Kwa hukumu hizi; Je, Mahakama za Tanzania zinatumia Sheria tofauti ?

Kwa hukumu hizi; Je, Mahakama za Tanzania zinatumia Sheria tofauti ?

Ukipata nafasi ya kuiba hela ya serikali usiache iba yote,case study na kwa uzoefu utafungwa mda mchache.
 
Siku zote huwa nasema afrika jela huwa ni kwa ajili ya watu masikini.
Ukiwa na pesa hukumu huwa tofauti
 
Ipi ina madhara makubwa kwa nchi? Milioni 30 iliyoibwa au bilioni 100 iliyopotea?
Linaangaliwa kosa, sio kiwango. Ukitumia nguvu kujaribu kuiba au kufanya uovu (ukivunja nyumba, ukiteka, ukitumia silaha), hata kama hukufanikiwa kuiba hela au mali yoyote, adhabu yake ni miaka 30 jela au faini au vyote viwili
 
Hamna kitu kama hicho ulichoandika hapa, rejea zipo kila mahali kwenye vitabu vya sheria, na mara nyingi rejea hizo hutumiwa kuwahukumu wasio na kitu, lakini sio kwa huyo kigogo mwenye marafiki zake CCM, lazima wamlinde mwenzao.

Hata common sense inakataa, mtu apoteze bilioni 100 halafu alipe faini milioni 8!, upuuzi kabisa.
Labda Mataka alikuwa mpendwa "Afsa kipenyo"
 
Unasema hivyo kwa kuwa haujui sheria na adhabu za ukiukwaji wa sheria hizo
Nazungumzia upendeleo kwenye kesi,au upindishwaji wa hukumu.
Wote ni wezi kwann kibaka anapigwa mvua nyingi na fisadi anapewa hukumu ya kupiga deki wodi.
 
Hukumu ya kibaka na ya fisadi haziwezi lingana japo wote ni wezi
 
Linaangaliwa kosa, sio kiwango. Ukitumia nguvu kujaribu kuiba au kufanya uovu (ukivunja nyumba, ukiteka, ukitumia silaha), hata kama hukufanikiwa kuiba hela au mali yoyote, adhabu yake ni miaka 30 jela au faini au vyote viwili
Asante kwa elimu ILA hapo sasa ndo udikteta unapotakiwa kwa asilimia zote. Mimi sioni tofauti kati ya aliyetumia nguvu kuiba na huyu aliyeiba kilaini kwa kiwango cha nguvu.

Anayetumia nguvu kuiba, anaweza kuua kwenye harakati hizo. Yule aliyeiba kwa kiwango cha nguvu, anasababisha mamia kwa maelfu kufa kwa kukosa panadol, maji safi na salama, wazee kukosa pension zao n.k WOTE WANAUA TU.
 
Mkuu, hizo ni hukumu tayari, ushahidi ulishafungwa [emoji23][emoji23][emoji23]
Au haujasoma hapo, mbona pameandikwa waziwazi kwamba arejeshe sh. 30,850,000/= alizoiba?
Huyu mganga hakuwa na hata nusu ya fedha anayotakiwa kurejesha. Ingetokea angekuwa na hata nusu yake na angekubali waigawanye kifungo kisinge muhusu.
 
Back
Top Bottom