Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Mume wa huyu mama kipindi cha uhai wake alishakuwa na mashaka ya kufanyiwa matukio ya uhalifu yaliyotishia usalama wake. Hadi mauti yanamkuta inakonekana wazi kuwa kuna mtu wa karibu ambaye anahusika na suspect wa kwanza alikuwa ni mkewe kwenye mazingira ya mauwaji.Hivi sababu hasa ya Mke wa Msuya kuhusishwa na kifo cha Wifi yake ni ipi ? na kwamba kama angemuua wifi angepata nini zaidi ya mali ambazo alikuwa nazo za bilionea Msuya?
Na kwamba uwepo hai wa huyu wifi ungezuia kitu gani kwa mke wa Msuya kupoteza mali za mumewe na huku ni mke halali?
Hapa nahitaji kueleweshwa .
Inasadikika kuwa huyu mama aliyeachiwa huru alishirikiana na majambazi wa kukodi kumuua mume wake na kufanya tukio lionekane ni la uporaji kumbe ni assassination ili mume afe yeye mke arithi mali ambazo kwa wakati huo umiliki ulikuwa chini ya mume wake ila ndugu na jamaa zake mke walikuwa wameshaingia sana kwenye makampuni ya huyo billionaire na kuleta hofu kwa ndugu na jamaa upande wa mwanaume.
Baada ya kifo cha mwanaume Mdogo wa kike wa marehemu hakukubaliana kabisa na swala la kuwa tukio la kuuwawa kwa kaka yake ni ajali ya ujambazi bali lilikuwa no tukio maalumu la kumtoa uhai kaka yake na kumuua kwa makusudi.
Alishikia bango na ndipo hapo kwa mujibu wa historia ya matukio alifuatwa nyumbani kwake na kufanyiwa mauwaji ya kikatili nyumbani kwake jambo ambalo likaongeza suspiciousness juu ya mke wa marehemu kuwa ndio orchestrator wa haya mauwaji yote ya kaka na mdogo wake.
Kesi ndio hiyo ilikuwa ikiughuruma kati ya huyo mwanamke na familia ya marehemu hawa wawili na mke wa marehemu wakimtuhumu kuuwa ndugu zao ili kujitwalia mali za marehemu pekee yake bila kushare chochote upande wa mume wake.
Kwahiyo ndio tamati ya kesi imekuwa kama ulivyoona kuwa familia ya marehemu hawa wawili imeshindwa kesi na mke wa marehemu ameshinda baada ya kusota na hizi kesi tokea mwaka 2017.
Kwa kifupi pesa na mali zipo kwa watoto na mama yao.