Kwa Hiyo Yanga Mmeingia mkataba wa milioni 16.6 kwa mwezi na GSM?

Mo foundation inaweka shillingi ngapi kwa mwaka???

Mwanamme kuwa mnafiki hivi haipendezii
 
Huo uwanja wa bunju mpka sasa umejengwa kwa sh ngapi maana hela zenu za mchango nazo zilimezwa huko na bado hata ukuta hauja kamilika
 
Hapo sasa.
 
Ulitaka wapate ngapi ndio uridhike?
 
Ukweli usemwe huo mkataba ni wa unyonyaji
Miaka yote hiyo nafasi ilikuwa wazi, hamkuona fursa hiyo nyie makampuni makubwa, make uwezo wa makampuni yenu mngekuwa mnatupa hata milioni mia kwa mwezi, sasa nafasi imejazwa kelele zimeanza so uongozi unaona ni heri hiyo kidogo kuliko kukosa kabisa.
 
Bora huu wa Simba
 
Mo foundation inaweka shillingi ngapi kwa mwaka???

Mwanamme kuwa mnafiki hivi haipendezii
Usiwe mbishi, hakuna mkataba wa Simba wenye hela ndogo kama hiyo. Mo Energy tu mwaka 2018 ulikuwa sh. 250M kwa mwaka, huu mwaka 2024 mtu anakuja kukupa 200M kweli, halafu anakupa mkataba mrefu wa miaka mitano bila kujali thamani ya fedha ya wakati huo? Heri basi angeweka mwaka mmoja mmoja kama Mo Energy ya Simba ili walau kila mwaka kuwepo mazungumzo ya kuupandisha thamani
 
Safi sana
 
Hicho ndicho nawapendea Yanga, Acha wakusanye pesa. Hiyo kampuni ndiyo uwezo wake. Hauwezi kuwa na udhamini mkubwa tu. Hata timu kubwa Zina udhamini mdogo pia.
 
Na hapo bado TRA hawajachukua chao.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Wewe Huwaga unatoka ngapi hata kwenye misiba tuu au timu unayoshabikia?
 
Haitoshi hata kulipa mshahara wa Chama kwa mwezi,huo ni unyonyaji
 
529,000 na kidogo kwa siku wewe unadhani haitoshi? Swali fikirishi wewe unaweza changia ngapi kwa siku, GSM is a group of companies and one of them is ready to contribute that much every day
 
Mpinzani wa gsm katika huo udhamini aliweka propasal ya kiasi gani?
 
Umesoma nilichokuuliza??
 
Mlete mtu ambae walau atatoa mil20 kwa mwezi tuone
 
Thamani ya mkataba wa tangazo kwenye jezi inategemea pia nembo ya bidhaa imewekwa wapi! Mo Extra ipo mbele, tena kifuani inaonekana wazi wazi! Hata ukisema u-Google jezi za Simba, Mo Energy utaiona lakini tangazo la Utopolo lipo mgongoni tena juu kabisa karibu na shingo.; na hata uki-Google ni ngumu kuona kwa sababu mara nyingi hizi jezi mitandaoni zinaoneshwa mbele! Hata ukiingia kwenye pages zao za klabu, tangazo la Mo Extra utaliona kila palipo na jezi ya Mnyama lakini itabidi upekue sana kuona tangazo la energy ya GSM kwenye jezi za Uto hata kwenye pages za klabu! So, ukitoa factors zingine, matangazo kama hayo kwa kuangalia positions zao hayawezi kuwa na gharama sawa! Tena Mo alitakiwa kulipa zaidi ya hiyo kutokana na position ya Mo Extra Logo.
 
Labda wamemaanisha bilioni 1 kwa mwaka kwa miaka mitano.

Yaan 5 bilions in totoal
Tunaleta ushabiki tu lakini 1B haiwezi kuwa viable kwa GSM kwa sababu pamoja na mambo mengine, logo yenyewe ipo nyuma ya jezi tena juu kabisa karibu na shingoni. Hii ni tofauti na Mo Extra tunayoisema ambayo ipo mbele tena kwenye best position. Mbali na hayo, kinywaji chenyewe bado kipya, ndo kwanza kinaingia sokoni na unaweza kukuta bei yake ni 500! Sasa ukitoa costs zote (before Utopolo) za kuzalisha na kuuza chupa ya sh 500; assume wanabaki na Sh 300. Sasa kutoka hapo kwenye 300 halafu ulipe 1B nyingine huku soko likiwa limefuruka energy drinks; sio kazi ndogo! Mbaya zaidi, GSM hajajikuta kwenye fast moving consumer products kwahiyo hata distribution channel yake labda inaweza kuwa robo tu ya watu kama Azam wanaouza hadi maandazi na chapati hadi uswahilini!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…