Nauomba Uongozi wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) haraka sana umchukulie hatua kali za kinidhamu mtangazaji wa hovyo wa michezo nchini Maulid Kitenge kwa kitendo chake cha kumpa 'Airtime' Mhamasishaji Mkuu wa Yanga SC Haji Manara tena akimtaja kabisa kuwa Msemaji wa Yanga SC aliye kifungoni.
Niliwahi kusema hapa hapa kuwa mtangazaji huyu wa hovyo na mwenye Uyanga uliopitiliza na anayetumika vibaya na matajiri wa Yanga SC, wadhamini wao GSM ipo siku atakuja kujikuta pabaya au hata pia kuigharimu kampuni yake yenye chombo hicho husika cha EFM.
Kwa kitendo 'very unprofessional' alichokifanya Mtangazaji Maulid Kitenge wa EFM cha kuweka hewani 'clip' ya Haji Manara (ambaye anajua yuko kifungoni sasa) na amekiri mwenyewe kwa kusema (Msemaji wa Yanga SC aliyekifungoni) ni kuidharau na kuikejeli TFF na pia ni kutaka kuiweka Media ya EFM anayoifanyia kazi kwa sasa.
Nauomba Uongozi wa TFF haraka sana umchukulie hatua kali Mtangazaji wa EFM Maulid Kitenge kwa hiki alichokifanya na sina shaka kuwa amekifanya makusudi kutokana na kutumika kwake vibaya na matajiri wa Yanga SC akina GSM, Uyanga wake na uswahiba wake mkubwa na mnafiki mwenzake (mwenzie) Haji Manara.
Alichokifanya Mtangazaji Maulid Kitenge ni kiburi, dharau na jeuri kwa mamlaka ya soka nchini Tanzania, hivyo achukuliwe hatua haraka ili iwe fundisho kwa watangazaji wengine wapuuzi na 'very Unprofessional' kama yeye na tasnia iheshimike.