PostGE2025 Kwa hapa tulipofika; Ya Oktoba 29 tungeyaacha, tuendelee na mambo mengine

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Dr Adam Francis hivi mauaji kama hayo unaachana vipi? Unadhani ni rahisi sana!! Mimi hizo picha zinanusumbua sana, hata nikifa baadae itakuwa ni mojawapo ya sababu!

Do you still have trust in State apparatuses with courage to engage in that escalated levels of cruelty against humanity?
Why massacre your own citizens?
 
Ni muhimu kuweka Rekodi sawa ili Uongo, Hadaa, Udanganyifu na propaganda za wauaji zisitamalaki..


View: https://www.instagram.com/reel/DXqolt7jsr_/?igsh=MWoyeWFpOTdibG5jbw==
Comrade kwenye hili ukweli ni upi? Serikali na Tume zinasema kilichotokea kilikuwa ni vurugu zilizopangwa, kuratibiwa na kufadhiliwa kwa lengo la kuiba, kuharibu mali na kupindua serikali.

Kwa upande mwingine wanaharakati, wanasiasa wa upinzani na baadhi ya viongozi wa dini wanadai yale yalikuwa ni maandamano ya kudai mageuzi kwenye sheria zetu za uchaguzi, katiba mpya na kukomeshwa kwa utekaji.

Serikali, Tume na jeshi la Polisi wanasema video clips za mauaji zilitengenezwa kwa AI, wanaopinga wanadema video ni halisi.

Sisi wananchi wa kawaida tumwamini nani?
 
Yani watu wamekufa 0ct 29 unasema tuachane nayo
Tunaomba ww utupe solution na mkakati wa utekelezaji wake kuifikia haki!
Mm sioni kama kuna dhamira ya dhati ya kuwajibishana. Huu ndio msingi wa hoja yangu kuwa hili limetushinda, tumwachie Mwenyezi Mungu, atalitolea hukumu siku ya kiama kwa haki!
 
Kwa hiyo unataka watu waliozika nguo wasahau kilichowapata ndugu zao???inaonekana ww hujapoteza mtu oktoba 29 huko kusahau au kukubali kutokukubaliana unaposema wewe ndo wanapopataka wenyew wahusika wa yale mauaji wanataka tusahau as if nothing happened embu jaribu kuangalia zile video za watu walivyokua wanarundikwa mochwari kama maembe,au ile ya mwanza watu waliokuwa wakiangalia mpir awalivyouawa ukiona hizo hazijakugusa angalia ile ya yule mama alivyopigwa risasi mbele ya binti zake af vaa viatu vya ndugu zao then uje hapa urudie ulichokiandika sio unakurupuka tu.
 
Tukitaka maridhiano haikwepi Tundu Lissu na wengine walioko na kesi mahakamni zifutwe pia na waliotekwa serikali itoe maelezo ya kina kwa wananchi na hatua zilizochukuliwa za kiuwajibikaji kisha tusonge mbele
Serikali inataka kila kitu!
Inataka maridhiano, inataka kuwashikilia watu na kuwapeleka mahakamani bila kosa, inataka ipate sura nzuri kutoka jumuia ya kimataifa, inataka wenye makosa wao waonekane hawana makosa kwa kuua watu kinyume cha katiba, inataka isiulizwe kitu chochote kuhusiana na mauaji ya October 29 na inataka kila mtu aipongeze kwa yote!
 
 
Serikali, Jeshi la polisi na Tume ya Jaji Chande kwa pamoja wamesema hizi picha ni AI. Sasa tumwamini nani?

Comrade kuna mambo mengine ni yakukubali tu, kuwa hata kama umeonewa dhahiri shahiri, ni Mwenyezi Mungu tu ndio atakulipia.

Swali langu kwako, niambie ww unampango gani wa kuhakikisha haki ya waliojeruhiwa na kupoteza maisha inapatikana katika mazingira ambayo tunaambiwa kilichotokea kilikuwa ni vurugu zilizopangwa, kuratibiwa na kufadhiliwa ili kuiba, kuharibu mali na kupindua serikali?
 
Acha upumbavu na ondoa hiyo title ya Dr., unadhalilisha taaluma.
 
Nasisitiza hapo hapo

Masuala ya haki na kuwajibishana tumwachie Mungu, sisi yaneshatushinda
 
Unaweza kucheka kana kwamba ni mazuri!
 
Kuendelea na mambo mengine ni uamuzi wetu.Lakini,kuwaacha na kukaa kimya ni kutozitendea haki tabia zetu za asili za nongwa na gubu.Gubu liendelee!
 
Tunaomba ww utupe solution na mkakati wa utekelezaji wake kuifikia haki!
Mm sioni kama kuna dhamira ya dhati ya kuwajibishana. Huu ndio msingi wa hoja yangu kuwa hili limetushinda, tumwachie Mwenyezi Mungu, atalitolea hukumu siku ya kiama kwa haki!
Kama huoni dhamira yake achana nalo, sisi tutaendelea kuliongelea
 
Tunaomba ww utupe solution na mkakati wa utekelezaji wake kuifikia haki!
Mm sioni kama kuna dhamira ya dhati ya kuwajibishana. Huu ndio msingi wa hoja yangu kuwa hili limetushinda, tumwachie Mwenyezi Mungu, atalitolea hukumu siku ya kiama kwa haki!
Wenzako wanaleta hisia kwenye jambo ambalo halihitaji hisia. Na kutokana na kuendekeza mambo ya hisia unakuta wengine wanaota kwamba kuna kesi zitafunguliwa ICC wanasahau msemo wa Kiswahili usemao Mwenye nguvu mpishe.
 
Imechanganyikiwa
 
Kesi za aina hii watu huwa wanaweza kuja kuwajibishwa hata miaka 20 mbeleni mambo yakibadilika.
Walionyimwa haki zao, wanafaidika vipi baada ya miaka 10 au hiyo 20?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…