Kwa heri Chadema, sitakuwa siwezi kuwa chawa wa kumsafishia njia Samia

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001

Habari zote kuhusu Mbowe kung'ang'ania madaraka zipo humu, kwa hiyo hakuna haja ya kurudia.
Nimekuja hapa kutoa taarifa tu kwamba nimeshtukia hii deal ya Mbowe na CCM. Sisi sio wajinga wa kufanywa kama CUF ya Lipumba. Sisi tuna akili, nenda peke yako bwana Mbowe kulamba viatu vya Samia. Kama ulitegemea tutakuunga mkono, basi ulichanga karata zako vibaya.

Hatutaondoka Jukwaa la Siasa, lakini sio kuunga mkono hotuba zako za kitapeli.
 
Tumtoe Rais katika hili, tupambane na tuliyemuona kama alama ya upinzani na demokrasia nchini kumbe naye ni mpinzani ndani ya chama na mminya demokrasia.

Heshima yote niliyokuwa nampa Mbowe nimeiondoa jana.

Tutakuwa na hoja gani endapo Rais aliyeko madarakani akiadhimia kuongeza muda?
 
Umechelewa sana kujua hawa jamaa wako planted na serikal
 
Yaani huyo mzee mbowe ni mbinafsi sana kakubali kuwa kibaraka wa sa100 kwenye chama kikuu cha upinzani
 
Matapeli wanaondoka chadema mmoja mmoja, katiba yenu inatoa uhuru wa kugombea kwa kila mtu, kwa nini mnashinikiza mtu asitumie haki yake ya kikatiba? Nyie ndio mnasema katiba mpya ni suluhisho wakati hiyo ya kwenu hamuheshimu? Kwa nini mminye haki ya Mbowe kugombea? Kila mtu auze sera, wananchi wataamua
 
Tangu lini uliwahi kumuunga mkono Mbowe na Chadema? Mbona siku ile ya maandamano Mbowe alikuwa peke yake na bintiiye tu? Eti leo sikuungi mkono! KUMBAVU!!
 
Karibu CHAUMA nimekuwekea sitina sahani ya ubwabwa
 
Usimtaje tena huyo kirusi karibu Chauma
 
Mkuu uko sahihi mno mno. Mbowe nanadhani ameona maisha yake ya kisiasa yanafikia ukingoni, basi akaamua chama kife ili tu yeye afaidike. Miaka 20+ kwenye uenyekiti halafu anasema eti bado kuna kazi hajamalizia. Ni kama Samia alipokuwa anaambiwa katiba ni muhimu anasema tumpe muda alete maendeleo kwanza. Tushukuru sana hakuweza kuwa rais alipogombea kwani angekuwa rais wa maisha.
 
Mbowe yupo kwenye dili la kuwamilikicha WAZANZIBAR WAPUMBAVU NCHI YA TANGANYIKA
 
Naunga mkono hoja.
CHADEMA chini ya Mbowe imepoteza mwelekeo imekosa agenda hawajui hta wanapigania kitu gani.
Mabadiriko ya kweli yataletwa na umma wenyewe ukichoka madhila ya kuwa chini ya utawala wa chama kimoja Kwa muda mrefu.
Tusiwategemee hawa wanasiasa wenye ndimi mbili ambao kwao kipaumbele ni MATUMBO YAO na sio kuwa sauti ya wanyonge.
NB:Vijana msikubali kutumika na hawa wahuni wahuni CHADEMA mtakufa na kupata vilema vya kudumu huku wao wakifurahia kunywa mvinyo mwekundu na hawa watesi wetu.
 
Hata mm ni chadema toka enzi za Ndesa niko Moshi na chaguzi zoote kura yangu huws ni chadema.
Ila ktk hili mbowe ameniudhi na kunikatisha tamaa kabisa kwa kung'ang'ania kwake madaraka.
Uchaguzi mkuu ujao sitapiga kura popote labda Mbowe ashindwe na hilo sitegemei kutokea kwakuwa wajumbe wengi watakuwa ni machawa yake.
Ila uchaguzi ungekuwa unaamuliwa na wanachama Mbowe angeaibika kwa kura ambazo angeambulia!!.
 
Ukimtoa majalaana samia bushiri kwenye hili umesha jichanganya tena unakuwa ujatumia akili ..leo mbowe akiitisha maandamano ya kumuunga mkono abaki madarakani bila hata ya kibari cha polisi yatafanyika bilashida yoyote tena hadi polisi waliovalia gwanda za chadema wataongeza nguvu ili kuonyesha kuwa muhuni mbowe anakubalika ...sasa jiulize kwanini?
 
Lissu alikuiteni tarehe 23/9 sijui mlikuwa wapi ndio alipanga kumpindua Mbowe!
 
Ni furaha kubwa mbinguni mwenye dhambi mmoja akitubu,vivyo hivyo ni furaha kubwa duniani nyumbu mmoja akijitambua na kuacha unyumbu!。
Karibu tena uraiani kama binadamu kutoka kwenye umnyama nyumbu!。
P
 
Naunga mkono hoja mkuu tupo pamoja 💯💯💯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…