Kwa heshima na Tahadhima tunaiomba Serikali yetu sikivu ya JMT ianze kuipa muundo wa kiutumishi na mshahara Masters/PhD degree

Kwa heshima na Tahadhima tunaiomba Serikali yetu sikivu ya JMT ianze kuipa muundo wa kiutumishi na mshahara Masters/PhD degree

Hongera mkuu, endelea kuchapa kazi ipo siku ushauri wako utafanyiwa kazi

Zipo taasisi za kitaaluma Zina uhitaji wa rasilimali watu wenye elimu kama yako na kuendelea

Hivyo nakushauri ungeanza na huko kwa kutafuta nafasi ya kuamia huku ukiendelea kufikisha mawazo yako kuhusu namna bora ya kuwa tumia watu wenye elimu kwenye vyeo fulani kimuundo

Una hoja na nina Imani ipo siku wazo na hoja yako itafanyiwa kazi...
 
Tunataka tija ya hiyo masters ako na siyo cheti, watumishi wa umma nyie ni wajinga sn, kutwa kujisifia elimu badala ya kufanya kazi mzalishe wananchi wapate unafuu wa maisha nyie ni maigizo ya masters. Haya tangu umemaliza masters umefanya nini cha tofauti na wenye degree? au ulitaka tujue kuwa una masters hapa? Masters yenyewe assignments + research ulifanyiwa ulichofanya ni kutoa hela tu. Shame on you
Umegusia kitu cha muhimu sana, yaani nimesoma ujumbe mwanzoni kabisa nimekutana na neno TIJA. Hili ni neno fupi lakini ni mada pana sana. Taifa lina watu wengi sanaa waliosoma kwa ngazi tofauti tofauti, wameajiriwa maeneo tofauti tofauti. Lakini ni muhimu kuona tija ya kila mtu kwenye eneo lake la kazi hadi nyumbani kwake kupitia hiyo elimu yake. Ni mambo ya upuuzi taifa leo hii kina watu wengi waliosoma lakini bado ukipita kwenye makazi ya watu kwenye mitaa mingi takataka zimezagaa. Magonjwa ya mlipuko bado yanalisumbua taifa hii ni hatari. Ina maana hakuna tija hata ya elimu msingi ndani ya taifa letu??
 
Mkuu ukikaa na watumishi wa umma kupiga story ndiyo utagundua elimu haina thamani yaani wao akili zao zinawaza mishahara badala ya kuhudumia jamii kwanza(legacy), then maslahi yatakuja menyewe, kama uzalishaji ni mkubwa maanake wananchi watafaidi watalipa kodi na mapato ya nchi yataongezeka na mishahara ipatanda, ni aibu unaenda karibu ofisi nzima ya halmashauri watu wana masters lakini tija ni zero, why tuna gas, tanzanite, mito, mabwawa, makaa ya mawe, ardhi nzuri ya kilimo, mbunga za wanyama, bahari, maziwa, milima, misitu, mabonde mazuri, madini ya kila aina, mifungo kibao na watu wa kutosha lakini tumeshindwa kuvitumia sababu ya elimu yetu ya kijinga haitusaidii, anakuja mchina na diploma anakuja kuchimba makaa ya mawe lakini kuna jitu lina masters halijui hata linafanya nini duniani. Hovyo kabisa tuwekeze kwanza kwenye ujuzi tuweze kutumia rasilimali zetu zinufaishe jamii badala ya kunufaika binafsi.
 
Ni ubinafsi tu umemjaa yeye anawaza mishahara tu
Yeye na wewe nani mbinafsi?

Yeye anataka malipo kwa kazi anayoifanya, wewe hutaki alipwe kwa kazi anayoifanya

Na huna cha kushauri ili kuboresha au kueleweshwa pale ambapo wewe unahisi una gap bali unakuja kumvamia na kumuita mbinafsi.

Mei mosi inakuja inawezekana kutakuwa na mabango ya kuomba nyongeza ya mishahara, posho, vyeo, mafao na stahiki zingine

Tuna kuomba na wewe uweze kuja na bango lako la kupinga nyongeza za mishahara na stahiki zingine kwa wafanyakazi
 
Shukrani Sana mkuu🙏🏿
 
Back
Top Bottom