Nimejaribu kumsikiliza na kumsoma alichoongea Mkurugenzi wa Bandari. Kwa maelezo yale Mnunuzi wa Bandari yetu ni Paul Kagame. Angalia huu mtiririko.
1. 2013 anasema angekuwa mmiliki wa Bandari, Tz au nchi yoyote inaweza kujiendesha
2. 2016 anampa ushauri Mzilankende Kuboresha Bandari
3. 2017 Rwanda inakomaza ushirikiano na UAE kwenye sekta ya usafiri.
4. Kati ya 2015 na 2019 Rwanda inaipigia Chapuo Congo kuingia EAC
5. 2017 Tanzania inavunja mahusiano ya kibandari na CONGO DRC
6. 2016/17 Rais wa Tanzania inaamua ghafla kuanza ujenzi wa SGR Kuelekea Isaka. Na kipande Cha Isaka kwenda boda ya Tz na Rwanda
7. 2017 Rais wa Tz anazuia Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo
8. 2018 DP World wanaanza kujenda Dry port kubwa Rwanda.
9. 2021 Panga pangua Zinashika kasi Dar port baada ya Ziara ya Mama Kigali.
10. 2022 Samia anatangaza kubinafsisha Dar Port. Bila kumtaja atakae pewa.
11. 2022/23 Ziara lukuki za wafanya maamuzi kwenda Dubai Zikaongezeka.
12. Ziara ya Ghafla ya PK 2023.
13. 2023 Bunge lachomekewa agenda ya Azimio ambayo haikuwa kwe ye ratiba.
Yajayo.
1. Mizigo itakuwa cleared Rwanda. Magari ya Congo, Uganda, Si lazima tena kuja Dsm
2. Ajira za vijana wa kusafirisha mizigo na magari kuhamia Rwanda.
3. Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kusitishwa Rasmi.
4. Tanzania kuishi kama haina Bandari na Rwanda kuishi kama inapakana na Bahari. PK kuwa na nguvu kubwa ya kuingiza lolote atakalo kupitia Dar Port.
Poleni Wanajeshi wetu mnaopambana kuilinda nchi Congo Na Mozambique. Mmepigwa ndani