Kwa hasira hizi na maelekezo haya tumekwisha

Kwa hasira hizi na maelekezo haya tumekwisha

Wasaidizi wa Mama wamezingua sana, hivi watu wanapotekwa huwa hawamshauri hata aongee chochote, hata kinafiki tu??
 
Mama amekasirika sana
Kwa clip hII, nineogopa sana. Lisu awe macho sana, na wasiwasi wangu unakuja pale ambapo hatuna independent judiciary. MAHAKANA HAZIKO HURU, hawa wanapokea maelekezo, huyu mama ATATOA MAELEKEZO! MAELEKEZO MABAYA

Kesi ya Lisu ni simple sana, lakini kwa maelekezo ya mahakama kutoka kwa mama ni mbaya sana!
We need much more pressure from outside, especially "super powers"

😅😅😅
 
Magufuli aliona mapema kwa huyu msaliti na kumpeleka uhamishoni Ubelgiji,mama akaenda kumfuata eti 4R! Ngoja amnyooshe. Kila alichokifanya magufuli alikuwa sawa,vichaa ndio hawakumuelewa.
Sababu ya kunuka damu za watu ikiwepo ya Lisu Mungu akaondoa liuwaji lile. Uzuri Watu kama wale Mungu anadili nao mwenyewe. kaonywa kashupaza shingo. Kashaoza kaburini.
 
Magufuli yuko wapi?

Mwambieni Samia kuteka watu au kuua sio mwisho au suluhu ya kukosolewa , anatakiwa atende haki kelele zitaisha la si hivyo apumzike tu.

Willy Mutunga jaji mkuu mstaafu aliyemzuia kuingia Tanzania , amesoma UDSM hapo na hata Moi alipomfunga kifungo kilipoisha alikimbilia uhamishoni Canada na hata aliporudi alikuwa miongoni mwa nguzo kubwa katika kupata katiba mpya 2010 leo hii wanapata uhuru wa mihimili tofauti na katiba yao ile chakavu ya 1963 na aliyewatishia alishakufa ila Kenya bado imebaki na itaendelea kuwepo.

Historia inajirudia Magufulia aliteka na kuua watu wengi tu lakini wakosoaji wamekuwepo hadi anakufa na sasa bado wapo hivyo Samia asifikiri kuna namna ya mkato kuwamaliza wakosoaji maana ipo sababu ya watu kumkosoa ila yeye anajificha kwenye kichaka cha jinsia ilhali yanayofanyika hayapendezi.
 
KWa hiyo wakenya ndiyo wamemweka Lisu ndani? Waafrika tuna matatizo ya kifikra sana yaani uvurunde mwenyewe afu uwalaumu maadui zako hii si sawa
nakubaliana na Samia katika hili. CJ wawili toka Kenya ambao hawawezi kutoka kuja hapa bila kibali cha Ruto, na wote waliokuja, serikali imewaheshimu sana,walitakiwa waadibishwe kabisa. kenya ni EU kuna uwezekano mkubwa wazungu wameona wameshindwa pa kutuvuruga wanaingilia kenya, yaani tangu lini wakenya wakatupenda namna hii kutupigania? never on earth. wazungu wameingilia hapo, na kenya wenyewe tumeshawapiga sana kwenye biashara, SGR inawaumiza moyo kwa sababu tukifia burundi/kigoma rwanda na mwanza, basi bandari yao ya mombasa italia machozi wanatamani tusiendelee ili wao waendelee. kuna mengi sana yamejificha naomba watanzania msijefikiri hawa watu wanatupenda. CJ wawili wasingetoka kule kuja hapa kama hawajatumwa, na waliowatuma hawatutakii mema. tumalizane sisi kwa sisi mambo yetu lakini tusiruhusu jirani atuvuruge.
 
Magufuli alifanya mazuri na kwangu ni Rais Bora kbs, lkn kizuri hakikosi kasoro...hakutaka kukosolewa kbs, na hakutaka kitu kinachoitwa upinzani..hivyo basi tumia akili yako vzr unapojenga hoja, kukosoa sio usaliti.
Usaliti no usaliti na kukosoa no kukosoa,TL alionesha usaliti wke kwenye madini
 
Back
Top Bottom