Kwa hili la Ndugai na Rais, linaonesha watanzania ndio tuna matatizo makubwa

Kwa hili la Ndugai na Rais, linaonesha watanzania ndio tuna matatizo makubwa

Kauli za Ndugai hazivumiliki....kusema nchi itakuja kupigwa mnada hapa anamaanisha huyu anaeongoza nchi ni hovyo...

Kauli ya kusema 2025 mtachagua wenyewe kuendelea na hawa wa kukopa kopa ama la...bado ni ya Kumsimanga Rais kwamba hafai kuongoza nchi inafaa abadilishiwe..

Ndio maana jana Mama Samia kasema kuna watu walitilia shaka uwezo wake wakati anaapishwa kuongoza, Sasa wanaona aibu kwa mambo makubwa anayoyafanya...
Hivi Ndugai angeweza kuhoji kama ingekuwa mkopo huo umekopwa na serikali ya Magufuli?
 
Ndugai kawa jaairi katonya yanayoendelea jikoni...
Tatizo watonywaji hatujielewi... Mbaya anatabaki kuwa Ndugai!
Huenda rekodi yake ya nyuma imemfanya kutoaminika tena hata kama anachoongea kina umuhimu.
 
Hii vita inayoendelea inaonyesha Jinsi gani watanzania ndio tuna shida kubwa na ndio sababu hatuendelei.
Tatizo siyo watanzania bali ni chama tawala..
Ile dhana ya Bunge kuisimamia serikali imegeuzwa kinyemela na chama tawala, sasa imekuwa ni jukumu la spika na Bunge lake kuunga mkono serikali kwa kila kitu hata kikiwa cha hovyo!
Kwamba hata spika hana uhuru wa kukosoa serikali/rais. Kwa muktadha huu, hakuna umuhimu wa kuwa na bunge!
 
Habarini!

Hii vita inayoendelea inaonyesha Jinsi gani watanzania ndio tuna shida kubwa na ndio sababu hatuendelei.

Ndugai kasemea Juu ya jambo ambalo lina maslahi kwa Nchi lakini anakuja Mtu ana mjibu kwa kuangalia Maslahi yake tena kwa kejeli watu Wooooteee wanashangilia Kweli Mpo serious?

Yeah ni kweli kuna sehemu nyingi Ndugai kateleza sana huko Nyuma ila Kuna msemo unasema "Mnyonge Mnyongeni Ila Haki yake Mpeni" Ndugai ana haki ya kujibiwa Sio kwa Njia ya personal attack ila kwa njia ileile aliyotumia kuelezea Issue yake.

Hili suala la Ndugai tuweke Makosa yake pembeni tumhoji Rais sio tufurahi kifo cha Ndugai.

NOTE:
Swala la Msamaha alioomba Ndugai to Me usiulete hapa, ule alileta Njaaa zake tu na hizo ndio errors zake Kila siku tujadili Issue.
nakwakutambua akili za wana ccm zinawaza madaraka ya teuzi,ikatangazwa nafasi za uwaziri, angalia matamko kwenye mitandao yakumponda nakumtaka ajiuzuru, ukiangalia sababu et kwakuwa amehoji kuzidi kukopa wakati tuna tozo na kodi inalipwa vizuri tu! Nahapa tupaze sauti kumuunga nape nauye kwenye hoja yake ya CAG kufanya uchunguzi ya mikopo yote na matumizi yake ili tujue mikopo yote za awamu ya tano na sasa inaendana na miladi iliyopo?
 
Hoja ya kutokuwa na Imani na raisi ipelekwe haraka bungeni , Raisi wa mipasho hatufai
We inaonekana haujui mchakato wa hoja ya kutokuwa na imani na Rais bungeni.

Kasome katiba ibara ya 46A uone mchakato wake halafu uje udanganye watu hapa.

Katika kuwasiliana hoja yake Spika alikosea Sana tena Sana kwa ukubwa wa nafasi yake.

Hoja yake nzuri hiyo alikuwa na uwezo usio na shaka ama kwenda moja kwa moja kushauriana na Rais au kuiweka vizuri hoja yake ili ijadiliwe huko bungeni.

Ukumbuke kwa tukio kama alilofanya Ndugai hilo hilo na mazingira hayo alimhukumu J Slaa, na Gwajima, scholia mbali upinzani ambao kwao ni wahanga wakubwa. Tusijisahaulishe hapa.

Mwisho Ndugai lazima ajiuzulu na yeye kufukuzwa uspika ni kazi rahisi Sana endapo atakaidi maana ni kufutwa uanachama tu mengine yatakuwa yamekoma.
 
Back
Top Bottom