Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Hiyo ni mifumo tu ila mindset zao bado ni primitive.
Hawana ustaarabu na maamuzi yao yanaongozwa na ukabila.
Kwa sasa matokeo bado.
Vurugu huwa zinatokea wakati wa matokeo na sio wakati wa kupiga kura.
Matokeo rasmi bado kutangazwa.
Kwakua wanajielewa kuwa hawana ustaarabu wowote ndio maana wakamuita kikwete kama Muangalizi ili aende kuwasaidia kikinuka kama alivyowapa mawazo kipindi kile wakaelewana.
Wazo la UPM lilitoka kwetu na Odinga akawa PM.
Hivyo bado wanasafari ndefu sana kufikia ustaarabu tulionao sisi na bado wanatuhitaji mno.
Jifinzeni kuipenda nchi yenu na kuthamini mlichonacho.
Maamuzi yao yanaongozwa na ukabila, kwani kuna ubaya gani kama wanajitambua? Hawajamuita JK kwa mantiki ya ubora wake usitake kupotosha, bali wako waangalizi wengi ikiwemo JK na marais wengine wastaafu, huo ni utaratibu wa kawaida kwenye chaguzi za nchi nyingi.
Wazo la uprime minister lilitoka kwetu, kwani Tanzania pekee ndio nchi yenye mfumo wa waziri mkuu? Isitoshe cheo cha waziri mkuu huko kiko ceremonial zaidi na sio kama hapa kwetu.
Sisi sio wastaarabu bali ni makondoo, usichanganye ustaarabu na ukondoo.
Wanatuhitaji kwa sababu za kibiashara, na sio Tanzania tu bali na majirani wao wengine, huku wao wakiwa wafaidika wakubwa wa ushirikiano huo. Tunaipenda nchi yetu lakini sio serikali ya majizi ya kura. Na hiyo haiondoi ukweli kuwa Wakenya they are far better than us.