Kwa hili la mwaka mmoja wa kifo cha Magufuli, Kanisa Katoliki linapaswa kuona aibu

Kwa hili la mwaka mmoja wa kifo cha Magufuli, Kanisa Katoliki linapaswa kuona aibu

Futa huu uzi wako hapa,Magufuli ni Rais bora wa wakati wote.

Ukiwa kiongozi si lazima watu wote wakupende
Magufuli ni Masihi wa wakati wote jina lake limeandikwa na wino wa dhahabu kwenye mioyo ya watanzania
waliowengi.
 
Wewe Nguruwe,Ben Saanane angekuwa jaamaa Yako ungeandika mavi haya! Pumbavu!
Watu wameumizwa wewe unaleta Uch....
Huyo mjinga mmoja ndio unaniuliza? Sasa sio ndugu yangu na hata angekua ndugu yangu singekua na ubinafsi kuishutumu serikali bila ushahidi.
Kwanza huyo mpuuzi aliendesha kampeni ya kijinga kumtukana na kumkejeli jpm eti degree yake feki. Aliongozwa na chuki tu. Kwa ujinga wake akajiwekea uadui na wale waliyokula kiapo kumlinda rais wa jamhuri.
Halafu ni kurudishie matusi uliyonirushia..nguruwe mwenyewe.
 
Magufuli amevipiga vita vilivyo vyema, vita vya roho na mwendo ameumaliza.

Sasa anangojea kupewa taji ya ushindi. Na siyo yeye peke yake, bali pamoja na wateule wengine walioshinda vita.

Keep RIP our best president, JPM.
Dah [emoji1][emoji1]
 
Mada ya kipagani hii.

Sisi Wakristo hatuishi katikati ya VISASI bali tumebeba UPENDO mioyoni mwetu.
ambie marafiki, jamaa na watu wa ben saa nane, azory gwanda na wengine wengi ambao waliuawa na huyu katili wa ajabu magufuri, mimi ni mkristo lakini nashukuru mungu kwa kumuondoa huyu muuaji na kumutupa kwa shetani, magufuri hakuwa na tofauti na shetani
 
Lakini wakifa mafirauni lazima tushangilie
Firauni gani amekufa nchi nzima ikazizima kwa huzuni na majonzi. Na kesho utashuhudia taifa linavyomkumbuka. Wewe na wenzako ndio mafirauni adui wa matendo mema ya jpm. Huenda ni fisadi wa madawa ya kulevya au unategemea haramu au dhuluma ya aina yoyote kwa umma. Nyie ndio watu pekee mnamuona magufuli alikua mtu mbaya.
 
Viongozi walikuwa wa hovyo ila baada ya kumsifia wakawa wazuri?

Kakobe alikuwa mkwepa kodi na mhaniai haramu ila alipomsifia akaitwa Ikulu...

Nyie wafuasi wa huyu mfu mnavichekesho kweli
Dah, kweli una hasira jamaa [emoji1][emoji1]
 
Unataka Kanisa Katoliki limhukumu mtu ambaye kabla ya kifo chake alipokea Sakramenti zote na linaamini yupo Mbinguni?
Alipokea sakrament lakn kama Kuna mungu kwl huyu jamaa yupo motoni nw kwa matendo yake
 
[emoji23][emoji23] Mzee vipi nimeongea chochote Cha uwongo kuhusu mungu wako hapo?
Endelea kutoa kilio cha maumivu ulichokipata wakati huo na haisaidii chochote hapa. Ni bora ungekuwa unagugumia nyumbani na familia yako. Hapa ni mahali pengine!
 
Ulichoandika ni katekesi ya shetani tangu mwanzo mpaka mwisho umeonyesha dhahili chuki zako kwa JPM ningeshauri tumwache apumzike huko aliko kuliko kumtuhumu mtu ambaye hawezi kujitetea.
 
Unateseka ukiwa wapi?

Mafisadi, mabeberu, vibaraka wa mabeberu, wabadhirifu na vyeti feki mnamchukia sana Magufuli.

You guys should move on.
Huyu jamaa lazima atakuwa mmoja wapo kwenye hayo makundi uliyoyataja
 
Sameheaneni ninyi kwa ninyi,na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi makosa yenu.Usiishi kwa vinyongo.Kwani Wewe mwenyewe binafsi,ukiwa mkweli wa nafsi yako,Ni madhambi mangapi umeyafanya toka uamke Asubuhi kwa kuwaza,kunena n.k.Kwa taarifa yako,dhambi Sio kuuwa TU, kiburi pia Ni dhambi.Kutokusamehe pia Ni dhambi kubwa zaidi.Hata kuacha kutenda mema pia Ni dhambi.Kwa Mungu hakuna dhambi isiyosameheka.Mwenzio Kama alitubia dhambi zake saa zake za mwisho wa uhai wake,Mwenzio Atakuwa yupo mahali Salama mbinguni.Na ukweli ndio hUO haiwezi kubadilika.Wewe endekeza TU kubeba vinyongo vyako,na Hiyo ndio itakuwa ndio boriti lako kubwa.
 
Sijui maana ya kuadhimisha, ila kanisa ufanya misa za kuwaombea wafu, bila kujali waliishije duniani, juwa kanisa uweka madaraja kwa marehemu kipindi cha maziko kuna wanaopata sala tu, ibada na misa takatifu, hivyo kama aliungama kabla basi misa takatifu ni alali kwake, ila jinsi alivyoishi duniani kwenye uongozi wa juu, sijapenda!
 
Sitaki kuzungumzia maovu ya kisiasa aliyoyafanya kwa Taifa huyu mtu, maana hata ukurasa huu hautatosha, nataka nizungumzie tu maovu aliyowafanyia kanisa Katoliki na Makanisa Mengine, halafu leo hii wanaadhimisha mwaka mmoja tangu kifo chake

Kwanza kabisa kulikuwa na mauaji na watu kupotea kulivyoshamiri mwaka 2017 Kanisa Katoliki lilitoa waraka wa kulaani mambo hayo na kuliombea Taifa lirudi kwenye mstari, alichojibu bwana huyu ni kulikejeli Kanisa katoliki na kusema kuwa halikukemea mauaji ya Kibiti (Kitu ambacho ni uongo, Kanisa lilikemea) na hata kama halikukemea kweli ndio itafanya mauaji ya watu wale kuwa sahihi? Ni mtu muovu namna gani anayeweza kuwaza hivi? Kanisa halioni aibu kumuadhimisha mtu kama huyu?

Pili, Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kiprotestanti nao wakatoa waraka wa kukemea mauaji yaliyokuwa yameshamiri nchini kipindi kile, lakini mtu huyu alivyokuwa wa ajabu alitoa wa notisi kwa makanisa hayo kufuta waraka huo ama yatafutiwa usajili, hii ilileta sekeseke hadi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani kipindi kile Mwigulu Nchemba kuondolewa

Tatu, Askofu Kakobe, aliposema kuwa Tanzania ni nchi ya vyama vingi na vyama vyote vinapaswa kupewa nafasi, askofu huyu alitukanwa na kudhihakiwa sana na vijana wa kazi wa huyu mzee, na kunyang’anywa paspoti yake na kuambiwa sio raia wa Tanzania, haikuishia hapo askofu Kakobe alitishiwa kufilisiwa mali zake na za kanisa endapo ‘asingeunga juhudi’ . Huytu ndiye mtu Kanisa Katoliki linamuadhimisha?

Nne, Askofu Niwemugizi aliposema kudai katiba mpya sio uchochezi, mtu huyu bila chembe ya aibu alimuundia zengwe kuwa sio raia wa Tanzania na akapokjonywa paspoti, japo Askofu huyu ndio alikuwa Askofu wake tangu kabla hajawa Rais..!

Tano, Kulipokuwa na Wimbi la ugonjwa Corona, mtu huyu kwa siasa zake za kilaghai akasema Corona imeondolewa kwa maombi ya siku 3, Kanisa Katoliki ambalo linajua kuwa Mungu katupa Sayansi ya kukabiliana na majanga, likasisitiza watu kuchukua tahadhari za kisayansi na kushauri Serikali ifuate njia zilizothibitishwa Kisayansi kukabiliana na hili Janga.

Kanisa lilienda mbali na kutoa takwimu za watumishi wake kama maaskofu, mapadri, masista n.k waliokufa wengi kwa kipindi kifupi kwa dalili za ugonjwa wa Covid. Mtu huyu mnakumbuka alifanyaje?

Alikejeli vibaya viongozi wa Dini na kusema wanapotosha watu kiimani, kuna kipindi aliingia kanisani na kumkejeli padre mmoja aliyekuwa anazingatia kanuni za kujikinga na Corona. Mtu huyu leo ndio Kanisa..Au linataka kumtangaza Mtakatifuu?

Nimechagua baadhi tu ambayo yalifanyika hadharani na mtu fmfuatiliji wa siasa atayajua, ila yapo mengi sana mtu huyu aliwafanyia viongozi wa Dini kama yale ya akina Mwingira, na kukamata mapadri huko Moshi, ila niishie hapa

Najua baadhi wanaweza kuteta na kusema alikuwa kiongozi mkubwa wa nchi aliyefanya mambo makubwa hivyo lazima wamuadhimishe.

Lakini Mkapa, ambaye ni kiongozi aliyekuwa na mapungufu yake pia japo hayakufikia kiwaongo hiki, alifanya mambo makubwa sana na alipofikisha mwaka mmoja tangu kifo chake, Kanisa Katoliki halikufanya chochote
Rubbish, nchi hii ina mapunguani ya kutosha moja wapo ni hili.
 
Walimshauri nakumuandikia nyaraka akiwa mzima.Kanisa silaha yao ilikuwa neno la Mungu,Magu silaha yake ilikuwa nguvu ya dola.
Aliyehukumu nakuhitimisha ni Mungu.Kanisa lisilaumiwe kwa hili,
Muulize Hangaya aliambiwa nini na TEC walipomwomba wakae faragha na wasaidizi wake wa ndani tu.
 
Mbona unajichanganya mwenyewe.
Yeye hii njia ndiyo aliyoichagua, kuchambua maovu yaliyofanywa na huyo mtu. Tatizo liko wapi?

Magufuli alikuwa ni mtu mwovu; shetani aliyekuwa kwenye kiwiliwili cha binaadam.
Ndiyo atulie sasa kila mmoja afanya yake. Kinachomuwasha nini mpaka akosoe wengine?
 
Back
Top Bottom