Kwa hili la Mbowe Marekani na Umoja wa Ulaya wamejitia aibu, ni rasmi sasa kuna kitu wanakitafuta Tanzania


Picha ya alichofanya huyo polisi kila mtu kakiona, CCTV footage za hilo tukio la Mbowe umeliona? Huyo polisi huko US kaachiwa kwa dhamana maana sheria zao zinaruhusu, sio hizi sheria za hapa za kukomoana. Suala la kuwa wazungu kuwa juu kuliko sisi, na wamestaarabika kuliko sisi wala halina mjadala. Na hili sio suala la kuwasifia bali ndio ukweli. Narudia tena hakuna mzungu wa kuamini huo uchafu wa polisi, walishaamka zamani sana kwenye huo utoto.

Umejaribu kuandika mambo mengi kwenye uzi wako namba moja, ukidhani utaweza kutuchota mawazo, lakini kwa bahati mbaya tumeshaamka. Kwa huku mitandaoni ile propaganda mfu iliyoandikwa ni kama unapaka rangi upepo. Labda mkawahubirie watu huko mtaani , ambako wanawasikiliza bila ruhusa yoyote ya kuhoji.
 
Ubalozi wa Marekani unayo video ya shambulizi la Mbowe ( nimeiona ) , ukiwekewa utakuwa tayari kuomba radhi ?
 
Hili tukio kwa wenye uwezo mzuri wa kufikiri walihoji uwepo wa red brigade, uwepo wa walinzi nyumbani kwa mbowe
Afadhali angesema tu kateleza kuliko kusingizia mambo, Mungu hapendi uongo.
Suala la ulinzi usilitegemee sana, hasa kwa matukio ya kupangwa. Kwa mfano aliposhambuliwa lissu ni mahali penye ulinzi mkali, na si ulinzi wa watu tu adi camera zakuangalia usalama zilikuwepo.
 
Tuna haja ya kuwaondosha nchini. Wamevuka mipaka katika kuingilia mambo ya ndani ya taifa letu.
 
Mimi siwezi kukubariana na hoja yako kwani kwa sasa nchi yetu kila kitu kipo kisisa mpaka ugonjwa wa corona sisasa tupu hatuambiwi ukweli, polisi wapo kisiasa mf kifo cha mwangosi,Akwilina,shambulio la Tundulisu na mengine mengi tu viko wazi lakini sijaona haki ikitendeka ni propaganda tu ndicho kinachofanya mataifa ya Ulaya na Marekana watilie shaka
 
Kwahiyo unataka tuwaamini hawa policcm waliompiga risasi Akwilina wakawashtaki akina Mbowe?
 
Kama polisi ingekuwa inaruhusu tungeandaa maandamano makubwa kuelekea balozi hizi kuwataka wandoke nchini haraka!!wameua ndugu zetu weusi wakaona ni sawa wala hawakutoa matamko,walimuua Gadhafi wakaona ni sawa,,wanaendelea kuichokoza nchi wanaona ni sawa na tumekaa kimya
 
Policcm na nyinyi mataga wake ndio mnajitia aibu. Siwashangai kwa kumtia aibu hiyo kila njia mnatumia ili mummalize kisiasa Lakin bado yupo vizuri.
 
Wamejitia aibu unadhani nao wanategemea taarifa kutoka jeshi lenu la polisi linalofanya kazi kisiasa?

Wao wanaenda mbali zaidi ndio maana tangu waseme Bashite ananyima watu haki yao ya kuishi kaufyata mkia mpaka leo.

Hamna cha kwenda mbali chochote, tatizo wakati mwingine mko blinded sana na utumwa wa kimawazo. Hili kwenu linachagizwa na imani kuwa, Wamarekani wanaweza kuwapa msaada ya kisiasa kufanya regime change labda. Pambaneni kwa mikakati yenu. Kwenye suala la haki za watu, Wamarekani moral authority yao inaibua maswali kila siku. Wenyewe hawataki kumulikwa na vyombo Vya kimataifa kama ICC wanapofanya unyama na nadhani umesikia Trump kafanya nini jana kuhusu hilo. Soma tu hapo chini.
Trump authorizes sanctions against International Criminal Court officials
 
Wamejitia aibu unadhani nao wanategemea taarifa kutoka jeshi lenu la polisi linalofanya kazi kisiasa?

Wao wanaenda mbali zaidi ndio maana tangu waseme Bashite ananyima watu haki yao ya kuishi kaufyata mkia mpaka leo.

Taarifa zao wanapata kutoka kwa mbowe na zito pamaoja na mange kimambi na ngurumo, sasa hapo si wanaingia chaka?
 
Tuna haja ya kuwaondosha nchini. Wamevuka mipaka katika kuingilia mambo ya ndani ya taifa letu.
Mambo ya ndani ni yapi ?!.
1. Kuua wapinzani wako ?
2. Ni kudhibiti vyama vya upinzani visifanye kazi zao za kikatiba ?.
 
Wewe bado hujaamka kutoka kwenye usingizi wowote wewe bado ni mtumwa kabisa maandiko yako yanathibitisha hilo wazi kabisa.

Kesi zote zinazofanyiwa utafiti na polisi hapa nchini huwa unaletewa video CCTV camera??
Hiyo cctiv camera si ipo hapo nyumbni kwake kwanini wasiitoe wao wenyewe sasa waje wathibitishe??

Heti sheria zao nzuri kuliko za kwetu yaani unakuja hapa kumtetea mtu aliye ua live kwamakusudi kabisa halafu anapewa dhamana, kama sio utumwa kumbe ni nini hicho mkuu.

Katika hoja nilizo zitoa hapo kwenye uzi wangu ni kipi nilicho ongopa hapa.
Kwamba hawakututangazia Ebola au??
Hawakutangaza magaidi hapa kwetu au??

Hawakusema kuwa tutaokota maita mabarabarani au??

Labda ni wewe ndio ambaye hujastaarabika na ndio maana unajiona si kitu mbele ya wazungu nadhani hata wakikuita nyani kama wanavyofanya mara nyingi basi utafurahi tu wewe na utakubaliana nao(kwasababu mwenyewe ndio umekili kuwa hujastaarabika)
Dunia ya 2020 alafu wewe bado unakuja na Imani za ustarabu wa wazungu alafu unasema umeamka!!!
Umeamka kutoka wapi? na sidhani kama unaweza kujitoa kwenye huo utumwa kamwe.
Kama si hivyo basi siasa ndio zimekuharibu wewe.
 
Serikali inahusika,vinginevyo wamkamate mhusika na Bashite kiongozi wao
 
Ubalozi wa Marekani unayo video ya shambulizi la Mbowe ( nimeiona ) , ukiwekewa utakuwa tayari kuomba radhi ?
Wewe ni afisa kwenye ubalozi wa marekani??

Una uhusiano upi na ubalozi wa marekani hadi uione hiyo video ambayo haijatolewa mahara popote??

Na huo ubalozi wa marekani hiyo video wameitoa wapi ina maana wanafanya ujasusi hapa nchini kwetu sivyo??
Kama ni hivo sheria za kimataifa zinasemajekuhusu hilo??
Au sheria hizo zinatuhusu sisi tu wao haziwahusu.??

Kama wameweza kutoa matamko ya hovyo kama yale sasa wanashindwa nini kutoa hiyo video ili kuweka ushahidi wazi tuuone??
mana kama ni diplomasia wamesha iharibu kwa yale matamko yao.
 
Hatuwezi kuwadharau kwa sisi kuendelea kufanyiana unyama. Tungewadharau kwa sisi kufanya vizuri zaidi ya kwa kila sekta.

Unalishikia bango la police yule kumuua George Floyid unasahau hapa kwetu kila siku unasikia police wameua saba !! . Tuwadharau kwa kufanya mambo yetu bora kuliko wao . Si haya mambo ya wasiojulikana
 
Wao Wana mangapi yanayofanyika huko huko kwao hayatolewi majibu mkuu!??
Unaposema huelezwi ukweli kwenye Corona una maanisha nini Mana taarifa ya mwisho tuliambiwa tuna wagonjwa wanne sasa wewe unautaka ukweli upi zaidi??
Au ni ule wa kuokota maiti barabarani ndio huo ukweli unao utaka??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…