Nilimuona hata mimi wakati anachangia mawazo yake wakati Waziri mwenye dhamana ya Michezo na burudani/utamaduni alipokuwa akiwasilisha bajeti yake!
Kiufupi Babu Tale anaumudu Umeneja tu wa timu yake ya Wasafi na Tiptop Connection! Ila siyo Ubunge. Maana muda wote aliutumia kuwasema BASATA na COSOTA kwa sababu tu wamekuwa na utaratibu wa kufungia Wasanii wasio jitambua, na pia nyimbo zilizo kinyume na maadili ya Mtanzania!
Ifikie wakati 2025, watu wasio na sifa ya kuwa Wabunge, wafanye tu shughuli zao za kila siku za kuwaingizia kipato! Na hivyo Bunge jipya liundwe na watu smart kichwani!