Kwa Hiyo Yanga Mmeingia mkataba wa milioni 16.6 kwa mwezi na GSM?

Kwa Hiyo Yanga Mmeingia mkataba wa milioni 16.6 kwa mwezi na GSM?

Thamani ya mkataba wa tangazo kwenye jezi inategemea pia nembo ya bidhaa imewekwa wapi! Mo Extra ipo mbele, tena kifuani inaonekana wazi wazi! Hata ukisema u-Google jezi za Simba, Mo Energy utaiona lakini tangazo la Utopolo lipo mgongoni tena juu kabisa karibu na shingo.; na hata uki-Google ni ngumu kuona kwa sababu mara nyingi hizi jezi mitandaoni zinaoneshwa mbele! Hata ukiingia kwenye pages zao za klabu, tangazo la Mo Extra utaliona kila palipo na jezi ya Mnyama lakini itabidi upekue sana kuona tangazo la energy ya GSM kwenye jezi za Uto hata kwenye pages za klabu! So, ukitoa factors zingine, matangazo kama hayo kwa kuangalia positions zao hayawezi kuwa na gharama sawa! Tena Mo alitakiwa kulipa zaidi ya hiyo kutokana na position ya Mo Extra Logo.
Hapa umeoandika kama msomi na mtu wa marketing haswaa siyo hawa wengine wanaandika tu kwasababu simu ina bunddle au wapo kwenye WI-F maofisini huko
 
Huo si mshahara wa CEO Wa geita gold kwa mwezi.
 
Tunaleta ushabiki tu lakini 1B haiwezi kuwa viable kwa GSM kwa sababu pamoja na mambo mengine, logo yenyewe ipo nyuma ya jezi tena juu kabisa karibu na shingoni. Hii ni tofauti na Mo Extra tunayoisema ambayo ipo mbele tena kwenye best position. Mbali na hayo, kinywaji chenyewe bado kipya, ndo kwanza kinaingia sokoni na unaweza kukuta bei yake ni 500! Sasa ukitoa costs zote (before Utopolo) za kuzalisha na kuuza chupa ya sh 500; assume wanabaki na Sh 300. Sasa kutoka hapo kwenye 300 halafu ulipe 1B nyingine huku soko likiwa limefuruka energy drinks; sio kazi ndogo! Mbaya zaidi, GSM hajajikuta kwenye fast moving consumer products kwahiyo hata distribution channel yake labda inaweza kuwa robo tu ya watu kama Azam wanaouza hadi maandazi na chapati hadi uswahilini!!
Azam mbishi sana

Jamaa anauza hadi barafu, tuliokula barafu kpnd tunasoma tukiona hizi icecreams zake mabarabarani tubakumbuka mbali sana
 
Back
Top Bottom