Kwa hiki wanachokifanya DP WORLD bandarini, maadui zetu wakubwa ni viongozi wetu walioruhusu upuuzi kudumu muda mrefu

kwa lugha nyepesi bandarini kuna maboresho kwenye utendaji au kazi zimeendelea kusuasua?
Umeuliza vyema, maana na mimi baada ya kusoma kichwa cha habari na yaliyomo nimeshindwa kuelewa nini ni nini.
 
Unafikiri pale bandari kuna cha maana , urasimu pale wa kuchelewa ilikuwa ni awatu wenyewe ...Wale wafanyakzi ambao sasa wapo Dp world ndio hao hao wanapiga kazi maana huku wanaweza kutimuliwa.

Hakuna cha maana zaidi ya kubweteka kwa watanzania , kufanya kazi kwa mazoea ...Lazima wamuogope Muarabu wafanye kazi .

Kama tungekuwa na utaratibu wa kuwa na DG kutoka nje labda wachina , wazungu , wahindi , basi wabongo wangefanya kazi kwa shuruti tungefika mbali sana .​
Na hiyo ndiyo sifa ya mtanzania, halafu boss ukiwa mkali unaonekana mkorofi.
Hata hizi idara za taasisi za serikali ukisimamia kazi vizuri hutaki utani unaletewa zengwe mpaka kulogwa🤣🤣
Niliwahi pigwa tukio sitasahau kila kipimo hola nikanyosha mikono for the first time I had to visit a spiritual watchman (napunguza makali ....)....Ni bagamoyo hapo. God forgive me.
 
Kitu ambacho hujajua ni kwamba kuna biashara ya wenye meli kulipwa demurage charges. Meli inapocheleweshwa bandarini malipo yake ni makubwa sana kwa siku. Ukiwa na management ya bandari ya wala rushwa kwa kushirikiana na baadhi ya wenye meli huhakikisha mzigo haushushwi mara moja ili meli kulipwa gharama za ucheleweshaji. Kwa hivyo mambo ya bandari sio rahisi eti unampa mwekezaji tu kuendesha unaketi akupe hela. Hakika tutapigwa tu maana tumekubali mfumo wa wajanja ruksa kula vya umma.
 
Kwa asiye na akili ataona ubinafisishaji umeleta manufaa kumbe tumeuza raslimali yetu Kwa mgeni Kwa mapungufu ambayo tulikuwa na uwezo wa kuyarekebisha. Na haya ndo maoni ya Wanaharakati Tangu mwanzo, tusibinafsishe kitu ambacho tunaweza kukiendesha Sisi wenyewe. Ni kama magari ya Halmashauri yanavyokuwa grounded Kwa ukosefu wa ball joint na baadaye gari Hilo linauzwa Kwa Mtu binafsi anakwenda duka la spare ananunua kipuri anapeleka Kwa fundi gari linatembea zima kabisa ndani ya siku 2 wakati limekaa juu ya Mawe miaka 2. Hii ndo CCM na tiss usiwaguse wanatafuta Vijana wanaoandika kinyume na serikali mitandaoni.
 
Kwa hiyo hapo DP World ameongeza ufanisi au ameharibu?

Wewe tuambie Je Mapato ya Bandari kwenda Serikalini yameoungua au hapana? Kama hayajapungua shida Iko wapi?
 
Nilishangaa sana kuona watanzania wanaagiza mizigo kupitia bandari ya Mombasa.Kiufupi Huo uwekezaji wa dp world ni wa kinyonyaji.
 
Kwa asiye na akili ataona ubinafisishaji umeleta manufaa kumbe tumeuza raslimali yetu Kwa mgeni Kwa mapungufu ambayo tulikuwa na uwezo wa kuyarekebisha. Na haya ndo maoni ya Wanaharakati Tangu mwanzo, tusibinafsishe kitu ambacho tunaweza kukiendesha Sisi wenyewe. Ni kama magari ya Halmashauri yanavyokuwa grounded Kwa ukosefu wa ball joint na baadaye gari Hilo linauzwa Kwa Mtu binafsi anakwenda duka la spare ananunua kipuri anapeleka Kwa fundi gari linatembea zima kabisa ndani ya siku 2 wakati limekaa juu ya Mawe miaka 2. Hii ndo CCM na tiss usiwaguse wanatafuta Vijana wanaoandika kinyume na serikali mitandaoni.
Umesema kitu cha maana. Sasa tumeona tunakwama kwa mambo madogodogo ya utekelezaji. Kwa hivyo ni mambo ya uzembe wa utendaji. Ni kukosekana usimamizi imara wa serikali kuanzia rais wizara, bodi za ulaji tu za wakurugenzi etc. Kwa ujinga au udhaifu tunawapa wageni mali zetu kama kwa bure kabisa.
Kwa asiye na akili ataona ubinafisishaji umeleta manufaa kumbe tumeuza raslimali yetu Kwa mgeni Kwa mapungufu ambayo tulikuwa na uwezo wa kuyarekebisha. Na haya ndo maoni ya Wanaharakati Tangu mwanzo, tusibinafsishe kitu ambacho tunaweza kukiendesha Sisi wenyewe. Ni kama magari ya Halmashauri yanavyokuwa grounded Kwa ukosefu wa ball joint na baadaye gari Hilo linauzwa Kwa Mtu binafsi anakwenda duka la spare ananunua kipuri anapeleka Kwa fundi gari linatembea zima kabisa ndani ya siku 2 wakati limekaa juu ya Mawe miaka 2. Hii ndo CCM na tiss usiwaguse wanatafuta Vijana wanaoandika kinyume na serikali mitandaoni.
 
Wananzengo, mu Hali gani?

Kwa masikitiko makubwa Leo nawatangaza hadharani maadui wakubwa wa taifa letu.

Laiti tungekuwa na uongozi imara tungekuwa mbali sana kwenye mafanikio ya kiuchumi.

DP WORLD wamepewa bandari bure, wamepewa na vitendea kazi bure. Leo wameongeza Terminal Trucks kumi na trailers 27. Wameleta Rubbered Tyred Gantre (RTG) nane. Na sasa hamna meli inakaa mwezi mzima dock ikisubiri foleni. Container ships zinaingia moja kwa moja kupakua mzigo.

Pia soma: DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

Walichofanya DP WORLD ni kujaza vipuri kwenye warehouse, TPA wao hawakuweka kipuri hata kimoja warehouse, hadi magurudumu yakiisha kwenye Rich Stacker, wanatafuta Rich Stacker mbovu wanaivua gurudumu.

Viongozi wetu walikuwa wanayaona haya lakini wakishirikiana na CCM wakawa wanachukulia poa sana.

Mapapapa fisadi wa CCM wakanunua Quay Crane mbili kwa mabilioni ya pesa, kwa miaka nenda rudi hizo QC hazikufanya kazi, wamekuja DP WORLD wamenunua jenereta mbili, QC zinafanya kazi sasa, wamepata bure.

Folk lifts zinakuwa grounded kwa kukosa matairi; ni aibu gani hii?
Kama nimeelewa haya maelezo unamaanisha endapo kungekuwa na viongozi wafuatiliaji, wawajibikaji, wanaopenda maendeleo na kujua wanachokifanya kulikuwa hakuna haja ya kuwaleta hawa DP WORLD kwasababu "ni kama" kila kitu kilikuwepo kilichofanyika ni kuwakabidhi tu wafanye kazi

Kama hivyo ndivyo, mimi nakubaliana na wewe kwasababu ni kweli tuko hapa si kwakukosa rasilimali vitu bali kwa kukosa rasilimali watu inayowajibika

Juzi nimemsikia Tibaijuka anasema alikataa kusaini ujenzi wa karakana ya mwendokasi iliyojengwa pale jangwani lakini hatimaye ilijengwa. Sasa jiulize mamilioni mangapi yameteketea pale?

Kuna upuuzi mwingi ukiufuatilia utaona jinsi tulivyo na viongozi ambao hawako serious. Kila sehemu wao wanaingiza siasa siasa, kujuana, kutegeana na kutengenezeana ajali tu

Ni dhahiri kabisa DP WORLD watapandisha mapato ya TPA, lakini haitaondoa ukweli kwamba watatucheka kwa kujipatia utajiri kwa bei rahisi maana watakachovuna ni kikubwa kuliko kitakachobaki
 
Kwa hiyo hapo DP World ameongeza ufanisi au ameharibu?

Wewe tuambie Je Mapato ya Bandari kwenda Serikalini yameoungua au hapana? Kama hayajapungua shida Iko wapi?
Naomba kuuliza jamani msinicheke please! Hivi gharama walizotumia dpw kuboresha bandari zinatofautiana na gharama za Pikipiki zilizogawiwa 700 kila mkoa za SSH2025? Kama zinakaribiana Kwa nn hatukuzitumia hizo kuboresha bandari zetu! Tanzania bwana!!!!!
 
Gharama wewe unazijua za hicho ulichoandika?
 
Wafanyabiashara wenaotumia bandari na wafanyakazi wa TPA ndio wenye nafasi ya kuthibitisha haya unayoyasema
 
Ashukuriwe Rais Samia kwa kuleta maboresho ya bandari.

Wewe ni lower thinker. Nchi hii inahitaji maboresho ya uongozi na wala siyo upuuzi wa kuwaleta watu wanaoitwa wawekezaji wakati wanakuja kutumia kila kitu mlichogharamia ninyi wenyewe, lakini kutokana na uongozi dhaifu mnawapa utajiri wa bure wageni ambao hawawekezi chochote cha maana.

Wawekezaji wa kweli, ambao wana mitaji na tekinolojia bado wanahitajika, lakini siyo huu upuuzi wa DP World. DP World kama ni wawekezaji kweli wapewe eneo wakajenge bandari mpya. Siyo huu utapeli wanaoufanya kwa kushirikiana na watawala dhaifu.
 
Kwani kabla ya DP world si mlikuwa nyie watanzania. Kipi mlichofanya zaidi ya urasimu, wizi na rushwa.
 
Kwa asiye na akili ataona ubinafisishaji umeleta manufaa kumbe tumeuza raslimali yetu Kwa mgeni Kwa mapungufu ambayo tulikuwa na uwezo wa kuyarekebisha. Na haya ndo maoni ya Wanaharakati Tangu mwanzo, tusibinafsishe kitu ambacho tunaweza kukiendesha Sisi wenyewe. Ni kama magari ya Halmashauri yanavyokuwa grounded Kwa ukosefu wa ball joint na baadaye gari Hilo linauzwa Kwa Mtu binafsi anakwenda duka la spare ananunua kipuri anapeleka Kwa fundi gari linatembea zima kabisa ndani ya siku 2 wakati limekaa juu ya Mawe miaka 2. Hii ndo CCM na tiss usiwaguse wanatafuta Vijana wanaoandika kinyume na serikali mitandaoni.
Tangu uhuru tunaendesha wenyewe kipi cha maana kimeweza kupatikana?.

Mswahili ukimpa aendeshe sehemu anaanza kuwazia kufanya ufisadi na kutanua mabega na masuala mengine ya ukabila yanazaliwa humo humo.

Acha DPW wapige kazi ili tuondokane na huu urasimu wetu mwingi, mswahili pia akiona anafanyia kazi shirika la umma anakosa kabisa uzalendo.

Hatuna uwezo wa kujiendesha wenyewe, na katika mkataba wa DPW kuna kipengele cha kuhakikisha anaongeza tija ya wafanyakazi kwa kuwapa maarifa ya masuala mazima ya usafirishaji wa bandari (shipping).

Hao wanaharakati wanatumiwa na mafisadi katika kutetea malengo yao ya kishenzi.
 
Back
Top Bottom