Kwa hesabu zangu Makusanyo ya DP World bado yapo chini kulinganisha na miaka ya nyuma 2019/20

benignusmulisa

Senior Member
Joined
Feb 4, 2014
Posts
138
Reaction score
140
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amedai DP World kwa miezi mitano tangu ianze kazi imekusanya Bilioni 325. Hii ni sawa na Bilioni 65 kwa wastani wa kila mwezi mmoja.

Natuzingatie hii ni miezi yenye meli nyingi na mizigo mingi. Kwa mwaka wa 2019/2020 Serikali ilikusanya Bilioni 901 kwa mwaka (12 miezi). Hii ni sawa na Bilioni 75 kwa wastani wa kila mwezi mmoja (1) kwa miezi 12.

Hapa kuna tofauti ya Bilioni 10 kwa kila mwezi. Source google mapato dar Port 2019/2020.

Ushauri: DP World walete mitambo hasa ya kupakua mizigo kutoka kwenye meli. Offshore gantry cranes. Wameleta mitambo ya kupanga container sio kupakua. Bandarini inaonesha bado wanatumia mitambo ya TICTS na ile mipya miwili ya Serikali. Kimakusanyo wamekuwa chini. Mungu ibariki Tanzania muhimu tuzingatie facts..
 
Mwarabu atoke kwake aje kuwekeza pesa zake then ufaidike wewe? Humjui mwarabu nyie.
 
Kumbuka pale Kuna dp world, adani na ticts
 
Admin kwenye kichwa cha habari mwaka ni 2019/2020 sio 2029/2020
 
NI KWELI DP WORLD wanatumia quay crane mbili walizochukua TPA, ambapo TPA hawakuwahi kuzitumia kabisa.

Pia DP World wameleta Terminal Trucks kama 20 hivi na used Rubbered Tyre Gantre ( RTG) 8 ambazo ni used.

Pia walileta Harbour Cranes 2 kuu kuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…