Uchaguzi 2020 Kwa hizi sababu Lissu anaweza kukosa sifa za kupeperusha bendera ya CHADEMA kwenye kumpa changamoto Mgombea wa CCM

Uchaguzi 2020 Kwa hizi sababu Lissu anaweza kukosa sifa za kupeperusha bendera ya CHADEMA kwenye kumpa changamoto Mgombea wa CCM

CHADEMA kama mnataka msidumbukie shimo kaeni mbali na lissu mtakiua chama akigombea Urais

Kwasababu Lissu amekuwa ni mtu wa jazba asiyedhibiti emotional za ndani.

Ana chuki na vyama vingine vya kisiasa na kuvidharau mfano huita CCM"maccm" yaani yeye watu wa muhimu kwake ni Chadema tu wengine ni takataka huyu moja kwa moja anakosa sifa za kuwa kiongozi

Alimdhalilisha Baba wa Taifa bungeni kwa kutoa maneno ya kejeli na kudhihaki hii haijawahi kutokea kwa kiongozi yeyote toka Nchi yetu ipate uhuru

Wakati akiwa mbunge alkuwa akiwakataza Wananchi wasichangie michango ya maendeleo jimboni kwake hali iliyopelekea shughuli za maendeleo kusimama

Wakati Rais Magufuli anatetea Watanzania juu ya madini yetu yaliyokuwa yakiporwa na Mabeberu tunajua Lissu alikuwa anawatetea watu gani

Kazi kwenu Chadema muamue msimamishe lissu mfe kabisa au muangalie watu wanaoweza kukibeba chama

Kwa maoni yangu watu kama Peter Msigwa, Lema, Nyalandu au Membe wanaweza kuonesha upinzani kwa mgombea wa CCM Rais Magufuli la sivyo mkimsimamisha Lissu hata diwani hamtapata.
MACCM ndo walio nachuki naye kwa kuandaa mkakati wa kumpoteza ila Mungu hakupenda afe kwa zamu ile
 
Pesa Lisu Hana za kampeni na chadema haina hela. Akiulizwa una shilingi ngapi za kampeni mfukoni Hana hata Mia

Na safari hii Hakuna tajiri atakuwa tayari kumgharimia kampeni Baada ya kuwatoa Lowasa na Sumaye wenye connection na matajiri

Kiujumla chadema uchaguzi huu kina Hali mbaya pesa hakina na Lisu lofa
JIWE fedha za kampeni atapata wapi? CCM fedha za kampeni itazipata wapi?
 
Na huu umri wangu sijawahi kuona Mzalendo anayewatetea Mabeberu km Lissu
Mtu mzima bila aibu mishipa imemchomoka anawatetea Mabeberu yatuibie raslimali zetu!

Mna raslimali gani za kuibiwa? Ni mzungu gani anamsubiri Lissu ili aibe raslimali za nchi hii? Kwani ni kipi mpaka sasa hivi wamekosa kwenye hizo raslimali, hadi wasubiri Lisu awatetee? Bado mnaishi kwenye hizo propaganda za kizee?
 
Na aliyakiri hadharani mapungufu yake. Aliandika na vitabu viwili vya kukusoa, Tujisahihishe na Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania. Vitabu hivi vyote vililenga kujikosoa na kurekebisha
Halafu wanatokea wajingu kama hawa wanamuona kama alikuwa Mungu mtu
 
JIWE fedha za kampeni atapata wapi? CCM fedha za kampeni itazipata wapi?
Tuna bilioni 80 za miradi ,ruzuku nk hatujazifisadi zime park zinasubiri filimbi tu ya uchaguzi . Chadema mumezila zote hamjabakiza kitu akaunti nyeupeee mtakoma
 
Amka ndotoni Mkuu
Jana vyombo vya duniani vimemuingiza Rais Magufuli katika orodha ya Ma Rais kumi bora duniani wanaojenga uchumi na maendeleo kwenye Nchi zao

Membe anawafaa Chadema kwakuwa wanakumbatia mafisadi
Hapana Mkuu, hapa naongea kama mwana CCM kindaki ndaki. Membe atatufaa sana kwa awamu ijayo, Magufuli ameishiwa pumzi. Uchumi umekorogeka, deni la Taifa linazidi kuongezeka, ufisadi wa zile Trilion 2.5, matumizi mabaya ya madaraka na kujilipa bilioni 1.2 za chee kila mwezi n.k. Huoni kama likiruhusiwa JUKWAA HURU, CCM hatutakuwa na hoja yeyote? Magufuli sasa basi, Twende na Membe.
 
Sijaambiwa na mtu nimesoma tathimini za awali na za sasa za ndani zilizofanyika

Ni wazi Chadema haina jimbo hata moja
Magufuli ndio kakuambia kuwa ameiagiza tume ya uchaguzi kufanya hivyo?
 
Mbunge wa Chadema alisema lissu kupigwa risasi ilikuwa mpango wa chama Kwasababu alitaka kujijenga yeye

Ndio Chadema walimtorosha dereva wa lissu asihojiwe kuna mengi yamejificha
Mlivyo taka kumtoa roho hamkujua kuwa ni mropokaji?
 
Huo ni uwongo dhahiri shairi, Rais Magufuli ni mwanademokrasia
Angekuwa anakubalika asingekuwa anaagiza mabox ya kura yatolewe vituoni kwenda kujazwa kura za ccm. Tusingekiwa tunaona ukatili na uhayawani wa wazi kwenye chaguzi ili ccm watangazwe washindi.
 
Sasa mnashindwa nini kumkamata huyo mbunge ili awaeleze ukweli?
Mbunge wa Chadema alisema lissu kupigwa risasi ilikuwa mpango wa chama Kwasababu alitaka kujijenga yeye

Ndio Chadema walimtorosha dereva wa lissu asihojiwe kuna mengi yamejificha
 
Tunamsubiria tuje tumpige kwenye boks la kura

Saa tatu asubuhi tu iyena iyena inaanza mtaani
Mnaweweseka na hapo ndiyo bado asubuhi, bado dume la mbegu halija tia team
 
Back
Top Bottom