Mkuu sera nzuri, lkn zinahitaji ufafanuzi wa ziada ni namna gani zitatekelezwa, zipo too general, sera zinatakiwa ziwe specific, otherwise huwezi ukafanikisha chochote zaidi utashika hichi, utaacha hichi utaenda kile, miaka 5 itaisha hujafanya chochote, angalia ACT wazalendo sera zao zipo very specific, wanataja sera na namna ya kuikamilisha, labda sijui ushiriki wa sekta binafsi unaotakiwa na CDM ni wa namna gani wakati tangu enzi za Mzee wa ruksa sekta binafsi walipewa nafsi lkn maendeleo hayakuwepo, au tuje kwa CCM ya viwanda a. k. a CMM ya Magufuli angalia sera zao, Magufuli anaamini bila umeme wa uhakika na miundombinu thabiti huwezi kuwa na viwanda ndio maana kajikita huko. Ni vizuri pia Chadema muwe specific kwenye sera zenu