mbuyake
JF-Expert Member
- Feb 20, 2013
- 293
- 510
Kuna jamaa tulifanya biashara ya kumuzia tovuti ya biashara. Alitanguliza nusu ya malipo, lakini alipoenda kumalizia, akaghairi na kuhitaji hela zake. Kiukweli, niliuza tovuti hiyo kwa sababu ya shida, nikamwambia sina hela hadi nitafute, na nitamrudishia bila ya kukata gharama ya usumbufu.
Niliahidi kumpa nusu ya Shilingi 300,000 mwezi huu na kumalizia mwezi ujao. Kabla ya siku iliyopangwa, nilimpa Shilingi 100,000 na tulipoenda kwa balozi kuandikiana, tulifanya hivyo.
Sasa tarehe ya kumpa Shilingi 50,000 imefika, na amekuwa kero akituma vitisho hadi nimeghadhabika jioni hii. Amefikia hatua ya kuleta mganga akidai anaonyesha ofisi yangu.
Je, unanishauri vipi kuhusu huyu jamaa?