Kwa hukumu hizi; Je, Mahakama za Tanzania zinatumia Sheria tofauti ?

Kwa hukumu hizi; Je, Mahakama za Tanzania zinatumia Sheria tofauti ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hebu angalia hukumu hizi mbili halafu toa maoni yako

Mwezi_May_mwaka_huu_huko_Mbozi,_Mahakama_ilimpata_na_hatia_Dr.Semeni_Mswima_kwa_kuisababishia_...jpg
 
Inawezekana ushahidi haukuwa mkali sana kwa bwana mfukua mitaro kama ulivyokuwa kwa bwana mganga
 
Tunahitaji Katiba Mpya ije kuwaweka huru mahakimu na majaji toka kwenye kifungo cha CCM.

Kama mahakimu hawana elimu, waondolewe kwenye nafasi zao bila kuangaliana usoni, muda wa kulindana umekwisha.
 
Mkuu

Mahakama hizi hazina kawaida kufanya rejea kesi za aina hiyo zilizokwisha hukumiwa nchini Tanzania zaidi kurejea kutoka nchi zingine ndio maana unaweza kukuta kesi kama hiyo ina hukumu tofauti!!!!
Hamna kitu kama hicho ulichoandika hapa, rejea zipo kila mahali kwenye vitabu vya sheria, na mara nyingi rejea hizo hutumiwa kuwahukumu wasio na kitu, lakini sio kwa huyo kigogo mwenye marafiki zake CCM, lazima wamlinde mwenzao.

Hata common sense inakataa, mtu apoteze bilioni 100 halafu alipe faini milioni 8!, upuuzi kabisa.
 
Unapinga, baadae unajipinga kisha unaniunga mkono utaelewekaje?
 
Unapinga, baadae unajipinga kisha unaniunga mkono utaelewekaje?
Sijui hujaelewa nini, mahakama hufanya rejea ya kesi kabla ya kutoa hukumu, unaposema hazina kawaida ya kufanya rejea unapotosha, kinachosababisha tofauti kwenye hizo hukumu ni mahakimu/majaji kuangalia sura za watu kabla ya kutoa hukumu.
 
Rejea nyingi zinazofanywa huwa ni za kutoka nchi za nje ambazo zimo ndani ya jumuia ya madola (Kenya, Uganda, South Africa, Uingereza nk)

Ni mara chache rejea ya hukumu za kitanzania na hata hivyo kwenye mantiki hukinzana
 
Hakimu ana mamlaka ya kuhukumu atakavyo, kwa mujibu wa Sheria zetu.
Sasa usiombe siku ya hukumu yako umkute hakimu kalanduka
Siku ya hukumu ukisikia hakimu au jaji anaanza kusifu namna mshitakiwa alivyoweza kujitetea na kujibu hoja za upande wa mashitaka ujue wewe ndio unaenda kuhumiwa kifungo au faini. Lakini ukisikia akianza kusoma maelezo yanayoonesha utetezi wako ulikuwa dhaifu ujue unaenda kuachiliwa huru kwakuwa baada ya maelezo yale atasema 'LAKINI.......'
 
Hukumu tofauti hizo
1. Mganga ameiba, na anatakiwa kurejesha
2. Boss ATCL amesababisha hasara (haijatamkwa kwamba ameiba, yawezekana ni usimamizi mbovu)

1629475138327.png
 
Back
Top Bottom