Kwa hesabu zangu Makusanyo ya DP World bado yapo chini kulinganisha na miaka ya nyuma 2019/20

Kwa hesabu zangu Makusanyo ya DP World bado yapo chini kulinganisha na miaka ya nyuma 2019/20

Kwani hata hiyo DP World ya hapa ni ya hao waarabu, au ni ya wajanja wa hapa hapa. Usidanganyike boss ni wajanja wa humuhumu.
😀😀😀wametuzunguka. Ila kwa ule mkataba you can think tumepigwa na watu wa nyumbani
 
Kumbuka pale Kuna dp world, adani na ticts
Hiyo ni jumla ya kinachotokana na bandari, hao uliowataja aapo included.

Wewe nakumbuka last week tulibishana siku nzima kuhusu dola kushuka. Sasa hivi inapanda kwa kasi je tumeacha kununua madini? Export values zimeshuka? Tumeacha kuuza korosho? Nadhani sasa hivi utaelewa sababu za kweli zilizofanya ishuke na sababu zinazofanya ipande kwa kasi
 
Still haya si mapato ya Bandari bali mapato ya Bandari Yaliyotokana na Dp world, huna Data za TPA after Q1 mwaka huu?
Kuna vitu unachanganya. Hayo mapato ni ya Dar port ambayo ipo chini ya Dp world. Ambapo ndio wamekusanya bil 325 kwa mwezi.

Mapato ya TPA kwa ujumla yanajumuisha na ports zingine ambazo hazipo chini ya Dp world
 
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amedai DP World kwa miezi mitano tangu ianze kazi imekusanya Bilioni 325. Hii ni sawa na Bilioni 65 kwa wastani wa kila mwezi mmoja.

Natuzingatie hii ni miezi yenye meli nyingi na mizigo mingi. Kwa mwaka wa 2019/2020 Serikali ilikusanya Bilioni 901 kwa mwaka (12 miezi). Hii ni sawa na Bilioni 75 kwa wastani wa kila mwezi mmoja (1) kwa miezi 12.

Hapa kuna tofauti ya Bilioni 10 kwa kila mwezi. Source google mapato dar Port 2019/2020.

Ushauri: DP World walete mitambo hasa ya kupakua mizigo kutoka kwenye meli. Offshore gantry cranes. Wameleta mitambo ya kupanga container sio kupakua. Bandarini inaonesha bado wanatumia mitambo ya TICTS na ile mipya miwili ya Serikali. Kimakusanyo wamekuwa chini. Mungu ibariki Tanzania muhimu tuzingatie facts..
Nasikia kuna hasira sana juu ya bandari ila wanasubiri muda ufike walisanue hahaha kuna mtu atafia gerezani Mungu bariki mfumo
 
Kuna vitu unachanganya. Hayo mapato ni ya Dar port ambayo ipo chini ya Dp world. Ambapo ndio wamekusanya bil 325 kwa mwezi.

Mapato ya TPA kwa ujumla yanajumuisha na ports zingine ambazo hazipo chini ya Dp world
Dar port haipo chini ya Dp world, Dar port toka zamani imegawanyika, nimewahi Fanya kazi ICD fulani hapo Bandarini kulikua na mizigo inatolewa na Ports gati za mwanzo mpaka 5 kama bado kumbukumbu zipo sahihi, na gati nyengine walikua TICTS.

Sehemu ambayo Bandari wenyewe walikua wanasimamia ndio wame pewa Dp world, sehemu ambayo TICTS walikuwa wanasimamia ndio wame pewa Adani Group.

So kupata Mapato ya Bandari Dar lazima ujumlishe Gati zote including Adani.
 
Wala sio pesa za kampeni. Kampeni haitaji pesa nyingi kama unavyofikili. Lowassa alitumia pesa yake na akafanya kampeni kubwa tu. CCM kwa mapato yake ya majengo inaendesha kampeni vizuri tu.
Ndio maana huwa wanavunja BoT kwa sababu hela zao zinatosha au sio!? Sawa!
 
Dar port haipo chini ya Dp world, Dar port toka zamani imegawanyika, nimewahi Fanya kazi ICD fulani hapo Bandarini kulikua na mizigo inatolewa na Ports gati za mwanzo mpaka 5 kama bado kumbukumbu zipo sahihi, na gati nyengine walikua TICTS.

Sehemu ambayo Bandari wenyewe walikua wanasimamia ndio wame pewa Dp world, sehemu ambayo TICTS walikuwa wanasimamia ndio wame pewa Adani Group.

So kupata Mapato ya Bandari Dar lazima ujumlishe Gati zote including Adani.
Mkuu hiki ulichoandika upo serious? dp world ndio operator wa dar port, lazima kazi zingine zitakua subcontracted kwa wengine. Kwani tuliposema dar port ipo chini ya TPA maana yake wale TICTS hawakuwepo bandarini?

Pili unasema ulifanya kazi ICD fulani hapo bandarini? Ni ICD gani hiyo? Pia unaelewa maana ya ICD/ bandari kavu?? ICD inakuwaje bandarini? Unataka kuleta uongo sio?

Kwenye mapato hapa ni kwamba hujaelewa? Hayo ni mapato ya jumla ya bandari ya Dar including hizo areas zote. TPA wameweka all revenues collected from dar port. Au fanya kutafuta hayo mapato kutoka adani terminals uyalete hapa, uone kama utayapata. Sasa unataka kusema hayajumuishwi popote yanapotelea hewani?

Ni kwamba unaona hayo mapato ya bil 325 kwa miezi mitano ni kidogo???
 
Back
Top Bottom