Kwa hili la Ndugai na Rais, linaonesha watanzania ndio tuna matatizo makubwa

Binadamu na mapungufu yake mkuu ndio maana kuna Kuongoka hata hadithi ya Sauli ipo kwenye biblia inasema vizuri Ndugu JOBO sawa ana matatizo yake na ndio maana nilisema ila nikasema kwa Hili kazungumza Point ndio kuongoka kule
 
Kwahio swala la kukopa Nchi yetu kwa kasi sana na kuweka Tozo unalichukuliaje Mkuu?
Mbona hakufungua mdomo wake wakati wa mwendazake?,au CAG Assad alipotoa ripoti ya upotevu wa 1.5trillion mbona alikuwa wa kwanza kumuwakia CAG, Okay wale wabunge wa covid19 wasio na chama mbona bado ameendelea kuwakumbatia
 
Dikteta ndio Rais wa Kwanza kukopa hovyo? Mbona hatukusikia nyie wasukuma wenzie mkilalama!?

Nikwamba kwanza lilikuwa liongo,linadanganya halikopi kumbe anakopa matrillion ya fedha
Tunajenga kwa era zetu wenyewe [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hizo era zetu wenyewe sasa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hana hoja ya maana. Mikopo imekopwa tangu awamu ya kwanza, leo ndio anasema nchi itapigwa mnada?. Anajielewa kweli?.

Hoja yake kwa undani ni kama aliweka wazi aina ya maongezi wanayoongea yeye na watu wanaompinga rais wakiwa sehemu wamekaa.

Ni kama kinachofanywa na Samia na serikali yake kimewaduwaza, sasa wivu unawasumbua wanaamua kuongea walivyoongea.
 
Ndugai hakuwa anafaa kuwa spika kwa kuanzia. Ni kama kudra imekuwa inambeba muda wote na sasa ukweli wa mambo unajianika wazi.
 
Dikteta ndio Rais wa Kwanza kukopa hovyo? Mbona hatukusikia nyie wasukuma wenzie mkilalama!?

Nikwamba kwanza lilikuwa liongo,linadanganya halikopi kumbe anakopa matrillion ya fedha
Lini hakusema Na katika mradi gani hakusema unajengwa kwa ushirikiano na Nchi flani?
 
alilazimisha tununue sukari kwa jirani zetu,ili hali maghara ya viwanda yamejaza sukari!? Walipohoji kwann, akawaambia nonsense mbele ya jirani yetu!! mala ya pili Sasa inajirudia job kahoji kwann tuwekeze kukopa zaidi ,kaambiwa Kama anataka akajiandae vzr 2025, Sasa sijui haya yote yanakuja kwa sababu gani, swali la msingi watanzania kujiuliza ni hili-ni Nani yuko pamoja na watanzania kwa kumaanisha na ni Nani anatufanyia maigizo!!?.
 
Kwahio mkuu tunaangalia Mvurugano au point ilipo?
Mvurugano mpaka muda huu ni;
SASHA - 5
JOBU - 0
Jobu akiwa na guts za kuliendeleza(though I don't think that's gonna happen) ndiyo patanoga, tatizo hakuna wa vazi la kijani hata mmoja aliyejitoa muhanga kuwa upande wake hivyo ni sawa kusema amepigwa roba ya mbao pumzi inamuishia.
Kuomba msamaha was a tactical mistake.
 
Sasa mbona na Jobu mwenyewe alifanya reference ya 2025, afadhali angejisemea tu ya nchi kupigwa mnada kuliko kuunganisha na uchaguzi wa 2025.
 
Jambo gani la msingi ambalo Ndugai ameliongelea kwenye hotuba yake? Hakuna ubishi kuwa Ndugai alifanya Siasa kwenye hili suala la mkopo.
 
Sasa mbona na Jobu mwenyewe alifanya reference ya 2025, afadhali angejisemea tu ya nchi kupigwa mnada kuliko kuunganisha na uchaguzi wa 2025.
Here is the where the problem started. Lakini swali la pili, ni kweli Job alimaanisha kupitia domestic resource mobilization inawezekana kutekeleza miradi hii? Kama kwa kiwango kilichopitishwa cha tozo kila mmoja analalamika, vipi kiwango kikiongezeka?
 
Ndugai kawa jasiri katonya yanayoendelea jikoni...
Tatizo watonywaji hatujielewi... Mbaya anatabaki kuwa Ndugai!
 
Siku viwanja vya ndege, bandari na Tanesco vinachukuliwa na waliotukopesha ndipo tutakumbuka maneno ya Job Ndugai, wakati huo tumeishachelewa saaaaana!
Aibu yetu watanzania.
Hakuna mtu atumkumbuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…