Kwa hili la mwaka mmoja wa kifo cha Magufuli, Kanisa Katoliki linapaswa kuona aibu

Kwa hili la mwaka mmoja wa kifo cha Magufuli, Kanisa Katoliki linapaswa kuona aibu

Kupewa sakramenti siyo uthibitisho kuwa yuko mbinguni. Sakramenti hizo ni haki yake kama mkristo, na ni wajibu wa kanisa kuwapa sakramenti hizo wale wanaozistahili, lakini hukumu bado ni ya Mungu mwenyewe.
Mpaka anapewa Sakramenti maana yake anastahili.

Kwanza lazima anakuwa amepokea Sakramenti ya ubatizo ambapo:
01: Anakiri utayari wake wa kumkataa shetani na mambo yake yote na fahari zake zote.

02: Anakiri kusadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi, Mwumba mbingu na dunia.

03: Anakiri kusadiki kwa Yesu Kristo, Mwana wa pekee, Bwana wetu, aliyezaliwa na Bikira Maria, akateswa, akafa, akazikwa, akafufuka katika wafu na ameketi kuume kwa Baba.

04: Anakiri kusadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa Takatifu Katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele.

Ndiposa anakuwa amefunguliwa mlango wa kupokea Sakramenti nyingine. Sakramenti pekee ambayo mtu anaweza kupokea akiwa katika hali ya dhambi ni Kitubio.

Mpaka Magufuli anapokea Sakramenti za Ekaristi Takatifu na Mpako wa Wagonjwa maana yake alikuwa ameshapokea Sakramenti ya Kitubio. Maana yake ni kuwa alikuwa msafi na amekufa katika hali ya neema ya utakaso.

Wewe kama una chuki naye hiyo ni juu yako. Ila mwenzio yupo mbinguni anakula maisha. Pole kwa kuteseka.
 
Basi muombeeni na Mkapa msiwe Bias Kama alivyokuwa huyo mnayemtukuza
Tulimuombea na tunaendelea kumuombea.

Hata Jumapili tutakapokuwa tunamuombea Magufuli tutawaombea pia akina Mkapa, Nyerere na waamini wengine marehemu waliopo toharani.

Hatuna bias wala ubaguzi wowote.
 
Hivi, wewe ni mgeni wa Nchi hii? Unataka uthibitisho gani kuuelezea UOVU wa mtu yule? Binafsi, nilitamani maiti yake IFUKIWE badala ya KUZIKWA!
Tuwekee uthibitisho hapa achana na chuki.

Mbona tukiwaomba uthibitisho maneno yanakuwa mengi?

Weka vithibitisho hapa tukuunge mkono ama tukupinge.
 
Huo ndio ukweli usioacha shaka. Hakuna mwenye muda wa kukudhibitishia ukweli ulikuwa wazi.
Ukweli usioweza kuthibitishwa! 😁

Chuki inawatafuna, na msipotafuta msaada wa Mungu na Wanasaikolojia itawaua.

You guys should move on, muacheni jemedari a-enjoy maisha mbinguni.

Nyie endeleeni na kupiga madili, nchi yenu hii amewaachia.
 
Kanisa ni mali ya waumini, kama linafanya kitu ambacho sio sahihi waumini wanapaswa kukemea
Nenda kakemee huko huko kanisani kama vipi, Yesu alikuja Duniani kwa ajili ya wenye dhambi, kama unaona JPM alitenda maovu, huo ndo muda sahihi wa Kanisa Katoliki kufanya kazi yake ya kitume na siyo kutengeneza visasi
 
Umesahau kuandika alikuwa ibada za jumapili akosi awe Chato, Dodoma, Dar au mji wowote atatafuta kanisa.

Umesahau kusema alikuwa mtu ambae akimtegemea mungu sana

Imani yake ilikuwa kubwa mpaka dakika chache kabla ya umauti tunaambiwa aliitwa padre waombe pamoja.

Na kila mara alitukumbusha kumuomba mungu tunapokuwa na shida.

Hayo yote hapo juu yana ushahidi

Wewe una ushahidi wa mtu ata mmoja ambae Magufuli aliagiza, auwewe zaidi ya story zenu za mitandaoni.

R.I.P shujaa wa ukweli
 
Historia inaonyesha kanisa katoliki lilimwaga sana damu za binadamu, limekata vichwa vya watu wengi, wengine wamechomwa moto, wengine wamekatwa kwa panga mpaka kufa
 
Ukweli usioweza kuthibitishwa! 😁

Chuki inawatafuna, na msipotafuta msaada wa Mungu na Wanasaikolojia itawaua.

You guys should move on, muacheni jemedari a-enjoy maisha mbinguni.

Nyie endeleeni na kupiga madili, nchi yenu hii amewaachia.
Unadhibitisha kwa chombo kilicho huru? Hata Hitler bado tunamzungumzia hii leo, ndio itakuwa yule uchwara?
 
Mlidhani angechukiwa Milele, mlijiaminisha ni Dikteta sababu aligusa Maslahi yenu ila deep down mnamkumbuka, mnatamani arudi walau sekunde moja tu mumwambie 'Samahani', Haiwezekani,

Mna Maumivu ya Nafsi, mnacheka lakini Roho zinawasuta, Magufuli Kipenzi cha Wengi,

Continue to Rest Easy Mzalendo halisi.
 
Mtu mwovu anaombewaje Bwashee? Tymwache atulie mavumbini
Inategemea na namna unavyotafsiri uovu.

Ni kama wale Wabahai wamekatazwa kula nguruwe lakini wakiwa jangwani na hakuna nyama nyingine isipokuwa nguruwe basi wameruhusiwa kula.

Ipo tofauti kubwa kati ya uovu na dhambi.
 
Kwani Mwenyekiti wa TEC anapaswa kuwa na vigezo gani? Askofu (Mkuu) Nyaisonga hana hivyo vigezo?
Tatizo alilonalo huyu Bwana aliyeanziah uzi huu ni chuki yake kwa Magufuli sasa anataka iwe institutionalized.

Kanisa kwanza haliadhimishi bali ni misa ya marehemu kwa desturi za Kanisa.

Hili hufanyika kwa maombi ya mtu au watu na sijaona sehemu yoyote ambako kuna waraka wa TEC kuhusu hii ibada zaidi ya Jimbo kuu la Mwanza.

Chuki ya kiasi hiki dhidi ya binadamu mwenzako ni dhambi pia
 
Inategemea na namna unavyotafsiri uovu.

Ni kama wale Wabahai wamekatazwa kula nguruwe lakini wakiwa jangwani na hakuna nyama nyingine isipokuwa nguruwe basi wameruhusiwa kula.

Ipo tofauti kubwa kati ya uovu na dhambi.
Hv Tanzania kuna Wabahai zaidi ya wale pale Kisutu?😊
 
Umesahau kuandika alikuwa ibada za jumapili akosi awe Chato, Dodoma, Dar au mji wowote atatafuta kanisa.

Umesahau kusema alikuwa mtu ambae akimtegemea mungu sana

Imani yake ilikuwa kubwa mpaka dakika chache kabla ya umauti tunaambiwa aliitwa padre waombe pamoja.

Na kila mara alitukumbusha kumuomba mungu tunapokuwa na shida.

Hayo yote hapo juu yana ushahidi

Wewe una ushahidi wa mtu ata mmoja ambae Magufuli aliagiza, auwewe zaidi ya story zenu za mitandaoni.

R.I.P shujaa wa ukweli
Hivi mkuu... Unaamini kabisa kwamba aliitwa Padre kumuombea?

Jamaa alikuwa in Coma mkuu (hakuwa na ufahamu)... na wakajaribu kwenda hapo kwa nchi jirani wakaambiwa hakuna uwezekano wowote ule wa kupona... Wakageuza kurudi.. anyway ngoja tunyamaze
 
Back
Top Bottom