Madeleka kuwa unahitaji Neema ya Mungu pekee kutokuchanganyikiwa mpaka sasa.

Ukisoma maoni ya wengi, ni dhahiri kuwa serikali, vyombo vya dola, vyama vyote vya siasa na waandamanaji, wote kwa pamoja wana cha kulaumiwa kwa namna moja au nyingine; Lakini ripoti ya Jaji Chande inaegemea kupeleka lawama zaidi kwa waandamanaji, wachochezi kutoka nje ya nchi na wachochezi wa ndani ambao kwa ujumla wao walipanga, waliratibu na kufadhili vurugu.

Kwa mtazamo wangu, ripoti ya tume haijafanikiwa kuliunganisha Taifa kuelekea kwenye maridhiano. Tulipofikia sasa, tumegawanyika zaidi kuliko tulivyokuwa awali jambo linaloleta mashaka kama maridhiano yataweza kupatikana kwenye mazingira haya.

Kwa maslahi ya Taifa, na kuepuka kuendelea kupoteza fedha za walipa kodi masikini wa nchi hii kwenye hizi tume, ni vyema TUKAKUBALIANA KUTO KUKUBALIANA. Maadam tayari serikali ilishawasamehe watuhumuwa wa kinachoitwa vurugu za Oktoba 29, tuishie hapa hapa, tuendelee tu na shughuli zingine za ujenzi wa Taifa. Masuala ya haki na kuwajibishana tumwachie Mungu, sisi yaneshatushinda.
Daktari,

Mambo haya huwa hayajifii/hayamalizwi kwa kusema tuyaache. Sayansi ya jamii inasema hatua muhimu kwenye kujenga mahusianao mema/reconcilliation:

1: Aliyekosa/akubali kutenda makosa kama yapo.

2: Onyesha kujutia kwa kilichotokea/kubali kubeba lawama na thamani ya tatizo husika.

3: Tengeneza uaminifu mpya kwa mhusika.

4: Tengeneza mahusiano mapya yenye afya, mawasiliano mazuri na tabia njema.

Kuishindwa kutenda haki kwenye hili ni kwa kupimo kupi? Na kama utashindwa kwa hili lililo wazi, credibility ya kuongoza iko wapi?

Haya mambo tatizo kubwa ni kuzungukwa na chawa. Wanashindwa kuliendea jambo kwa mujibu wa muktadha wake:

1: Haya mambo yataendelea kuzalisha visasi hata kama ni kwa vizazi vyetu au vijavyo.

2: Kuna watu wanamatatizo ya kisaikolojia/afya ya akili na wataendelea kuongezeka kama hatua halisi hazitazingatiwa kwani watu wanaishi na maumivu.

3: Hatutaweza kupata utengamano wa kijamii na kitaifa kwa kufunika kikombe.

4: Serikali iyaendelea kutumia gharama kubwa kujiendesha kwa mazingira husika ili kudhibiti hofu yake.

5: Huwezi kuleta maendeleo kwa watu ambao kwa kiasi kikubwa wako emotionally detached na wewe, ni kujidanganya.

6: Hata huko serikalini tutaanza kuona afya zao za akili mmoja mmoja wanatupa mashaka. Kwani mambo ni mengi na wo si mawe.

Wito: Tufuate taratibu za kiungwana, zinazofahamika na zinazokubalika kutatua matatizo tuliyoyatengeneza. Tusirahisishe mambo na kujizima data.
 
Back
Top Bottom