Kwa jinsi Simba wanavyobebwa nashauri wapewe kombe

Kwa jinsi Simba wanavyobebwa nashauri wapewe kombe

Acha siasa
Makosa aliyofanya refa yameibeba timu. Goli lile ndio lililoamsha morali ya Simba huku ikiishusha morali ya Polisi Tanzania. Tuje kwenye upande wa maamuzi yaliyoionea Simba, je ukiacha mechi dhidi ya coastal Union je ni mechi ipi nyingine simba walionewa? Maamuzi ya kuwabeba simba yamekuwa mengi sana kuliko maamuzi ya kuonewa.

Turudi kwa upande wa Yanga:

Yanga pia wameathirika na maamuzi mabovu ya waamuzi. Kuna maamuzi yaliyoyabeba na kuna maamuzi yaliyowaonea. Mechi dhidi ya Mtibwa kuna filimbi nyingi walizopigiwa mtibwa kuashiria kuwa wameotea wakati hawakuwa kwenye offside position. Lakini pia kuna filimbi iliyopigwa kwa Yanga kuashiria ni offside wakati haikuwa offside na mchezaji alikuwa kwenye position ya kufunga na kuna penati ya wazi walinyimwa baada ya kipa kumchezea vibaya Sibomana.

Wote Yanga na Mtibwa waliathirika kwa maamuzi mabovu ya marefa japo mtibwa walioneshwa filimbi nyingi za offside. Mechi dhidi ya Prison yanga alipata penati iliyokuwa na utata hasa baada ya tukio kama hilo lilifanywa na beki wa Yanga (Jafarry Mohamed) lakini tukio alilolifanya Jafarry Mohamed lilikuwa nje ya box hivyo ingekuwa ni faulo ya kawaida. Kuibadilisha nafasi kuwa goli nii asilimia 50 kushuka chini.

Ukichukua idadi ya mechi ambazo yanga yamenufaika kutokana na maamuzi yasiyo halali ni ndogo kulinganisha na maamuzi yasiyo halali yaliyoionea Yanga.

Simba anaongoza kwa kupata magoli yasiyo halali yanayopelekea kuamua matokeo ya mechi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni kwamba marefa ni wa hovyo mno na tatizo hili halijaanza leo. Mechi za yanga pia kunakuwa na offside za uongo, rejea mechi za prison, mtibwa. Kama kweli tunataka mabadiliko kwa waamuzi basi ijadiliwe ubovu wa waamuzi na si kubebwa kwa simba.
 
Hapa Duniani Hakuna Mashabiki vichwa Maji Kama mashabiki wa Yanga hizi lawama zilishawahi kutolewa kipindi cha nyuma na Simba lakini wao walikuwa wanaleta kejeli na kushangilia Haji Manara alipowaita waandishi wa habari akiwa na Runinga kuonyesha makosa ya waamuzi wetu mashabiki wa Yanga walimkebehi na kumdhihaki leo kibao kimegeuka wamesahau kila kitu kila siku wao ni Malalamiko na vilio kwa TFF juu ya waamuzi. Sasa huu ni mwanzo tu Mbeleko zaidi Zinakuja kama inawauma hamisheni timu yenu mkashiriki ligi ya msumbiji sababu hii Mbeleko itaendelea mpaka 2030.
Mnadhani msomali ataendelea kuwepo? Kinachonipa raha mkienda kule mechi moko tu nje! Mkivuka kidogo hamsa bin sufuri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilichukua dakika ngapi bocco kupewa pasi?
Unaona kabisa bocco anatoka nyuma na mabeki wanamtegea kumkaba ili iwe offside unataka refa afanye nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Jikite kuangalia mieleka tu, huku kwenye soka sio kwako! Ile ya Boko hata mtoto wa chekechea anajua ni offside! Kubali kuwa mlibebwa hakuna atakayefuta matokeo na 'ubingwa' mtapewa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kwa lipuli lile goli au kona

Haaaahaaaa timu za simba na yanga bhana zinafurahishaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Marefa wetu sio competent kabisa,kila mechi ininyoangalia inakuwa na makosa mengi sana!Yaani kila nikiangalia mechi yeyote ya TPL basi lazima nikereke na waamuzi,pia mimi ni mfuatiliaji mzuri wa Kipyenga cha mwisho na Othuman Kazi!Kiukweli marefa wetu wanapaswa kujisahihisha kwa kuangalia hicho kipindi maana jamaa anachambua vyema sana sheria na kuonesha udhaifu kwenye maamuzi ya mechi za TPL!
 
Vipi wameanza kufunga kwa mikono, kama Hamis Tambwe au.?
 
,
Nikajua video uliyoleta ina sahihisha utata uliopo kuwa lile ni goli au sio goli. Kumbe ni video ile ile ya replay tu hakuna jipya. Hapa inahitajika video inayo clear doubt, yaani ioneshe position ya mpira ulipo kisha uchorwe mstari unaougawa goli (goal line) ili tuweze kuona kama mpira ulivuka mstari au lah!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom