Makosa aliyofanya refa yameibeba timu. Goli lile ndio lililoamsha morali ya Simba huku ikiishusha morali ya Polisi Tanzania. Tuje kwenye upande wa maamuzi yaliyoionea Simba, je ukiacha mechi dhidi ya coastal Union je ni mechi ipi nyingine simba walionewa? Maamuzi ya kuwabeba simba yamekuwa mengi sana kuliko maamuzi ya kuonewa.
Turudi kwa upande wa Yanga:
Yanga pia wameathirika na maamuzi mabovu ya waamuzi. Kuna maamuzi yaliyoyabeba na kuna maamuzi yaliyowaonea. Mechi dhidi ya Mtibwa kuna filimbi nyingi walizopigiwa mtibwa kuashiria kuwa wameotea wakati hawakuwa kwenye offside position. Lakini pia kuna filimbi iliyopigwa kwa Yanga kuashiria ni offside wakati haikuwa offside na mchezaji alikuwa kwenye position ya kufunga na kuna penati ya wazi walinyimwa baada ya kipa kumchezea vibaya Sibomana.
Wote Yanga na Mtibwa waliathirika kwa maamuzi mabovu ya marefa japo mtibwa walioneshwa filimbi nyingi za offside. Mechi dhidi ya Prison yanga alipata penati iliyokuwa na utata hasa baada ya tukio kama hilo lilifanywa na beki wa Yanga (Jafarry Mohamed) lakini tukio alilolifanya Jafarry Mohamed lilikuwa nje ya box hivyo ingekuwa ni faulo ya kawaida. Kuibadilisha nafasi kuwa goli nii asilimia 50 kushuka chini.
Ukichukua idadi ya mechi ambazo yanga yamenufaika kutokana na maamuzi yasiyo halali ni ndogo kulinganisha na maamuzi yasiyo halali yaliyoionea Yanga.
Simba anaongoza kwa kupata magoli yasiyo halali yanayopelekea kuamua matokeo ya mechi.
Sent using
Jamii Forums mobile app