Kwa hili la Corona, Magufuli anaenda kuonekana shujaa

Muda utaongea, bado muda kidogo tu mtaelewa kwanini wenzetu wanafungiana ndani. Kwa sasa endeleeni kupongezana.
 
Mara lockdown, Mara kilikwenda kikarudi. Hatua inazochukua serikali zinatosha sana na zinafaa kupongezwa mno. Big up Magufuli kuitisha maombi ya kitaifa. Watu wanasema Corona ni hatari, how? Kwani hadi sasa malaria imeua watu wangapi? Ukimwi he? Hii Corona yenye wagonjwa hata mia hawafiki na vifo viwili vitatu isitupotezee umoja wa kitaifa nchini.

Wanaosema Magufili kajifungia Chato anaogopa Corona pia hawana Hekima. Rais ni taasisi, kuna waziri mkuu anaunguruma kila siku, kuna Mh. Ummy anigana kila siku, watanzania tunataka nini hasa?

Baba Magufuli popote ulipo nakutakia Heri, piga kazi. Corona imeshaisha China, imepungua Ujerumani, inafifia Marekani na hapa Tanzania kwa maombi tunayoendelea nayo imeshakauka. Twendeni kanisani na misikitini, twendeni sokoni, tusali kwa bidii tuchape kazi kwa bidii, Corona itapita na nchi itabaki.
 
Tuacheni visingizio, tuchukue tahadhari lakini tuchape kazi.
 
Kazi apige kweli tunamtakia kila la kheri ila asikae anawaambia watu wakae kuomba tu, awaambie wafate maneno ya wataalamu. Maombi yalikuwepo toka korona haijaja yakashindwa kuzuia isije, sasa kama mnahisi yataondoa korona mnaota ndoto za mchana. Nendeni kanisani na misikitini mkaambukizane nyambafu
 
Sawa mkwe wake
 
bado ni shujaa?

Tanzania leo kuna 94 infections na 4 deaths (4.2% fatality rate karibia sawa na US).

hapo hatujahesabu wanaougulia na kujifia kimya kimya huko mtaani.
 
Maombi Day 1 - wagonjwa wapya 53 , tuendelee kusali na kujificha Chato
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora kukomaa tu na Mungu amfanye shujaa end of the day. In Jesus name amen.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boss are you out of your mind?
 
Mkuu hii strategy ilitumiwa na mzee Kinjekitire miaka hiyo ya giza,Mungu amewapa akiri itumie same way mnavyoitumia kupambana na wanaowakosoa na wapinzani wenu kwenye madaraka,msijitoe ufahamu
 
Kwani tumeshavuka kwenye Janga hili mpaka muanze kupongezana na kusifiana? Tusubiri tuvuke kwanza, mashule yafunguliwe, VPL iendelee, maisha yarudi kawaida kabla vifo zaidi kutokea, kisha ndo baada ya kumshukuru Mungu ndio tutajua nani alifanya nini kufanikisha, kwa sasa naona janga linazidi kuongezeka tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…