Kwa hawa Madaktari huko mbeleni tutapata tabu

Yaani kiinglishi cha Kyutiii ni bora mnooo kuliko cha baadhi ya madaktari
 
Kama daktari anaweza kuokoa maisha kingereza kinasaidia nini?, Nenda China, urusi, Spain, uarabuni, uone Kama kuna mtu anahusudu kingereza.
Kabisaa ni ulimbukeni tu hoja hapa labda hawapo compitent sawà mambo ya kingereza haya husiaani
 
Yaani Mimi pia Ni mmoja wa watu ninaosikitishwa Sana na wimbi la ongezeko la hutu tu vyuo twa afya,Kuna failures wakutosha humo,nilienda hospital na mtoto kipimo kikataka atolewe damu ya mshipa imagine mtu hawezi,kamchoma Mara ya kwanza kachokonoa kashindwa,kabadili sindano kachokonoa kashindwa,eti anataka kuchukua ya tatu, Aiseeee nilikuwa mbogo..namuuliza wewe huyu mwanangu ndio wa majaribio au vipi?nilikiamsha Hadi alikuja mtu mwingine kummalizia zoezi.....tangu siku hiyo Kama ulivyoshauri Niko selective Sana kwa watoa huduma.
 

Mahospitali mengi ukifika unaweza dhani unaongea na Daktari mahiri kumbe ni CO aliyepita njia za panya.

Kuna mambo mengine siwezi kuyaweka bayana humu lakini kimsingi huko mbele ni hatari kubwa

Alafu serikali nayo ati inatoa ufadhili wa mkopo milioni 3 tuu alafu hizo gharama zingine utajijua. Hivi Kama mtu alishindwa kusomeshwa shule ya sekondari ambayo Ada ikiwa kubwa ni laki tano Kwa mwaka. Huku Chuo akichukua MD ndio ataweza kulipia hiyo milioni 3.

Maana Ada ya kusomea MD ni around 6M katika vyuo vingi hapa NCHINI.

Serikali iangalie hili
 
Well said!yaani iliangalie hili suala kwa hicho la tatu.
 
Hahaaa kiingereza cha kuongea hakina mchango wowote kwenye taaluma ya udaktari, kutojua english fluently hakumzuii mtu kujua content kama dawa nakadhalika sababu hizo dawa kinachohitajika ni kukariri zaidi kutokana na majina yake ya kifamasia, mwisho kuna watu wanaongea vzuri english kichwani hamna kitu usidanganyike na kiingereza
 
Materials za Taaluma ya Udaktari nyingi zipo Kwa lugha ya kingereza.

Na kutokana na mabadiliko ya magonjwa na madawa Udaktari kila siku unahitaji ku-update.

Huwezi kuwa Daktari mahiri bila kujua Lugha ya kingereza
Kuna kiingereza cha kuongea na chakujua contents za kidaktari kama majina ya madawa,magonjwa, aina za huduma kama surgery, liposuction, c section mtu anaweza akawa competent kwenye haya lakini kuongea english fluently ikawa shida
 
Wakuuu mleta uzu yupo sahihi,

Ila kimombo sio sehem ya kumhukum daktari kuwa anaweza au hawezii.
Lugha wanaweza kuisoma nakuelewa ila wengi kwenye kuongea ndio ovyo ani pronounciation..hapo ndo wanaongeaga kiwanga
 
Kujua contents kama madawa na majina yake na kuongea fluently kingereza ni vitu viwili tofauti, kutokujua kuongea english fluently hakukuzuii kujua hizo contents sababu kinachosomwa ni procedures na kukariri pamoja na kujua majina ya madawa
 
Materials za Taaluma ya Udaktari nyingi zipo Kwa lugha ya kingereza.

Na kutokana na mabadiliko ya magonjwa na madawa Udaktari kila siku unahitaji ku-update.

Huwezi kuwa Daktari mahiri bila kujua Lugha ya kingereza
Uongo huuuu
 
Well said
 
Mkuu tafuta hela,ukiwa na hela hata ukiongea broken english utaonekana unakijua.
 
Kama ana d4 na akaenda kusoma na akafaulu tatizo liko wapi ?,au unahoji uhalali wa mitihani ya utabibu
 
Kumlaumu mtu kutojua lugha ya kigeni ni tatizo
 
Ni hatari sana nimewahi kuchomwa sindano ikakosewa sjui niliburuza mguu siku Tatu
 
Tatzo lako huwezi kutofautisha ,kuongea kingereza kilichonyooka na kujua contents za udaktari na kuzielewa, mtu anaweza kabisa kujua contents za udaktari mfano epilepsy, schizophrenia, c section na root canal treatment na akawa competent kutoa huduma kwa wagonjwa husika na akasifiwa sana lakini ukimleta kwenye kuongea kiingereza kilichonyooka akawa ana makosa mengi, na mwingine akaongea vzuri kiingereza kutokana na mazingira aliyokulia lakini asiwe competent katika kuperfom baadhi ya huduma
 
Kweli kbs wasiwaonee madaktari tu, hata Walimu na wengine kingereza ni tatizo.
Kiingereza kila secta ni tatizo sababu ni lugha yetu ya pili ,by the way hata mwalimu anaweza kua competent kudeliver materials na akasifika sana lakini anaungaunga kiingereza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…