Uchaguzi 2020 Kwa Ilani hii ya CHADEMA, CCM jiandaeni kuwa wapinzani baada ya kuanzia Oktoba 2020

Sasa jaribuni kuingilia matakwa ya wananchi ndo mtaona kama Kuna hatari ya nguvu ya umma au la!!
Nguvu ya uma isiyodhibitika ni mamlaka na hakuna anayeweza kuizuia na hilo lipo wazi. Tatizo ni kuitegemea kuingia ikulu bila kuwa na hakika kuwa uma upon tayari kuitumia.
 
Huyo jamaa kwenye uchumu imara na shirikishi naona anaioneshea kidole Boeing 787
Uchumi shirikishi na imara utaletwa na Sera hizi za Chadema na Lissu. Sio sera za kukimbiza wawekezaji na kuwafirisi Kama za Magufuli
 
Mkuu chunguza sana wanaosema hivyo wapo kama 10 hivi hapa Jf na id zao kila siku zinajulikana
Eti hawafiki hata 10! kwa taarifa yako huku ni watu huru wanaotoa mawazo yao huru. Hatuna haja ya kuwa kama nyie Lumumba na wakabila Kina Gwajima wanaohamaishana kufanya kampeni za kibaguzi kumbeba huyo magufuli wenu
 
Nguvu ya uma isiyodhibitika ni mamlaka na hakuna anayeweza kuizuia na hilo lipo wazi. Tatizo ni kuitegemea kuingia ikulu bila kuwa na hakika kuwa uma upon tayari kuitumia.
Nani kakwambia kuwa Chadema hawapo tayari??? Wako tayari kimkakati na hata kiakili pia!!
 
Wanafahamu wanachokipata.
 
Unasema unataka aseme atafanyia nini taifa kwani huu uzi unahusu Sera za Nani????

Kweli Mataga mmechanganyikiwa Aisee. Poleni sana
Endelea tu kujitoa ufahamu utadhani na wewe umekuja toka ubeligiji juzi juzi umeshaisahau tanzania! Haki ya mbongo mwaka huu wehu kutoka mtaa wa ufipa mtaongezeka sana mtaani!
 
Weka mikakati wazi utafanikishaje hayo unayoyahadi. Wansema," Chadema itaboresha mazingira ya uwekezaji" kwa namna gani!? Mtagawa vitaru vya uwindaji bure, mtagawa machimbo ya madini bure, mtaruhusu wamiliki wa shule binafsi wajipangie cha kufanya Kwenye shule hizo bili kuingiliwa na mamlaka za serikali!?... Ebu fafanua utekelezaji wa hata mnayoahidi.
 
Mlisema tarehe 27/2/2020 Lissu atapokew mtandaoni ila salamu mlizipata. Unazungumzia Sera kwani huu uzi uliochangia humu unahusu Sera za nani??? Hizo ndo sera za Lissu na hizi ndo Sera za Chadema!!
Hapo kwenye tarehe sijaelewa mkuu! Kulikuwaje siku ya 27 Feb 2020?
 
Hvi mwaka huu pia ufipa tutachenjia gia angani au barabarani? Maana yule sultani mwenyekiti chake hatabiliki !😁😁😁
 
Ajab ya mambo yetu
Cku hzi Tume Huru Ya Uchaguzi sio Ajenda Tena
 
Nani kakwambia kuwa Chadema hawapo tayari??? Wako tayari kimkakati na hata kiakili pia!!
Sijasema chadema hawapo tayari, nimesema uma wa Tz bado hakuna uhakika kuwa upo tayari kwa hilo linaloandaliwa. Kuna vipimo vinavyopima hatari ya machafuko na mpaka sasa vipimo havionyeshi hali ya hatari. Ndio hali inaweza kubadilika lakini mamlaka nayo inajiandaa kuhakikisha hali inabaki kuwa shwari.
Karata ya nguvu ya uma ni karata isiyo na uhakika japo inawezekana.
 
Nchi ya ahadi. CCM wanatuweza wapiga kura kwakwel.. unapigwa propaganda adi unatia dole gumba lako CCM then tunazisubiri ahadi..
 
Kwani Malawi upinzani uliposhinda kulikuwa na Tume huru??? Mtajua hamjui mwaka huu! Subirini
Yaani nina wasiwasi na uelewa wako. Kwa hiyo wewe unadhani Malawi ndiyo mara yao ya kwanza kuweka upinzani madarakani? Pia usifananishe mfumo wa siasa wa Malawi na Tanzania ni vitu viwili tofauti sana. Tena kwa malawi ni kama wananchi wameamua kuirudisha ccm madarakani baada ya upinzani kupewa nafasi ya kuongoza nchi na kuboronga. Kila kitu kina mizizi yake! Nakutakia ndoto njema karibu kunapambazuka!
 
Kwanza u naelewa nini unaposikia kwa kushirikiana na sekta binafsi

Moja chadema itahakikisha kuna certainty na predictability kwenye sera za uwekezaji na hili wataliweka kimfumo na kisheria ili mwekezaji akija asiwe na hofu ya kesho sera zitabadilika au atakuja kiongozi wa serikali na kumtolea matamko yasiyo na kichwa wala miguu

Pili Chadema itatangaza Rasmi kukaribisha uwekezaji kwenye sekta zote hizo. Uwekezaji unaompa amani mwekezaji na kumuondoa hofu ya kusumbuliwa na mamlaka. Sekta zote zitakuwa huru kwa mwekezaji kuja na kuwekezana aliweka mtaji wake atawasilisha business plan yake inayomwekea namna ya kupata faida na kulipa kodi stahiki. Namna atavyotoa Ajira kwa wazawa na serikali utasema commitment ya kumlinda na kuulinda huo uwekezaji wake.

Tatu mfumo wote wa uwekezaji utabadirishwa. Kusajili na kupata vibali vyote na leseni kwa mwekezaji hakutazidi kipindi cha wiki tatu.

Pia suala la kodi litawekwa wazi Kwa kumuondolea bughuza zote na kuhakikisha analipa kodi zote kwa kipindi sahihi. Hakutakuwa na kuwafungia wawekezaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…