Kwa jinsi hali ilivyo nchini, ukipewa nafasi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria utabadili nini kuongeza Uwajibikaji na Haki?

Kwa jinsi hali ilivyo nchini, ukipewa nafasi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria utabadili nini kuongeza Uwajibikaji na Haki?

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kama leo imetokea umepata nafasi ya kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, ukangalia hali ya masuala ya Kisheria nchini pamoja na mfumo wa utoaji Haki, utaanza na mabadiliko gani ili kuongeza Haki na Uwajibikaji nchini?
 
Ukiangalia kwa sasa nchini ni WANASIASA TU TENA WA NGAZI YA JUU NDIO WANAONEKANA WANA HAKI ZAIDI JUU YA SHERIA ZILIZOPO yaani hata wakikosea hakuna mamlaka ya kuwaadhibu au kuwawajibisha ipasavyo, wakitunga sheria mbovu hakuna kuwajibika ipasavyo kikatiba nknknk.Hivyo kuna ulazima wa kuiangalia katiba yetu na kuona namna nzuri ya kuibadili au kurekebisha.

Sheria za ndoa , sheria za watoto ziangaliwe au nitaziangalia hata hizi sheria za HAKI sawa hizi nitaziangalia kwasababu zimeanza kuleta tatizo kwenye jamii zetu mpaka inafikia mahali hata ubaguzi wa kijinsia umeanza UPYA KWA WATOTO WA KIUME NA WANAUME HALI INAYOHATARISHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA NA ONGEZEKO LA SINGLE FAMILY SINGLE MAMA NKNK.HAKI YA DEMOKRASIA NITAANGALIA NAYO PIA KISHERIA NK.

Ila ukweli ni kuwa mnaweza kuwa na sheria nzuri sana ila inategemea nani anaisimamia kwenye utekelezaji wake. Mnaweza kuwa na sheria mbaya sana kama alivyosema Mwl Julius Kambarage Nyerere juu ya ubaya wa katiba yetu LAKINI ALIYEPO MADARAKANI AKAWA HAIKUBALI HIYO KATIBA YENYEWE. HIVYO KUNA MUDA INATEGEMEA ILA KAMA NIKIWA MIMI NDIO WAZIRI NITAFANYIA KAZI SEHEMU ZOTE MUHIMU KATIKA KATIBA.
 
Kama leo imetokea umepata nafasi ya kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, ukangalia hali ya masuala ya Kisheria nchini pamoja na mfumo wa utoaji Haki, utaanza na mabadiliko gani ili kuongeza Haki na Uwajibikaji nchini?
Ni Kubadilisha Katiba ya nchi iliyopo pamoja na Sheria zingine zote zilizopo hivi sasa hapa Tanzania na kuigeuza nchi yote kuwa nchi yenye Utawala wa Kidemokrasia na unaofuata mfumo wa Utawala Bora wa Sheria.

Haki na Demokrasia huwa havikai pamoja na Utawala wa Kijamaa/Kikomunisti, never.
 
Achana na haki mkuu....
Hii nchi ili iendelee kwanza inatakiwa demokrasia ifutwe, then hukumu ya kunyongwa hadharani hadi kufariki irudishwe kwa makosa ya ufisadi, wizi wa mali za uma, rushwa, ubadhirifu, ujambazi, utakatishaji fedha, kutokuwajibika kazini/kodi/malezi, drugs dealers, ushoga/ufirauni/usagaji na kadhalika na kadhalika...
 
Abdul S Naumanga kuna hoja inakuhitaji huku
😀😀 Nadhani hili nimeligusia kwenye Thread: 'TANZANIA MPYA: Taifa Lenye Raia Wanaojiamini Wenye Kuleta Maendeleo' lakini hapa point kubwa ni Kushirikiana na wizara ya elimu kwaajili ya kuweka moduli za kisheria katika somo la Civics (uraia) ambalo hufundishwa kwanzia darasa la kwanza mpaka form 6 as "General studies (GS)".

Binafsi sioni sababu za kuweka moduli za uchumba (courtship) katika somo hili na kuacha kuweka nondo za maswala ya kisheria na haki za binadamu kama vile mpangilio wa mahakama (court hierarchy) , mamlaka za mahakama (court jurisdiction), aina za kesi n.k

Naamini kwa kufanya hivyo, Tanzania utaongeza uwajibukaji na haki kwani nchi itakua na msingi mathubuti ya uelewa wa maswla ya sheri na utawala bora.​
 
Back
Top Bottom