Kwa hoja za Babu Tale bungeni, ninakiri kuna ulazima wa marekebisho ya Katiba kwa sifa za mtu kuwa Mbunge

Hicho chama chako unachokipenda ndicho kinatuharibia inchi yetu kwa sasa. Wameshafeli
 
Nani atabadili katiba? Na ilikuwaje kilaza aingie bungeni 2020?
 
Bahati nzuri hakuchaguliwa na mtu yoyote alipelekwa kwa nguvu na marehemu, hatuna bunge mbali ni kusanyiko la wahuni tupu
 
Kumbuka huyu alishinda Ubunge bila kupingwa Mkuu..[emoji3][emoji3]
 
Bila kupata utaratibu wenye vigezo vinavyo eleweka ikiwemo elimu vya kupata viongozi wa Kisiasa tutarajie kuja kupata kiongozi Mkuu wa Nchi ambaye ni wa ajabu na hovyo hovyo mno. Kwa nini uongozi wa kisiasa ndio uwekewe vigezo duni vya kielimu kumpata mhusika, Kwani siasa sio ajira? Ajira yenye hadhi na mapurupuru ya Kibunge eti imewekewa kigezo cha kielimu cha kujua kusoma na kuandika huu ni mzaha wa kiwango cha juu. Tanzania kama taifa wakati nwengine tuna mizaha sana kwenye mambo ya'msingi yanayo gusa maisha watu.

Sifa ya kiongozi muhimu na muwakilishi kwenye chombo nyeti cha uwakilishi wa wananchi bunge kwa ajili ya kutungua/kupitisha sheria na kuisimamia serikali kigezo cha kielimu iwe ni kujua kusoma na kuandika. We are not serious.
 
Kumbuka huyu alishinda Ubunge bila kupingwa Mkuu..[emoji3][emoji3]
Wakati ule 2020 nilikutana na jamaa flani ambaye sio mtanzania akaniambia kwa kilichofanyika kama ingekuwa kwao basi yangetokea machafuko mabaya sana. Mwendazake aliubaka uchaguzi.
 
Ndio maana sisi tunapigania Katiba Mpya
 
Yule ibilisi ametuachia kusanyiko la mazuzu badala ya Bunge
 
Wa kulaumiwa ni huyo mnaemuita raisi wa wanyonge....chuki zake zilisababisha ajaze watu wa hovyo bungeni....mfano yule mama aliezungumza ishu za kunyonya maziwa wanawake....
Hivi hakuna namna ya kuwawajibisha kina Bashiru na Polepole pamoja na familia zao? Wameacha kovu permanent kwenye hii nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…