Kwa hili la Bandari nipo 'Neutral' kwa mtazamo ufuatao

Na wanaweza wakaipitisha hata tukipinga maana wao ndio last say
Hili ni wazi kabisa. Ila nakuhakikisha hata wakipisha (na likely ndiyo itakavyokuwa) basi itakuwa ni mwanzo wa Tanzania kuingia kwenye zama mpya..... Jambo linalofanyika kwa nguvu na rushwa namna hii halina future nzuri. Na zaidi, kupitisha mkataba kama huu siyo kuwa ndiyo mwisho wa mambo. Mkaburu na kujenga kote waliondoka iwe kuja hawa waarabu?
 
Hili jambo sio la kuwa neutral hata kidogo, hii ni dalili ya woga na kujipendekeza.

Hawa watu hawana malengo mazuri na Rasilimali zetu hatupaswi kuzungumza nao kwa lugha ya kidiplomasia.

Inatupasa kuwa wakali ili kuwapa ujumbe kuwa walichokifanya ni makosa.
Yaaah mim kwahili Nipo tayarii ikibidi HATA damu zimwagike maana Tanzania wogaa huwa unatuponza Sana hamna taifa lililo endelea kwaamani
 
Mtazamo Chanya...

1. Bandari itaboreshwa
2. Ufanisi Kuongezeka
3. Biashara Kuimarika
4. Maslahi juu kwa Wafanyakazi
5. Huduma yao itavutia nchi nyingi Jirani
6. Mapato Kuongezeka
7. Urasimu Kupungua

Mtazamo Hasi

1. Mkataba kutokuwa na Ukomo ni Hatari kwa wenye Bandari
2. Vipengele vinachojichanganya Kimaelezo vinaleta Wasiwasi
3. Kwanini hakukuwa na Mchakato mrefu unaohusisha hata Wananchi ili Kuuelewa?
4. Msemaji wa Serikali badala ya Kuelezea Kiundani muda mwingi anautumia Kufoka. Kukosoa na kutuonyesha Watanzania kuwa hana Akili
5. Tunatulizwa kuwa DP World wako hadi Uingereza ila hatuambiwi kwanini katika Mataifa mengine Wameshindwa
6. Wanasiasa kuingilia Kutetea Mpango huu kunaongeza Shaka kuwa huenda tatizo halipo tu katika Mkataba na DP World bali hata Akili za Wanasiasa Wetu ( hasa Wabunge wa CCM ) nazo zina tatizo
7. Spika wa Bunge kutumia muda mwingi Kuvitishia Vyombo vya Habari vya Tanzania juu ya Kuandika kuhusu huu Mkataba wa DP World na Bandari yetu kunaonyesha kuwa huenda Mihimili Mikubwa miwili imeshalainishwa Kifedha na Waarabu ili Kuuza Rasilimali za Watanzania na Watanzania wenyewe

Nini Kifanyike?

1. Mchakato juu ya huu Mkataba uanze upya na uhusishe Watanzania Wote
2. Lugha ya huu Mkataba iwe ya Kiswahili ili hata tusiojua Kiingereza akina GENTAMYCINE tuuelewe
3. Watanzania tuwe Wavumilivu juu ya Ufadanuzi utakaolewa
4. Wanasiasa na Wabunge wasiwe Wasemaji Wakuu wa hili bali Wataalam wasio na upande ndiyo Wasikilizwe
5. Rais, Waziri na Msemaji wa Serikali wasione Aibu kuwaomba Radhi Watanzania juu ya hii Sintofahamu inayoelekea kuzaa Chuki na Hasira kwa Wadau na Wananchi
6. Tubakie na Utanzania Wetu na kamwe tusianze Kubaguana Kimakabila na Kijiografia kwani Sisi sote ni Watanzania
7. Wale Wanaotetea huu Mkataba wa DP World wasionekane ni Maadui kwani nao wana Hoja mahala lakini pia na wale ambao Wanaukosoa huu Mkataba wasipuuzwe, wasidharauliwe bali Hoja zao nazo zipimwe kisha kwa upamoja Wao kupatikane muafaka thabiti ya huu Uwekezaji wa hawa DP World kama Wawekeze au Wasiwekeze.

Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ubariki Mtandao huu wa JamiiForums
Mungu Mbariki mno GENTAMYCINE

AMINA.
Tatizo wanaotetea ..badala ya kufafanua wao wanafoka ,hii pekee hata Mimi ambaye sijasoma kinayia mashaka kuwa hili ni bomu!
 
Daah wee nimtanzania kweli au mkataba hujausomaa
Rudia kusoma nilichandika. Najua nchi yetu tuna changamoto ya watu kusoma kwa ufahamu. Watu wengi hawaelewi hata wakisoma. Kwa kifupi nimesema mkataba ni mbaya kuliko shetani na haufai kabisa lakini umefanywa hivi kwa sababu hakuna mtu anayekuja kukujengea nchi yako wakati wewe umekaa kwenye kiti cha uvivu.
 
Hili ni wazi kabisa. Ila nakuhakikisha hata wakipisha (na likely ndiyo itakavyokuwa) basi itakuwa ni mwanzo wa Tanzania kuingia kwenye zama mpya..... Jambo linalofanyika kwa nguvu na rushwa namna hii halina future nzuri. Na zaidi, kupitisha mkataba kama huu siyo kuwa ndiyo mwisho wa mambo. Mkaburu na kujenga kote waliondoka iwe kuja hawa waarabu?
Makaburu waliondika wapi aisee!?
 
Bandari ni shamba la bibi, hao nao watabeba mali asili zetu na madini kuhamishia nchi zao kupitia bandarini, wapo huru sasa.

Kuirudisha bandari itabidi mtutu utumike japo itakuwa miaka mingi ijayo.
 
Rudia kusoma nilichandika. Najua nchi yetu tuna changamoto ya watu kusoma kwa ufahamu. Watu wengi hawaelewi hata wakisoma. Kwa kifupi nimesema mkataba ni mbaya kuliko shetani na haufai kabisa lakini umefanywa hivi kwa sababu hakuna mtu anayekuja kukujengea nchi yako wakati wewe umekaa kwenye kiti cha uvivu.
So sorry nliskim but ulichokianfika nisawa Sana mkuu Sasa wasomi tunao wategemea selkalin akiwemo ni speaker wa bunge lakin daaaah so hurt yani
 
Watu wenye akili washashtukia Jambo
Kuna kampeni ya kumchafua Rais na kuweka vipengele vya uongo..
Duniani hakunaga mkataba usio na kikomo......akili ya kawaida Tu inakwambia Dpworld wasingeweza kusaini mkataba wa utata waanze kuwekeza huku wanajua Tanzania hakuna Rais wa milele....kila mara kuna uchaguzi
 
Tumia akili Basi daaa kwasababu raisi kile nicheo naanavotoka nyalaka anaziacha inaonekana watanzania wengi wanaelewa kama wew ndiomana hawalipi uzito hili swala kasome mkataba alafu uje namajibu then nenda kwenye katiba uone principle of sabrogation ili ujue raisi ajae ataingiaje kwenye mkataba ambao hakuusain yeye
 
Mtazamo Chanya...

1. Bandari itaboreshwa
2. Ufanisi Kuongezeka
3. Biashara Kuimarika
4. Maslahi juu kwa Wafanyakazi
5. Huduma yao itavutia nchi nyingi Jirani
6. Mapato Kuongezeka
7. Urasimu Kupungua

Mtazamo Hasi

1. Mkataba kutokuwa na Ukomo ni Hatari kwa wenye Bandari
2. Vipengele vinachojichanganya Kimaelezo vinaleta Wasiwasi
3. Kwanini hakukuwa na Mchakato mrefu unaohusisha hata Wananchi ili Kuuelewa?
4. Msemaji wa Serikali badala ya Kuelezea Kiundani muda mwingi anautumia Kufoka. Kukosoa na kutuonyesha Watanzania kuwa hana Akili
5. Tunatulizwa kuwa DP World wako hadi Uingereza ila hatuambiwi kwanini katika Mataifa mengine Wameshindwa
6. Wanasiasa kuingilia Kutetea Mpango huu kunaongeza Shaka kuwa huenda tatizo halipo tu katika Mkataba na DP World bali hata Akili za Wanasiasa Wetu ( hasa Wabunge wa CCM ) nazo zina tatizo
7. Spika wa Bunge kutumia muda mwingi Kuvitishia Vyombo vya Habari vya Tanzania juu ya Kuandika kuhusu huu Mkataba wa DP World na Bandari yetu kunaonyesha kuwa huenda Mihimili Mikubwa miwili imeshalainishwa Kifedha na Waarabu ili Kuuza Rasilimali za Watanzania na Watanzania wenyewe

Nini Kifanyike?

1. Mchakato juu ya huu Mkataba uanze upya na uhusishe Watanzania Wote
2. Lugha ya huu Mkataba iwe ya Kiswahili ili hata tusiojua Kiingereza akina GENTAMYCINE tuuelewe
3. Watanzania tuwe Wavumilivu juu ya Ufadanuzi utakaolewa
4. Wanasiasa na Wabunge wasiwe Wasemaji Wakuu wa hili bali Wataalam wasio na upande ndiyo Wasikilizwe
5. Rais, Waziri na Msemaji wa Serikali wasione Aibu kuwaomba Radhi Watanzania juu ya hii Sintofahamu inayoelekea kuzaa Chuki na Hasira kwa Wadau na Wananchi
6. Tubakie na Utanzania Wetu na kamwe tusianze Kubaguana Kimakabila na Kijiografia kwani Sisi sote ni Watanzania
7. Wale Wanaotetea huu Mkataba wa DP World wasionekane ni Maadui kwani nao wana Hoja mahala lakini pia na wale ambao Wanaukosoa huu Mkataba wasipuuzwe, wasidharauliwe bali Hoja zao nazo zipimwe kisha kwa upamoja Wao kupatikane muafaka thabiti ya huu Uwekezaji wa hawa DP World kama Wawekeze au Wasiwekeze.

Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ubariki Mtandao huu wa JamiiForums
Mungu Mbariki mno GENTAMYCINE

AMINA.

Hongera umeandika vizuri na umechambua kwa weledi
Ila penye kila neno Tanzania ungeweka Tanganyika ingependeza zaidi.Asante
 
Tumia akili Basi daaa kwasababu raisi kile nicheo naanavotoka nyalaka anaziacha inaonekana watanzania wengi wanaelewa kama wew ndiomana hawalipi uzito hili swala kasome mkataba alafu uje namajibu then nenda kwenye katiba uone principle of sabrogation ili ujue raisi ajae ataingiaje kwenye mkataba ambao hakuusain yeye

Nyongeza tuu
Kuna mikataba mingapi imesainiwa na marais waliopita kuivunja ni shida?
Sijui watu huwa wanajitoa ufahamu?
 
Kunamikataba inatutesa mbaka leo wakulima wananyang'anywa mashambayao yaliyomo maeneo yamigodi kisa mikataba yakipumbavu hii ilikua starting point kwawatanzania kwan viongozi wanaona wanaongoza watu wasio naakili Ivo wanaamua mambo kilahisi sanaaa
 
Tanzania ni nchi ambayo hata kama unawachapa raia wake viboko ila unalipa kodi basi ruhsa yaani ukilipa kodi unaweza fanya chochote kile.
 
Mimi nashauri mikataba ya uwekezaji iwe inajadiliwa na wabobezi wa Sheria ( TLS) na sio wabungeni ambao wabunge wengi hanawa uelewa wa mambo ya mikataba ya Sheria!!! Wala mambo ya uwekezaji!!
Mheshimiwa msukuma,lusinde sijawalenga nyie
 
Nikweliiii kabisa ila kumbuka tuna mwanasheria mkuu waserkali pia raisi anamwanasheria wake je wanafanya kazigani?
 
Back
Top Bottom