Kwa Hiyo Serikali /DCI na Mahakama, mmeamua kuwaambia Watanzania kuwa Dada wa Msuya alijichinja mwenyewe?

Mume wa huyu mama kipindi cha uhai wake alishakuwa na mashaka ya kufanyiwa matukio ya uhalifu yaliyotishia usalama wake. Hadi mauti yanamkuta inakonekana wazi kuwa kuna mtu wa karibu ambaye anahusika na suspect wa kwanza alikuwa ni mkewe kwenye mazingira ya mauwaji.

Inasadikika kuwa huyu mama aliyeachiwa huru alishirikiana na majambazi wa kukodi kumuua mume wake na kufanya tukio lionekane ni la uporaji kumbe ni assassination ili mume afe yeye mke arithi mali ambazo kwa wakati huo umiliki ulikuwa chini ya mume wake ila ndugu na jamaa zake mke walikuwa wameshaingia sana kwenye makampuni ya huyo billionaire na kuleta hofu kwa ndugu na jamaa upande wa mwanaume.

Baada ya kifo cha mwanaume Mdogo wa kike wa marehemu hakukubaliana kabisa na swala la kuwa tukio la kuuwawa kwa kaka yake ni ajali ya ujambazi bali lilikuwa no tukio maalumu la kumtoa uhai kaka yake na kumuua kwa makusudi.

Alishikia bango na ndipo hapo kwa mujibu wa historia ya matukio alifuatwa nyumbani kwake na kufanyiwa mauwaji ya kikatili nyumbani kwake jambo ambalo likaongeza suspiciousness juu ya mke wa marehemu kuwa ndio orchestrator wa haya mauwaji yote ya kaka na mdogo wake.

Kesi ndio hiyo ilikuwa ikiughuruma kati ya huyo mwanamke na familia ya marehemu hawa wawili na mke wa marehemu wakimtuhumu kuuwa ndugu zao ili kujitwalia mali za marehemu pekee yake bila kushare chochote upande wa mume wake.


Kwahiyo ndio tamati ya kesi imekuwa kama ulivyoona kuwa familia ya marehemu hawa wawili imeshindwa kesi na mke wa marehemu ameshinda baada ya kusota na hizi kesi tokea mwaka 2017.

Kwa kifupi pesa na mali zipo kwa watoto na mama yao.
 
Mimi jana haikuwa siku nzuri kwangi. Ndiyo masna kumbe wanasema haki ipo mbinguni! Anyway
 
Hati ya kiwanja inaua ... ardhi inameza....
Ama wifi alikuwa na taarifa muhimu za familia kiasi kwamba alionekana tishio kwa wifiyeee?

Kwa kuwa sifahamu jambo ngoja niendelee baki humu JF
 
Makonda alishawaambia kwamba kama huna pesa na huna mizizi na Wanasiasa usijisumbue kwenda mahakamani.

Mahakama ni sehemu ya kuwapa Haki wenye pesa na Wanasiasa ila ni chombo Cha kukandamiza maskini.

Ni Bora maskini kuwekeza hata kwenye uchawi mkamalizana Nje japo wenye pesa wanakuaga na vyote kuanzia wachawi Hadi watu wa kanisani,labda Mungu ataamua japo hatujui.
 
Huo ukoo ushaingia dosari kubwaa, kisasi kitaenda karne na karne

Huyo mtoto wa Aneth atakua! mziki utaanza tena hivi ni wakiume😂
Sio wote wanaweza fanya hivyo,Mimi Babu yangu aliporwa Mali akasingisiwa kesi za uhujumu uchumi na kufungwa jela baadae akajiua lakini Watoto wake walikuwa wadogo ambao ni Baba zangu hawajafanya chochote zaidi ya kujitenga na familia ya wale baba zao wakubwa waliofanya hayo.
 
Sasa kama Mahakama inahitaji mambo ya lobbying na ujanja ujanja wewe unaona ni chombo cha Haki?

Naungana na Makonda hakuna haja ya maskini kwenda mahakamani ni umuachie Mungu ahukumu maumivu Yako au uwe mchawi nguli uroge Kwa kisasi Ili nafasi ipumue.

Hii mambo inauma kana kwamba ni ndugu yangu kafanyiwa wakati hata siwajui.
 
Kama kuna uwezekano Kitengo cha CID kiwe taasisi kamili inayojitegemea na CID lazima wawe polisi wenye shahada ya Sheria na wawe wamepitia Tanganyika Law School.
 
"Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu...." (Kurani 4:58)

Vilevile anasema:

"...Na hukumu ni kwa uadilifu. Hakika, Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki." (Kurani 49:9)

Tunafaa hata kuwa waadilifu kwa wale tunaowachukia, kama vile Mungu anavyosema:

"...Wala kuchukia wengine kusiwafanye kuacha uadilifu. Kuweni Waadilifu; hivyo ndivyo kuwa karibu mno na uchaMungu...." (Kurani 5:8)

Mtume Muhammad alisema: "Enyi watu, jihadharini na dhuluma,[5] kwani udhalimu utakuwa giza siku ya Kiyama."[6]

Na wale ambao hawajapata haki zao (yaani, kwa kudai haki zao) katika maisha ya sasa duniani watazipata Siku ya Kiyama, kama vile Mtume alivyosema: "Siku hiyo ya Kiyama, haki zote zitapewa kwa wale wanaostahiki (na maovu yatalipizwa)..."[7]
 
Dah
 
Ni wazi kesi ya Bilionea Msuya hujaifuatilia kabisa na unaleta stori za vijiweni. Jamaa aliuawawa kutokana masuala yake ya biashara hizo hizo za madini baada ya kuhitilafiana na wenzake.

Kwenye suala la huyu mama ni mazingira ndio yanamtia hatiani. Inawezekana marehemu Aneth pia alikuwa ana issues personal na watu wengine its just hili la huyu mama ndio likapewa uzito.

Mahakama imeamua kutokana na ushahidi uliowasilishwa mbele yake. Ukifuatilia hii kesi utaona kabisa kwa namna mambo ya mirathi yalivyo kibongo bongo hao ndugu zake na Bilionea hakuna namna mirathi wangepata wao unless watumie mbinu za ziada.
 
Kuna mambo mengi sana kwenye kesi uweledi kwenye upelelezi na rushwa vinachangia sana kuharibu kesi nyingi africa
 
Unataka wakakate rufaa kwao[emoji16][emoji16][emoji16]?
 
Hii kosa ilikosewa makusudi kuanzia kuandaa kesi hadi kuandaa mashahidi makosa ya ki ufundi ni mengi ...inawezekana tunamlaum kibatala lkn yeye kacheza na loophole za kesi ..
 
Mahakama sio sehemu ya maskini kupata Haki haijawahi tokea
Dah hizi kesi mbili zinaonesha ushahidi huo kuwa mahakamani haki kwa masikini hakuna..

Ila hii wakulaumiwa polisi na upelelezi wao kwa kushindwa kuthibitisha uhusika wa mtuhumiwa.. wameshindwa ktk ku file kesi...nilishtuka kuona muuaji ana kesi moja tu ya kuua..jamhuri ithibitishe hadi hapo ilikua tayari mazingira ya ushindi yamewekwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…