Kwa hili la Inyala, Mbeya ninampinga Makamu wa Rais Dr. Mpango kwa agizo lake "quick fix" na kumsihi awe serious na maisha ya Watanzania

Unalionaje agizo la Dr. Mpango?

  • Zuri linafaa sana

    Votes: 4 21.1%
  • Halifai kabisa

    Votes: 15 78.9%

  • Total voters
    19
Yaani madereva wa gari serikali na za viongozi Tz , wengi wao huwa ni ku' jimwambafy' bila sababu za msingi..... matokeo yake ndio haya...RIP Mkurugenzi.
 
Najaribu kuwaza nje ya bokisi. Wakati ule wa biashara ya viungo vya wenye ulemavu wa ngozi/ alibino ilipopamba moto sababu ilikuwa ni nini?
 
Ili upate suluhisho la tatizo kwa usahihi ni lazima nawe uingie uonje au uwe sehemu ya tatizo hilo, viongozi wetu hawaliwezi hilo la kujaribu kuzama kwenye matatizo ili kufeel namna sahihi ya kutatua matatizo.

Hili unaloshauri ni sahihi kabisa nakupa heko, TANROADS walitakiwa kumshauri hivi VP ili kauli yake iwe na mashiko, hao wanaoambiwa wakague malori siyo mafundi na hawana uelewa wowte wa mifumo ya magari makubwa, alichofanya hapo VP ni kupanua wigo wa rushwa.

Nchi hii ina shida kwenye uongozi, haya maamuzi ya kipuuzi ndiyo yaleyale yanayowatesa wananchi mijini kwa kuzuia mabasi kushusha abiria kwenye vituo vya katikati ya miji ukiuliza sababu ni vile wanakuuza ajira kwa bodaboda bajaji guta na daladala wanazomiliki wao which is a very wrong ideology and fixed mindset of politicians
 
Mnaosema gari ikaguliwe kabla ya kushuka mlima mnauhakika kuwa kabla ya gari hiyo kuanza kushuka haikuwa na brake?, je mnajua chanzo kikuu cha magari kufeli brake hapo inyala?.

Kwa nini mlima nyoka hakuna sana ajali zaidi ya hapo inyala/pipe line?.

Gari ishuke mlima nyoka vizuri halafu inyala kumaliza hapo ujue ni uendeshaji pia unachangia na barabara kwa sasa imeshakuwa ndogo hiyo haikidhi vigezo vya kuhimili wingi wa magari yanayopita kwa sasa.

Climbing lane zinahitajika,lay bay na njia za kuepuka ajali kama zile za migodini au hapo imhotep kaweka clip, hayo ndiyo yanayohitajika kwa sasa na wala si sababu za kila siku kusema brake brake.

Madereva wetu wa sasa sio kama wale wa zamani wa kuendesha tani 70 nk siku hizi wanyoa viduku nao wapo kwenye malori na hawa ni tatizo na wala hawashauriki na wala kutaka kujifunza mambo mapya.
 
Siku tukiamua kuanza kutumia wataalamu wa gani husika kwenye matatizo mengi ya nchi hii ili kupata ufumbuzi, hakika mambo mengi sana yatabadilika.
 
We ndiyo hujielewi ht umeandika nn. Ajali ya jana Lori ilifeli breki. Ajali nyingi ubovu wa malori
 
VP kila uchao analishwa matango pori tu, tuwaache wataalamu waje na suluhisho hilo eneo hata mtu wa kawaida tu anaweza kuja na solution, barabara ni mbovu sana na nyembamba.
 
Good analysis Dr Mpango kanogewa na asali siku hizi anajiongelea tu bora liende. Anataka kuwatengenezea Polisi mfereji wa rushwa kwa kisingizio cha kukagua malori wakati hata Sasa wanakagua na ajali ziko pale pale majibu rahisi kwa maswali magumu.
 
Miundombinu Inaruhusu kujihami? Unajihami vp kwenye single carriage road kwenye mteremko? Gari nyingine ikifeli break na kuja kwako unaenda wapi? Unapajua Inyala au?

Common sense isn't common hakika
K 5.
KUONA
Kutambua
Kutabiri
Kuamua
Kutekeleza
 
Mnaambiwa subirini,wao wanajifanya wana haraka

Ova
 
Mie sijaona gari inakaguliwa breki kabla ya kuanza kupanda mlima!

Halafu, Dr. Mpango anasema magari ya mizigo yakaguliwe pale. Ukifika kwenye sehemu za kupima uzito malori yanakuwa mengi sana kusubiri kupima uzito, kitu kinachotumia mashime. Sasa amefikiri hao mafundi , na sijui watakuwa nani, watachukua muda gani kukagua breki? Tutajikuta lori zinakaa pake siku mbili zikisubiri kukaguliwa ili zitelemke au kupanda Mlima wa Inyala! Sasa hilo wazo nalo ni akili kweli?
 
We ndiyo hujielewi ht umeandika nn. Ajali ya jana Lori ilifeli breki. Ajali nyingi ubovu wa malori
Sasa hayo maneno kamwambie Dr Mpango, maana kama lilifeli breki ina maana lingekaguliwa breki zikiwa hazijafeli na lingeruhusiwa kupita. Huwezi hata kufikiri kama tu yule jamaa
 
Mnaambiwa subirini,wao wanajifanya wana haraka

Ova
Mie sidhani wao kuamua kupita ni tatizo. Tusitafute tatizo la karibu. Kwani magari yanapita pale kwa zamu kwa kuwa malori huwa yanafeli breki? Jiulize hilo

Ila najiuliza, huyu dereva nae alikuwa mzanzibari? Hawajazoea mikiki ya barabara kama hizi hawaa, wao trip zao sana sana ndefu kuliko yote ni masaa matatu kama sikosei, hakuna hata kupishana na lori, hakuna milima. Hawa viongozi wanaoletwa bara toka Zanzibar kuja bara wasiwe wanaleta madereva wao.
 
Marlezo yote haya ni hofu ya ukaguzi kwani mnabeba vitu gani?
Hebu tumia akili kidogo wewe. Yaani wewe umefikiria ukaguzi wa kuzuia ajali Inyala ni kukagua lori limebeba nini? I say kuna watu mnajifinya na kulalamika. Halafu unakuta mtu kama wewe eti unaruhusiwa kupiga kura kutuchagulia viongozi!
 
Inasikitisha sana jinsi tusivyoweza kuwa na majawabu sahihi huku kuna lundo la Wataalamu
Kwanza Dr Mpango amejiuliza ukiweka utaratibu wa kukagua malori pale atapata wapi wakaguzi wa kutosha ili kutosababisha msongamano wa malori? Hajafikiria kwamba tunaweza kukuta lori linakaa pale siku mbili likisubiri kukaguliwa ili lishuke au kupanda mlima? Hebu atembelee mizani kwanza aone ikiwa mizani hali ndio hiyo, kukagua breki za malorii itakuwaje. Yatapaki wapi ili yakaguliwe? Nani watakagua? Watalala wapi? Watakula, kunywa na kunya wapi wakiwa katika zoezi hilo? Okay, na lori likikutwa lina tatizo, then what, tutaanzisha magereji pale? Yaani viongozi wanaongea tu, wanatoa tu maagizo "impractical" kirahisi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…